Kandarasi wa Barabara hii ni Kaserkandis construction, ni kilomita 23 tu kutoka Tamco/Vikawe hadi unatokezea Mapinga/Bunju.
Barbara hii ni muhimu sana kwani ndio kiunganishi cha wilaya ya Bagamoyo na makao makuu ya mkoa yaliyopo Kibaha lakini ujenzi unasuasua sana, Kandarasi yupo site lakini kila baada ya miezi 3 anajenga km 2 je kweli hizo km 23 zitaaisha kwa mwendo huo?! Au hadi aje waziri mkuu ndipo mchangamke?
Kama Serikali imewalipa fedha basi kuna haja ya kufuatilia kwa karibu ujenzi wa Barabara hii kwani hauridhishi kabisaa.
Wakazi wa Bunju na viunga vyake wanaitegemea sana barabara hii kwenda hospitali ya taifa Muhimbili Mloganzila lakini pia ni shotkati ya kwenda stendi kuu ya mabasi Magufuli, bado ni barabara mbovu na hivyo kukwaza shughuli za kiuchumi.
Tunaomba barabara hii ikamilike kwa wakati, kama kandarasi hajalipwa basi alipwe, kama kalipwa basi viongozi wa Tanroad mkoa wafuatilie kwa karibu.
Hicho ni kilio cha wananchi wa Bagamoyo, Mapinga, Kerege, Bunju, Vikawe, Kidimu n.k.