Historia nzuri. Ila nataka nikusahihishe kitu kidogo kwa nini mgodi wa Mwadui leo serikali ya Tanzania ina hisa 25% tu. Baada ya kuondoka Mr. Hunt na baadaye kuja wazelendo akina Rwakatare, halafu Mr. Manning, halafu Mr. Materu (? sikumbuki vizuri jina) mgodi ulizidi kudorora polepole. Mashine zilizidi kuwa mbovu na za kizamani. Mashine zile zilikuwa zinashindwa kuchambua vizuri almasi. Wafanyakazi wengi sana waliokuwa na uzoefu wa hali ya walikimbia Mwadui. Wizi ukawa unaendelea mtindo mmoja na hata kile kiwanda cha kuchonga almasi pale Iringa kikafa na wafanyakazi wake kukimbilia Botswana.
Alipoingia Mkapa katika jitihada za kufufua uchumi aliamua kufufua mgodi wa Mwadui. Aliwaalika De Beers kufanya kazi hiyo pamoja na kuchagua Mkurugenzi Mwendeshaji. De Beers walikubali lakini waliiambia serikali itoe nusu ya gharama na wao wangetoa nusu vile vile kwani wote walikuwa wanamiliki 50%. Serikali ya Tanzania ilikuwa haina pesa na ikaomba De Beers watoe hizo pesa ila hisa zake zipungue kutoka 50% hadi 25% na za De Beers ziongezeke kutoka 50% hadi 75%. Na ndiyo hali ilivyo leo japokuwa De Beers wameuza hisa zao kwa Petra.