Kwanini kuna watu wanaweza kukufanya chochote wakati wowote!?Regardless

1120ulimwengu

Member
May 23, 2013
77
120
Salaam wanaforums!
Moja kwa moja kwenye maada,mwezi wa tisa mwaka 2023 nilipatwa na tukio ambalo halijawah kunitokea na nnahisi halitofutika maishani mwangu.Kwanza kabisa mimi ni mjasiriamali mdogo ambae nimejikita katika uuzaji wa pafyum za kupima.Huduma hii huwa naitoa kwa kutembeza mtaani(door to door delivery) sina kaz nyingine na makazi yangu huwa ni Mwanza.Nimekuwa nikifanya kazi hii kitambo sana na nimekuwa napita maofisi mbalimbali na karibu kila mkoa nimefika nikifanya kazi hii!
Wakati husika nilikuwa Geita na nilikuwa naendelea na kazi jirani na stendi ya mabasi ya Geita.Hapo kuna grocery ndogo na kuna mteja wangu wa zamani aliniita nimpe huduma na nilifika.Wakati nampimia pafyum(perfume mixing) bwana mmoja aliyekuwa mbali kidogo ameketi na wenzake wakinywa konyagi alinifuata.Nikiwa sina hili wala lile aliniuliza 'unafanya nini' nilimjibu nachanganya pafyum na nikamwambia process nzima.
Bwana huyu hakuridhika na majibu yangu aliendelea kunihoji kwamba nnakibali cha mwanakemia mkuu cha kuuza pafyum(kwa maelezo yake kazi hiyo inafanywa tu na watu wenye kibali).Nikiwa najiamini nilimueleza kinaga ubaga kwamba mm ni mjasiriamali mdogo na kwamba hizo pafyum nanunua kutoka maduka makubwa na kwa watu ambao Serikali imewapa hicho kibali,nilienda mbali na kumtajia mtu anayeniuzia ARISON MWENGE.Bwana huyu alimuita mwenzake na ghafla wakataka kujua nawauzia wakina nan nikawaeleza kuwa huwa nawauzia watu mbalimbali mtaani na hata kwenye maofisi na kwamba kama wao wapo kwenye maofisi huko pia napita nawauzia "HATA WAKUBWA WAO"!!
Basi ndugu hawa wakaona kujiamini kwangu kumepita kikomo wakaanza kunipiga kwa kunikanyaga usoni,kuniumiza kunirekodi kwenye simu zao na baadae kuninyang'anya simu yangu ya mkononi.Wakati wote huo sikuonesha resistance ya namna yyt,sikukataa matakwa yao na hasa waliposema watanipeleka mbele nilikubali lakini ajabu walinipiga.Baadae wakanichukua mpaka kituo cha polisi Geita.
Tukiwa kwenye bajaji walidai wanataka kunisaidia tuongee nikawaambia twendeni mbele tu,baada ya kufika kituoni wawili hawa walifika na kuongea na polisi waliokuwepo pale bila maelezo yyt niliamriwa kuvua mkanda na kuswekwa korokoroni(cell).Baada ya masaa mawili niliitwa na gari ya polisi ikanichukua mpaka guest kusachiwa na nilikutwa na nguo za kubadilisha na zenyewe zikachukuliwa moaka kituoni na mm kurudishwa ndani.Nilikaa humo kwa takriban siku sita.Nikiwa ndani mkuu wa kituo akija kucheki wahalifu alishangaa toka lini kuuza pafyum ikawa kosa,askari waliokuwa wanakuja kuchukua rollcall walikuwa wanashangaa kwann nimewekwa ndani baadae ilikuja kujulikana kwamba watu wale ni usalama wa Taifa kwahyo wanaamua wao NANI TUMUWEKE NDANI NA ATOKE LINI bila sababu bila kosa!.
Maafisa hao wawili ambao walisemwa ni maafisa USALAMA WA TAIFA mmoja wao anaitwa KIPEJA(wote wawili ni wahaya) na inasemekana mmojawao yupo MIGRATION Geita kama cover.Nnayo namba ya mmojawao,hapo baadae nitakuja kuiweka namba zao hapa.
Kwakuwa sikuwa na kesi wala hapakuwa na mlalamikaji sikupelekwa mahakamani na baadae polisi waliniachia(na kama ujuavyo hutoki freely) regardless.Begi langu dogo la vfaa vyangu vya biashara nilipewa almost miezi miwili baadae nikiishi kwa kuhangaika kwa kukosa kazi!Tukio lile la kionevu na lisilokuwa la kiungwana lilinitesa,linaendelea kunitesa na sidhan litafutika katika kumbukumbu zangu!Inanisikitisha kwamba nilifanyiwa uonevu ule na watu wanaodaiwa kuwa na legacy ya weledi na ambao hawapaswi kuwa low kiasi!The most thing I really regret is to not fight back when they were beating me like a thief or a robber,like a dog!Nadhan ningerudisha mapigo basi walau ningekuwa na kesi na sabab ya kuwekwa ndani at least mzani ungebalansi wa sabab ya kuwekwa ndani BT mimi siamini katika VIOLENCE thats why I choose to remain calm and cool despite kipigo kile walichonishushia!!!Ikiwa ningekuwa na nguvu ya kipesa kwasasa ningewashtaki maafisa hawa wanaodaiwa ni usalama wa Taifa(Even the police officers admitted that those two hooligans were TISS officers and therefore they couldnt offer anything on my side rather than waiting for them to be pleased with the time I'm remained in a cell)
For now,Sina cha kuwafanya BUT I WILL NOT FORGIVE and FORGET.
 
Pole sana sana. Endelea na maisha rudi ujenge yaliyobomoka utafanikiwa kwa bidii yako na Mungu awe nawe.
Hawa watu walio kudhuru ndio adui wakubwa wa watanzania. Wanaishi maisha ya juu kwa kodi yako wewe unae henyeka juani kutaka kupata tonge.
Hawa ni tatizo kubwa kwa maendeleo na maisha ya mtanzania anae jitahidi
kujikwamua na maisha magumu.
Usiangalie nyuma mwachie Mungu. Hii ni hulka ya wafanyakazi wengi serikalini.
 
Pole sanaaa. Hivi hawa maafisa usalama huwa wana nguvu kiasi hicho ?
Kama ni maafisa usalama ndo wako hivyo basi tujitathimin kama taifa wanaacha kudili na mambo makubwa ya muhumu katika taifa wanaingilia kufanya kazi zisizowahusu mbaya zaidi kwa maelezo ya mleta mada wanataka rushwa hata kwa wafanya biashara wadogo wamekosa weledi kabisa nimesikitika sana
 
Recruitment shida inaanziaga huko napongeza Bunge kuondoa kigezo cha JKT.

MAANA hakuna mtu anayejielewa akaenda JKT kupoteza muda huko, kama swala la TABIA, NIDHAM, UZALENDO ni jambo ambalo lipo tu halijengwi kwa kozi ya miez mi3 au mwaka.
 
Pole sana,hiyo taasisi imejaa watu wa ovyo sana
Ila usiwaache angalia namna ya kuwalipizia kisasi

Ova
 
Back
Top Bottom