Kwanini Ndoa Hazidumu?

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
"Unapo oa au kuolewa unaapa upendo na kutarajia maisha ya furaha kwa wakati ule na ujao, ingawaje mambo yamekuwa tofauti kwa siku za hivi karibuni".
Anasema Rodney Simmons, mwandishi wa masuala ya mahusiano katika jarida la Tiny Changes Matter.

Rodney anasema ndoa sio taasisi imara Kama ilivyokuwa zamani kwani utamaduni wa sasa umeathiri ndoa na kufanya ndoa nyingi zisidumu.

Tafiti nyingi zinazofanyika duniani kote zinaonyesha misokosuko na migogoro inayozikumba ndoa na kupelekea talaka.
Utafiti unoanyesha katika kila ndoa 10 zilizofungwa ndani ya mwaka mmoja, ndoa nne zina migogoro au zimevunjika kabisa, ikiwa ni wastani wa 4.80 kwa ndoa 1000.

Sababu kadhaa zinatajwa kuwa kichocheo cha ndoa hizo kuvunjika.
Kutoheshimiana baina ya wanandoa kunatajwa kuwa sababu kubwa inayopelekea talaka kwani ni vigumu watu wawili kuishi kwenye uhusiano pasipo kuheshimiana, hivyo mmoja huamua kutafuta heshima nje ya ndoa na ndoa yake ya awali inavunjika.

Kukosekana kwa umoja na utofauti wa viapumbele katika ndoa ni sumu nyingine inayoteketeza ndoa nyingi.
Baadhi ya wanandoa hukosa umoja hasa kuwa na mtazamo wa pamoja pengine kuhusu maisha hivyo hujikuta wanaishi kwa kutokubaliana.
Mwanamke anaweza kuwa na viapumbele vyake na mume hivyo hivyo jambo ambalo linahatarisha ndoa yao.

Sababu nyingine iliyofanyiwa utafiti ni baadhi ya wanandoa kuingia katika ndoa wakiwa bado hawajakomaa vya kutosha kuwa na uwezo wa kuhimili changamoto za ndoa.
Kutokana na mabadiliko ya kitamaduni hakuna maandalizi na mafunzo ya kina kwa vijana wanaojiandaa kuingia kwenye ndoa hivyo wengi wao hukosa misingi imara ambayo ingewaongoza.

Mabadiliko ya Kiuchumi ni sababu nyingine iliyofanyiwa utafiti na kuonyesha kuwa baadhi ya ndoa huvunjika kutokana na hali ya Kiuchumi hususani pale mwanaume anapoanguka Kiuchumi wanawake hukosa uvumilivu na kuamua kundoka ndoa inavunjika.
Aidha wanaume wengine wanapofanikiwa Kiuchumi huamua kubadili wake kwa kuachana na mke wa awali na kuoa mwingine kwa kisingizio cha kutoendana hadhi.

Sio hivyo tu, utafiti unaonyesha kuwa "pesa ya mwanamke huondoa kichwa cha familia" iwapo mwanamke akafanikiwa Kiuchumi na akawa na kiburi basi atamdharau mume wake na ndoa inapoteza amani kisha kuvunjika.

Ushawishi na usaliti ni matokeo ya utafiti ambapo imeonekana kuwa baadhi ya wanandoa husaliti ndoa zao baada ya kushawishika na watu wengine kwa vigezo mbalimbali.

Pia imebainika kuwa kukosekana kwa uvumilivu na uaminifu ni chanzo kikubwa cha ndoa nyingi kuvunjika, iwapo mwanandoa atashindwa kuvumilia madhaifu ya mwenzake basi ndoa itavunjika.

Uwepo wa msukumo kutoka nje ya ndoa ni miongoni mwa mambo yanayopelekea ndoa kuvunjika, msukumo wa wazazi wa pande zote mbili unaweza kupelekea mwanandoa kuamua kuiacha ndoa yake.

Utafiti unaonyesha kuwa kuongezeka kwa mahubiri na semina za mafundisho kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo mahusiano ya ndoa na miujiza ya mafanikio kumepelekea baadhi ya ndoa kuvunjika.
Baaadhi ya wanandoa baada ya kuhudhuria mafunzo na mahubiri hayo hujihisi hawapo sehemu sahihi katika ndoa zao hivyo wanabadilika na kuamua kutafuta wenza wapya watakaokidhi matakwa ya yale waliyojifunza.

Matumizi ya mitandao na maendeleo ya utandawazi yameonekana kuwa chumvi kali inyotiririka kwenye kidonda cha ndoa nyingi.
Sababu zingine zilizofanyiwa utafiti ni ubishi, misimamo iliyopitiliza, ukaidi, ulevi, kiwango cha elimu na Kadhalika.

Hata hivyo kwa wakati wa sasa bado Kuna ndoa nyingi ambazo zipo imara kiasi kwamba zinaweza kutumika kama kioo kwa wanandoa wengine kujifunza.

Peter Mwaihola
Photo_1682356658444.jpg
 
Alhamdulillah namshukuru maulana kwa kunipa a husband huyu,naamini tutazeeka pamoja inshAllah.namwelewa yeye pamoja na mapungufu yake...... from my experience HESHIMA is everything,both sides.hii itawajaalia uvumilivu na utulivu.upendo na amani vitatawala.hofu ya kila mmoja kumpoteza mwenzie,sio kwa sababu ya watoto no kwasababu hujioni mtu mkamilifu bila mwenzie.
 
Alhamdulillah namshukuru maulana kwa kunipa a husband huyu,naamini tutazeeka pamoja inshAllah.namwelewa yeye pamoja na mapungufu yake...... from my experience HESHIMA is everything,both sides.hii itawajaalia uvumilivu na utulivu.upendo na amani vitatawala.hofu ya kila mmoja kumpoteza mwenzie,sio kwa sababu ya watoto no kwasababu hujioni mtu mkamilifu bila mwenzie.
Mashaallah mna muda gani kwenye ndoa?
 
Alhamdulillah namshukuru maulana kwa kunipa a husband huyu,naamini tutazeeka pamoja inshAllah.namwelewa yeye pamoja na mapungufu yake...... from my experience HESHIMA is everything,both sides.hii itawajaalia uvumilivu na utulivu.upendo na amani vitatawala.hofu ya kila mmoja kumpoteza mwenzie,sio kwa sababu ya watoto no kwasababu hujioni mtu mkamilifu bila mwenzie.
Kama hutaleta wenge mtazeeka wote. Ila siku mwenyekiti wa kikoba chako akianza kuwapa seminar za kuwa mnaweza bila waume zenu na zikakuingia, mtazeeka mmoja akiwa dar na mwingine kigoma
 
Unaambiwa kabla ya kuoa jaribu kwanza kufuga mbuzi,ukiweza kumfuga mbuzi basi hata mwanamke unaweza kuishi nae.

Kwa mimi mbuzi walinishinda hivyo siwez kuoa,
naunga mkono hoja ya KATAA*NDOA ndoa ni utumwa
 
Back
Top Bottom