Kwanini hakuna nchi Afrika imewahi kumiliki ndege Aina ya Airbus 220-300?

Kama ni ya kwanza kutengenezwa, basi ni ya kwanza duniani na sio Africa tu!!
kwa order kutoka Afrika ni ya kwanza kutengenezwa(kumbuka ndege zinatengenezwa kwa order sio kama magari)
Duniani zinatumiwa na swissair na makampuni mengine.
Kumbuka Egypt air wameorder ndege kumi za aina hii.
 
Kwa uelewa wangu hii ndege ni Bombardier kilichobadilika ni jina tu,Airbus a220-300 baada ya kuuzwa Airbus .Ila specs zote za ndege ni za bombardier iliyoagizwa!
 
Fanya kwanza your homework halafu ndio uje kuuliza.
Unashindwa hata ku google upate jibu..??
Kweli tuna safari.ndefu..elimu..elimu..elimu

safari ni ndefu sana mkuu,watu wamejitoa ufahamu na kuelekeza nguvu zote kwenye kukosoa tu.watu wamekuwa wataalam wa kila mada inayopita mbele ya macho yao.hakuna jema kwa mswahili
 
Unamaanisha mzigo tulioagiza na uliokuja ni miwili tofauti?
Ni hivi mkuu. Sisi tuliagiza Bombardier CS 300 kutoka kiwanda cha Bombardier kilichopo Canada. Hizi ndege Bombardier CS 300 zilikuwa designed na kutengezwa na hiyo Kampuni. Ndege zilipokuwa kwenye mchakato wa kutengenezwa, kiwanda chake kikachukuliwa na Airbus. Baada ya kuchukuliwa wakabadilisha jina la ndege kutoka Bombardier CS 300 na kuwa Airbus A 220-300. Kwa hiyo kwa ufupi ndege ni zile zile (hazikuwa designed upya bali zilibadishwa jina tu na kuongezewa vikombolwezo vinavyoendana na kampuni ya Airbus).
 
Wewe bado tu hujamjua Jiwe kuwa ni bingwa,wa kupiga fix??

Si ndiyo huyo huyo alitwambia watanzania kuwa alipoingia madarakani miaka 3 iliyopita, alikuta sukari shilingi 5,000 kwa kilo, wakati katika historia ya nchi hii, tokea awamu ya Mwalimu Nyerere hadi Jakaya, sukari haijawahi kufika bei hiyo

Kwa hiyo inabidi tumzoee tu, kwa kuwa tuna Presidaa, ambaye ni bingwa wa kupiga fix!

Na hiyo ndiyo sababu kuu ya kuzuia wapinzani wasifanye mikutano ya kisiasa, kwa kuwa anajua wataeleza ukweli, ambao utamwacha Jiwe "uchi" wa mnyama!
Hahaa ila nzee ana fix yule kupitia yeye nimegundua kuwa Mungu hayupo " maana huwa anatulisha matango pori halafu anasema mungu nisaidie na mungu hamuadhibu wala nini wakati anajua. Kuwa john analitumia jina lake vibaya kutulisha matango pori
 
Nilisikia kua hiyo kampuni ya bombadia imeuza hisa zake kwa boengi sasa hizo ndege baada ya kua chini ya boengi zikabadilishwa jina sababu bombadia is now part of boengi ila bombadia ndio wamezibuni
Actually it is Airbus not Boeing who bought Bombardier company.
 
Hebu tutulizeni akili kidogo. Huo ushamba na ubwege wa jamaa katika kuuliza swali sijauona. Ila nimeuona kwako katika kujibu swali
Acha ushamba na ubwege. Hili ni tolea jipya naTanzania imepokea ya kwanza kwa sababu ilikuwa ime-oda bombardier C series ambazo zilibadilishwa jina na kuitwa Airbus 220-300 baada ya kiwanda kuchukuliwa na Airbus.
 
Hebu tutulizeni akili kidogo. Huo ushamba na ubwege wa jamaa katika kuuliza swali sijauona. Ila nimeuona kwako katika kujibu swali
Ushamba na ubwege ni mtu anakuambia kitu cha ukweli halafu wewe unabisha na kusema ni mwongo wakati hujui ukweli wa jambo linalozungumzwa. Huu ulimbukeni Tanzania upo sana...mtu anabisha huku hana clue yoyote na kile anachobishia.
 
In kwasababu marais wao sio wazalendo kama kwetu, hawana hela pia hawapo kwenye rait track
 
Swali libaki kuwa, ni kwa nini unadhani ni ya kwanza Afrika?

Is it because may be Kenya Airways ama South African Airways ama Egypt ama Ethiopian Airlines hawakuwahi kuvumbua kiwanda cha kutengeneza ndege aina hiyo?

Is it because may be they are too expensive? Ama is it because of......?

Angalieni isije ikawa ni kama kashfa ya Rad

Na hivi jamaa anajipangia na kuamua kujinunulia kivyake akiwa amejifungia na mwanae Bashite chumbani Magogoni kwa fedha bila kupitia mifumo ya kibajeti kwa baraka za bunge......

Natari hiyo........ooh?
Hivi Kitaturu na ''ujembe'' wako wote hapa JF kitu kama hiki kinakutia shaka! Google utapata majibu yote.
 
Nilisikia kua hiyo kampuni ya bombadia imeuza hisa zake kwa boengi sasa hizo ndege baada ya kua chini ya boengi zikabadilishwa jina sababu bombadia is now part of boengi ila bombadia ndio wamezibuni
Hukusikia... Mm ndo nilikwambia kwenye story zetu za jioni pale kimboka inn buguruni
 
AIRBUS wenyewe kwenye twitter yao wameandika ni ya kwanza Afrika halafu wewe kijana kutoka nyanda za juu kusini unasema ni fix za Rais Magufuli.
Nyie wenzetu viroba mnavipata wapi?
Kama anatoka nyanda za juu kusini itakua anavipata [viroba] kutoka Malawi au Zambia.
 
Mhe. Rais ameeleza kuwa hakuna nchi barani Afrika imewahi kununua ndege Airbus 220-300, hii inatafsiri kwamba ndege hii ni ghali Sana? Je ni kwamba hazifai kwa mazingira ya Afrika?Siyo nzuri kibiashara? Ni nzuri Sana?

Maswali yangu yanalenga kufahamu kutoka kwa wataalamu wetu sababu za Tanzania kuwa wa kwanza kumiliki aina hii ya ndege wakati Afrika yapo mashirika mengi ya ndege yaliyoanza miaka mingi iliyopita na niwazoefu kwenye hii biashara.

Naamini kwamba TUNAJIFUNZA kutoka kwa waliotutangulia kwenye biashara zaidi ya kujifunza kutoka kwa makampuni yanayotengeneza ndege.
Sio kwa kuwa wengine hawawezi au wanashindwa kufanya basi na sisi tusifanye, tunaweza na tumeweza kununua ndege kubwa na tutafanya mengi sana tukiamua kuweka uzalendo na maslahi ya nchi, kutunza miundombinu yetu na rasilimali zetu zote kwa moyo mmoja, ila tukikaa kuwaza kufelifeli lazima tuanguke maana tutakuwa hatujiamini wala hatuna nia ya kujituma
 
Ni toleo jipya mkuu, Barani Afrika Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kuinunua
 
Back
Top Bottom