Kwanini Mawaziri na Viongozi wa chama tawala wanapenda sana kuwatisha watumishi kwamba watawatumbua? Kila waziri anatamka kutumbua, hadi lini?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
891
4,150
Mawaziri na Manaibu kila wanapopita jambo dogo tu nitapendekeza utumbuliwe; wakuu wa mikoa nao kila wanapokwenda wanawaza kuweka watu ndani na kuwatumbua.

Ipo wapi team work tuliyofundishana kwenye utoaji wa huduma? Ipo wapi team work ndani ya taasisi za umma? Tunapata muda wakujadiliana? Kutumbua kunaleta maendeleo au kunaongeza gharama za uteuzi kila siku na kulipa watu mishahara wasiyoifanyia kazi?

Mbona wanasiasa wa nchi zilizopiga hatua wanaishi na watendaji walio chini yao kama timu moja na wanapata matokeo. Leo UN agencies gani umeona inatumbua mtumishi? Lakini nidhamu wanayo na wanatekeleza wajibu. Sisi kwetu shida nini?

Private sector viongozi wanakaa miaka bila kutishwa kutumbuliwa na performance ipo. Waziri anatumbua mtu leo kesho naye anatumbuliwa.

Wanasiasa BADILIKENI....hawa mnaowaona kama wajinga siyo wajinga . Wanafamilia kama zenu......heshimianeni mtaona kazi itakavyofanyika kwa ufanisi.
 
Mawaziri na Manaibu kila wanapopita jambo dogo tu nitapendekeza utumbuliwe; wakuu wa mikoa nao kila wanapokwenda wanawaza kuweka watu ndani na kuwatumbua.

ama wajinga siyo wajinga . Wanafamilia kama zenu......heshimianeni mtaona kazi itakavyofanyika kwa ufanisi.
Hizi hoja zisizo na mifano hai ni za kijinga sana.
 
Mkuu hawa wa vyeo vya Asante Mama na Madiwani wa lasaba c wanajionaga hawajawai kukusea Kuna mmoja alilazimisha jengo kujengwa kwa mwezi mwenge ukaja zindua sahivi limegeuka bwawa kwa kuvuja na rangi inabanduka Kama ngozi ya nyoka
 
Back
Top Bottom