KENGE 01
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 1,595
- 3,854
Anaandika Kenge
Kwanini mawazo ya biashara hasa kwa sisi fresh youth yanafanana sana? yani ukikamata vijana kumi wa kibongo ukawapa mtaji ukawaambia fanya biashara..Watakimbilia kufungua duka
Kuuza la Nguo
Kuuza Viatu
Kuuza simu,charger,Makava
kufuga kuku
kuuza Nafaka
KUuza Chakula,Vipodozi,Saluni n.k
Hakuna mtu kati yao atafanya kitu kipya kikakuimoress ata alietoa mtaji aseme hapa kweli nimewekeza kwa kichwa.
Hivi Ndo kusema mawazo yetu yameishia hapa au ndio kujificha kwenye ile sababu ya "TATIZO MTAJI"
OK!!Sikatai kuwa na wazo la kuuza nguo.Lakini jaribu kuwaza mbinu tofauti za kuuza nguo.
..Mfano
Mchina anatengeneza nguo pia lakini alipowaotea ni kwenye Custom logo yeye anatengeneza wewe unampa Logo yako anakuwekea Mzigo anakutumia..unakuza brand yako na Logo yako Taratibu..Mfano kina JUKSI na nguo za AFB B12 na Born2Shine..Fred na VUNJABEI(VB).Brand nyingi za nguo kama Essential hapa bongo nyingi ni fake mchina kaweka Logo na Ushamba wetu tunaona kuuza na kuvaa nguo latest zenye Logo kama Essential na Balanciaga au D&G,Nike,puma etc.THINK DIFFERENT,GROW RICH
Haya Hizi biashara nyingine za Chakula badala ya kujipa stress na kuwaza kupangisha Fremu,Kulipa wafanya kazi..Kwanini mtu asiwaze njia mbadala.Food mobile truck.Unajichanga unanunua Truck yako ndogo unapika chakula unafanya packaging unalipia eneo town unatenga Truck yako unauza msosi.Kwani wote lazima muwe na mafremu?.THINK DIFFERENT
ASilimia kubwa ya vijana kwasasa uhisi kulewa ndio ujanja.Bar bubu zinaongezeka kila uchwao.Mikoa ya pwani Joto ni kubwa Maji yanauzwa kwa sana kwanini Asitokee kijana akawaza kununua Vending Machine? Wala sio garama kama tunavyodhani..Na ni rahisi kabisa kutumia..Unakuta Jitu linawaza kufungua au linamiliki Bar limeweka Dubu(Mashine la kamari) halafu jitu limeshindwa kujiongeza kuweka Vending machine wakati zote zinafanya kazi sawa.Ni kukosa exposure au Tatizo nini haswa?Vending Zipo chache sana Bongo na wala hazihitaji usimamizi mkubwaa.Think different.
Wadada mnaowaza kuuza mavipodozi kwanini usiwaze kuwa na brand yako ya vipodozi..Mchina anakufanyia packaging anakuwekea Logo yako unauza huku unakuza brand yako.sabunizperfume n.k
THink different.
Changamoto zipo na hazikwepeki.Lakini mambo ya kutoautisha Biashara yanakwepeka Aisee unakuta Fremu kama Nane zote wanauza Bidhaa aina moja.Hapo lazima kuwe na unafiki,Kurogana,Fitna majungu n.k.Sasa kwanini usije na wazo lako jipya na biashara unique?
Jamaa mmoja niliona analalamika anauza Nguo Morogoro na mzigo hauendi kabisaa moaka anajikuta anakula mtaji..wakamshauri abadili location..Aisee hata ubadili location wauza nguo wamekuwa wengi mno kuliko wavaaji..Mwingine analalamika Bodaboda hapati kitu na mkataba umekaribia kuisha..wakamshauri badili location..Aisee ukweli ni kwamba Boda wamekuwa wengi mnoo hata ubadili location kila mtaa kila kata kila wilaya kuna Bodaboda..kiasi kwamba ukitoka tu getini macho ya boda yote kwako..kwanini kijana usiwaze biashara Mpya na unique?
THINK DIFFERENT,GROW RICH
Nawasilisha