Kwanini kuwe na naibu waziri wa katiba na sheria?

Msendekwa

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
442
168
Wanajamvi, nijuavyo mimi, waziri wa Katiba na Sheria amekuwa akisaidiwa na Mwanasheria mkuu wa Serikali(AG) km Naibu wake.
Kulikuwa na ulazima gn wa kumteua Angela Kariuki kuwa naibu tena?
Au mchakato wa Katiba mpya ndio umefanya kuwe na hitaji jipya la naibu waziri?
 
Kwa kuangalia hali halisi ya sasa naweza kusema kuwa hii wizara ni 'technically' ya muungano. Nasema hivyo kwa sababu tuko kwenye mchakato wa katiba mpya, katiba ya Jamhuri ya muungano na hii wizara itahusika sana kwenye huu mchakato. Sasa nilitegemea kama kuwa na naibu ama rais (a) angeteua Naibu toka Zanzibar au (b) angeteuwa manaibu wawili, mmoja toka Tanzania bara na mwingine toka Zanzibar.

Na hapa ndipo naona bado safu wa washauri wa Rais wanafanya kazi kwa mazoea bila ya kuangalia hali halisi on the ground.
 
Hilo la manaibu wawili hapana, kungekuwa na watu wanne kwa jambo moja!
Yule mzenj aliemteua mchana na kumpa unaibu jioni angempeleka katiba na sheria km kweli anataka kubalance muungano na wizara ni ya mambo ya muungano.
Bd kuna Chenge, ambae mara nyingi humsaidia AG bungeni, yani wizara ina watu kibao!
 
Angela Kairuki ni mtoto wa Asha Mkwizu, mama aliye karibu sana na JK! Mumewe Angela ni mwandishi wa hotuba z a JK. Siasa bana....nafasi za kupeana tuuuuu! Angekla Kairuki hana uwezo kihivyo, alipokuwa anafanya kazi ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali alikuwa mzigo na akasepa mwenyewe. Akaajiriwa Vodacom, huko akashindwa ku-deliver makaburu wakamkalia kooni akakimbilia kwenye siasa, kichaka kinachoficha kenge, fisi, mbweha n.k. Hakukuwa na sababu ya wizara hiyo kuwa na Naibu waziri. Lkn wangekula wapi?
 
Mkuu uadhani mziki wa Lissu pale bungeni ni mdogo??

Lazima wawe wengi ili wawe wanadesa!!
 
Back
Top Bottom