Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
Serikali na chama tawala wamefafanua vizuri sana kuhusu mradi huu wa bandari ya Dar es Salaam aliopewa mwekezaji kutoka Falme ya Dubai anayeitwa DP World.
2. Waziri wa Mipango na uwekezaji, Prof Kitila na wenzake wameeleza vizuri kwamba huyu DP World ndiye aliyeshinda tenda kati ya waombaji saba kutoka nchi mbali mbali duniani. Kwamba tenda hii ilihusu kazi ya upakuaji na upakiaji wa makontena pale bandari ya DSM iliyokuwa inafanywa na kampuni ya TICTS kutoka China ambayo mkataba wake uliisha mwaka jana. Tofauti tu ni kwamba mwekezaji huyu mpya atatakiwa kutumia automated cranes za kufanya kazi hiyo na kuweka mfumo wa tehama wa uendeshaji wa shughuli za pale bandarini DSM.
3. Wamesema vizuri na wananchi wamewaelewa na kukubaliana nao kwamba mwekezaji huyu hatakuwa na hadhi tofauti na wale wa TICTS au wale tuliwapaga DAWASA enzi zile na walipozengua tuliwatimua. Au wale kutoka India tuliowapaga kuendesha shirika letu la reli (TRC) na walipotuzengua tuliwatimua. Au wale kutoka Afrika Kusini tuliowapaga shirika letu la ndege na walipotuzengua tuliwatimua.
4. Tatizo ni kuwa mkataba ulioandaliwa na timu yetu ya negotions iliyoongozwa na mwanasheria kutoka wizara ya uchukuzi, Bw. Hamza Johari (mwenye LLM in international law from Ukraine), hauendani kabisa na matarajio hayo yanayoelezwa na serikali. Halitakuwa jambo lepesi kumtimua akizengua kama hao wengine waliotajwa hapo juu. Mwekezaji huyu amepewa mamlaka makubwa sana ya kutoingiliwa na serikali katika maeneo yake. Halafu kapewa na bandari zote za nchi yetu na mambo mengine kadhaa.
4. Uwezekano ni mkubwa draft hiyo ya Hamza Johari haikupelekwa kupitiwa na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na ile kamati ya akina Kabudi na Osolo kabla ya kufika kwa rais kupata saini yake. Ndiyo maana AG na Kabudi wamejiweka mbali kuitetea. Huyu Hamza hataki kubadili hata nukta kwenye hayo maandiko yake. Watu kama Prof Shivji anawaita ni wazee ambao mambo ya IGA hawana ujuzi nayo kwani ni ya kisasa (new concept). Ni kama wale vijana wanavyowaita wazee ambao actually ndio waligundua computer kwamba ni BBC (Born Before Computer)!
Hamza hataki kubadili hata hiyo heading ya mkataba ili iendane na hayo matakwa ya serikali na wananchi. Kwamba "sea and lake ports in Tanzania" isomeke "port of Dar es Salaam". Hizo port zingine kazi ikipatikana si tenda itatangazwa na yeye si lazima ataipata. Haraka ya nini? Hamza alisema kitu kama bandari ya Bagamoyo karibu atapewa huyu jamaa wa DP World.
Kwamba kwenye Appendix 2 ya instrument of full powers, ..... maneno "and the Government of Dubai" yaondolewe kwani Prof Mbawala hawezi kusaini on behalf of the government of Dubai. Hata hili, Hamza ambaye LLB na LLM zake alizisoma kwa lugha ya kirusi nchini Ukraine (mwaka 1994 hadi 2000), hataki kabisa kukubali - yaani analiona ni sawa. Jamaa huyu anajua sana lugha ya kirusi kuliko ya kiingereza.
Article 20: Kwa nini Johannesburg? Kwa nini isiandikwe South Africa? Kwa nini isiwe Uganda au Kenya? Anasema Vienna convention wakati The Vienna Convention (of 1969) on the Law of Treaties is not yet in force because only 33 states have ratified the convention as per October 2022.
Sasa vitu obvious kama hivyo navyo vinakuwa tabu kukubaliana.
Sisi ni wanachama wa Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) na International Center for Settlement of Investment Disputes (ICSID), hatuhitaji bla bla zingine.
Hamza hataki kukubali kwamba Falme ya Dubai si nchi jirani na Tanzania na hivyo haina mamlaka ya kuingia mkataba huo na sisi. Mwenye mamlaka hiyo ni UAE. Yeye Hamza kang'ang'ania Dubai ni nchi jirani na Tanzania, upuuzi mtupu sawa na wa yule waziri aliyesema Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zambia.
5. Kwa nini serikali kupitia Mwanasheria Mkuu wa serikali wakakaa na wadau wengine wa sheria na uchumi, kuuweka vizuri mkataba huo wa Hamza kwa masilahi ya taifa. Kwa nini mvutano wote huu wakati jambo hili lilikuwa jepesi tu kuliweka sawa kwa majadiliano ya kitalaamu na kufikia maridhiano tukitumia zile R nne alizotuelekeza Mama.