Kwanini Rais anatudanganya?

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
1: asiyetaka kulipa 200 na apige mbizi kuja posta. Kilichofuata kununua boti chakavu kwa mabilioni pamoja na kukusanya hiyo 200.

2: Matajiri waliishi kama malaika nitahakikisha wanaishi kama mashetani. Kilichofuta walioficha pesa wazitoe niwape maeneo wajenge viwanda.

3: Walioficha sukari wala hawazidi kumi nitawashugulikia kweli kweli. Kilichofuata TPA mpeni sukari yake Bakhiresa wala isilale leo.

4: Mafisadi wakinishinda msiniite Rais . kilichofuata wazee wangu nitawalinda.

5: Kuna watu walisafiri sana kwenda ulaya kuliko walivyosafiri kwenda kuona wazazi wao nyumbani. Kilichofuata hata Bukoba hajafika pamoja na kuwa ni karibu na nyumbani.

6: Watu watetemeke kujenga Nyumba zao wasisubiri serikali tetemeko alijaletwa na Ccm. Kilichofuata ni kuwakamata wapinzani wanaotoa misaada na kuwahoji na kuwazuia..

7: Waliofukuzwa udom ni Vila.za waende watafute vyuo size yao. Kilichofuata msinidrive msinidrive wakati Jesca mtoto wake yupo Udom wakati na yeye ni kilaz.a

8: Wanaolalamika walizoea vya bure nitaendelea kuwashugulikia kweli kweli . kilichofuata kutoka bank kuu na bandari hali ya uchumi ni mbaya sana .

9:Nasikia kuwa watalii wanakuja na kukomea kwenye vinchi vya ajabu ajabu. Kilichofuata KDF wakapeleka misaada kagera kabla hata ya Serikali kufika.

10: Ningelikuwa Mimi ningeliwapoteza karibu nusu yao . kilichofuata bado tunakisubiri kama anaweza au laa.

Kuweka matumaini kwa kiongozi kinyonga kama huyu inaitaji moyo wa chuma ..

Alafu ndio eti anatupeleka kwenye serikali ya viwanda sitaki hata kuamini ..

1477462296126.jpg
 
Who are you kutaka kumuita rais wetu muongo? .

Jee wajua kwamba, kumuita rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwa ni muongo ni kosa la jinai la kumchonganisha na wananchi wake walimchagua kwa imani kubwa kufuatia ahadi hizo? .

Jee alipoahidi yote hayo, alitoa time frame?.
Acha kumuita rais wetu muongo, ahadi zote alizotoa zitatekelezwa tuu in due time hadi kufikia 2020 zote zitakuwa zimekamilika.

Pasco
 
raisi aliepoteza mvuto na kuchokwa mapema kushinda maraisi wote,japo alikuwa na ahadi motomoto kushinda hata za ari mpya nguvu mpya na kasi mpya...!!!mpaka sasa sina uhakika kama alishinda kweli
WELL SAID MKUU
 
11. serikali yangu haitakuwa ya michakato... kilichofuata tangu mwezi Wa 4 hadi Leo mchakato Wa watumishi hewa haujaisha...

12.nasitisha nyongeza za mishahara, upandaji Wa vyeo na ajira mpya kwa mwezi mmoja au mmoja na nusu Haitazid miwili.. kilichofuata.. hadi Leo miezi miwili haijaisha
 
Back
Top Bottom