Kwanini namuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan?

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Kumekuwa na maneno maneno humu kuwa mimi na wenzangu tunaomuunga mkono Rais Samia basi kama sio Waislamu basi ni Wazanzibar na kama hauko kote huko basi wewe ni chawa wake.

Hizi ni siasa za majitaka ambazo kusema kweli zimeegemea kwenye vihoja badala ya hoja.

Kwa upande wangu Mimi Lord Denning, mimi sio wa asili wa Zanzibar wala sio muislamu. Ni mkristo mkatoliki na kusema kweli simjui Rais Samia, Sijawahi onana nae na wala hanijui.

Katika uzoefu wangu wa kufuatilia siasa za dunia ikiwemo Afrika na Tanzania naweza kusema Mimi Lord Denning naweza kuwa mmoja wa watu wachache sana wanaoifahamu dunia na siasa zake. Kwa umri wangu wa miaka 47 sasa nimeenda nchi nyingi, karibu mabara yote. Na kote huko nilikofika nimekuwa nikijifunza sana historia ya sehemu husika, siasa zake, maisha ya watu na uchumi wao

Kwa upande wa marais wa Tanzania nimebahatika kuwepo kipindi cha Nyerere ingawa nilikuwa mdogo, kipindi cha Mwinyi nikiwa na akili, kipindi cha mkapa hadi saivi nikiwa mtu mzima na akili zangu.

Nilimkubali sana Mkapa na sera zake za kiuchumi. Nikamkubali sana Kikwete maana nae kwenye uchumi alienda sawa pamoja na kuyumba maeneo kadhaa na nikatofautiana na Magufuli hasa kwenye sera zake za kiuchumi za state capture na sasa namuunga mkono Samia kwa sababu so far nimemsoma na kumuelewa kuwa anaenda vizuri sana kwenye sera za kiuchumi.

Kwanini namuunga mkono Rais Samia?

1. Wanasiasa wengi wa nchi yetu ukiondoa Mkapa walikuwa wanaogopa kufanya maamuzi positive kweli kiuchumi kwa kuogopa siasa ila Samia hayuko hivyo. Kwa nilivyomsoma Samia, anajua sana geopolitics, anapenda vitu vizuri, ni mkisasa kweli. Kwa sasa dunia ilipo na inapokwenda fursa ziko kwenye maeneo hayo. Moja ni kwa namna gani unavyojiweka na kujitangaza vizuri na pili ni namna gani unavyojiweka kisasa. Kwa maamuzi ya kuboresha sekta nyeti za kiuchumi ikiwemo bandari, utalii tena bila kujali siasa, kusema kweli amenivutia sana.

2. Tanzania kuna wajinga wengi sana na ujinga wao umewafanya kuwa masikini sana. Katika kuwaondoa kwenye ujinga wao ni lazima uwaonyeshe kweli kuwa wanatakiwa kuondoka katika imani na mazoea ya kijinga. Kwenye hili kusema ukweli wa Mungu wangu Samia anafanya vizuri.

Mabadiliko yanayofanyika katika uendeshaji wa uchumi wetu ili kutufanya tuendeshe uchumi katika mazingira yenye ushindani ili kupata matokeo mazuri kweli yamenifanya nijitokeze wazi kumuunga mkono huyu Mama.

Tanzania shida kubwa iliyopo ni watu kutopenda ushindani. Na ndo mana ubora katika mashirika ya Umma umekuwa finyu sana. Kutufanya tuondokane na mentality hii inanifanya kumuona Rais Samia kama Rais bora zaidi kuwa nae katika kipindi hiki.

Mwisho napenda kumaliza kwa kusema uongozi na maendeleo ya kweli ni matokeo ya kutumia akili vizuri. Sio rasilimali wala sio utajiri ulio nao kama Taifa. Kuna sehemu Tanzania tunatakiwa kufika ila ili tufike lazima tutumie kweli akili zetu vizuri hasa katika kujua Dunia ipo wapi, inaenda wapi na itakuwa wapi katika siku nyingi zijazo.

Ili tufike huko lazima Watanzania tutumie akili zetu vizuri. Tuifanye nchi yetu kuwa sehemu ya mjadala wa dunia kama sehemu nzuri ya kuja, kuwekeza na kuishi ikiwemo kufanya starehe. Na ili tutimize hili lazima tuite watu wenye akili tofauti, wabadirishe fikra zetu, na watufanye tuwaze vizuri. Ni lazima tubadiri mfumo wa elimu yetu ili kutufanya tuende kama dunia inavyoenda ili tusiachwe nyuma.


Asanteni
Lord Denning
Kilimanjaro
 
Tunaomkosoa pia tunaompenda,

Yaani Dubei wamepata wapi experience kimazingira kutuelimisha kuhusu misitu au wanyama hai?

Wasiwasi ndiyo akili, na ni kheri nusu shari kuliko Shari kamili.
Ni sawa pia
Ila kwa taarifa yako sasa, Dunia imehamia Middle East. Kule ndo kwenye fedha na kule ndo kwenye picha halisi ya dunia iko wapi na inaenda wapi.

Ndo wanaendesha Dunia. Usishangae sasa wachezaji wanahamia Ligi ya Saudia.

Jifunze elimu haina mwisho
 
Back
Top Bottom