Kwanini Serikali ilianzisha miradi mikubwa Kwa fedha ambazo hazipo?

Ntozi

JF-Expert Member
Feb 1, 2021
226
299
Ukisikiliza kinachoongelewa juu ya mikopo ya nchi Kwa sasa,unagundua kuwa serikali ilianzisha miradi mikubwa kama SGR,Kwa fedha ambazo hazikuwepo.

Yaani ina maana serikali ilitegemea itakopa ili kukamilisha hiyo miradi?

Walijuaje kuwa wataupata huo mkopo?Ina maana walikuwa tayari kuja kukubaliana na masharti ya huo mkopo?Maana kinachoongelewa kwa sasa ni kwamba lazima tukope ili tukamilishe miradi.

Kinachowachanganya watu huku uraiani ni kwanini gharama ya maisha imekuwa juu Sana ghafla hivi? Mkuu wa nchi anaelezwa ukweli wote juu ya maisha ya watu huku mitaani?

Tozo zimetamalaki kila mahali ambazo zinalipwa na mwananchi kiasi kwamba ukiwatazama watu,huioni Amani tunayojifariji kuwa tunayo,bali unaona hofu.

Haya malumbano miongoni mwa wanaccm waandamizi, ni ishara ya uchungu utakao zaa yasiyotarajiwa. Mungu atunusuru.
 
tozo= samia erra.

jpm alikopa ila speed ilikuwa ndogo sababu mwamba alikuwa yuko makini sana kwenye matumizi,angalia bibie.miezi 10 tu kashamfuta jpm kwa 45%.
 
Back
Top Bottom