Kwanini Vatican haitambuliki na UN?

Vatikanil City ni taifa huru na pekee duniani ambalo limeamua kutokuomba uanachama UN. (Kumbuka kuwa mwanachama UN sio lazima).

Vatican City, pamoja na nchi nyingine ndogo za Ulaya kama Monaco, Andora, Liechtenstein na Malta ni nchi huru kabisa (sovereign states). Sema kutokana na udogo wao na maeneo yao kijiografia baadhi zina mikataba ya ushirikiano ya karibu sana na majirani zake kiasi kwamba watu hudhani ni nchi moja.

Mfano Vatican na Italy, Monaco na France, Liechtenstein na Switzerland n.k.

Vi nchi hivi vidogo vinashirikiana na hayo mataifa makubwa kwenye maeneo ya ulinzi, fedha, uhamiaji n.k.

Kwahiyo kwa kumalizia, Vatican City ni sovereign state, wao wenyewe ndio wameamua kutokuwa wanachama wa kudumu wa UN japo ni moja ya nchi waangalizi UN (observer state).

Maelezo zaidi soma the Lateran Treaty.
Vatican siyo nchi, ni mji ndani ya nchi ya Italy ambao ni makao makuu ya Kanisa Katoliki.
 
Mm nashangaa ukiristo umeanzia israil huko middle east alafu makao makuu ya ukatoriki uko itali ndo napata mashaka makubwa na wazungu na ukiristo....
Ukatoliki ni sehemu tu ya Ukristo, ni dhehebu moja hilo ila madhehebu mengine yana makao makuu yao sehemu tofauti tofauti duniani.
 
Vatican sio nchi ni mji Mtakatifu, wenye hadji ya nchi kimataifa na Balozi nchi zote duniani ila sio dola; hauna polisi, jeshi, sarafu, nchi yenye dola inayotambuliwa ni Italy. Vatican ni mji mtakatifu.

Kule UN utambuzi ni wa dola tuu, ndio maana hata Zanzibar haitambuliwi kimstaifa.

P
Vatican ni nchi kama zilivyo nchi nchingine.Ina sifa zote za kuwa nchi(Westphalia Treat).
 
Kwa hiyo katiba ya Zanzibar inavunja katiba ya JMT ?

JokaKuu Kalamu
Mkuu 'Proved', kwa hili ingefaa umwite Nguruvi3.

Maoni yangu juu ya huu Muungano, naona kama Zanzibar inaelekea kuitawala Tanganyika. Sielewi hatma yake itakuwaje.

Muungano haukuundwa na malengo haya tunayoyaona hii leo.; ya nchi moja kubaki na utambulisho wake na kufanya mambo yake, huku ikifaidi faida zote za muungano, wakati nchi nyingine ilipoteza kabisa utambulisho wake na watu wake hawana haki sawa na wale wa nchi nyingine.
 
Kwani zanzibar ni nchi?
Yes Zanzibar ni nchi ndani ya nchi, kitaifa Tanzania japo ni nchi moja ya JMT, ndani ya JMT kuna nchi mbili, Tanzania bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, tuna serikali mbili za SJMT na SMS, tuna marais wawili, mabunge mawili, na Mahakama mbili. Hivyo ndani ya muungano wetu ni muungano wa federation.

Nje ya muungano, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye muungano wa union wenye rais mmoja, rais wa JMT na Amiri Jeshi Mkuu, ina serikali moja ya JMT, Bunge moja, Mahakama moja.
P
 
Back
Top Bottom