Kwanini DPW Wameamua Kuchua Bandari za Tanzania, Kenya na Msumbiji kwa Wakati moja. Hii ndiyo sababu.....!!

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,397
12,979
Kuna video nimeiona Wakenya wanalalamika kuwa serikali yao pia imesaini mkataba kisiri na DP World kucontrol bandari zote za Kenya. Kama hii ni kweli, hivi kweli kuna sababu yeyote ya kuendelea na hawa watu? Haiwezekani wachukue bandari zetu zote pamoja na za majirani zetu halafu tuwaamini kuwa ni wawekezaji wenye nia njema!

Kwa jinsi inavyoonekana UAE wanajua kuwa mafuta yao yatakwisha muda siyo mrefu. Hivyo sasa wameamua kuwekeza kwenye sector mbalimbali ikiwemo Usafiri wa anga (Etihad na Dubai Airline), kwenye bandari (DPW), Michezo (Machester City, New Yolk City, Melbourne City, Yokaham, Bumbai City nk), Utalii (dubai City), Crypto hub (Dubai) nk. Kwa jinsi inavyoonekana UAE wako desperate kuwekeza sasa, kwa ajili ya kizazi chao cha baadaye.

Kwa uwekezaji wanaoufanya kwa sasa hasa East Africa ambapo wanataka kuchukua bandari zote Kenya (Mombasa, Lamu nk), Tanzania na Mozambique hautakuwa uwekezaji wa faida kwa nchi husika, bali watakuwa wanajaribu kutake control ili huko mbeleni tusiwape shida kibiashara, yaani tusiwe washindani wao. Strategically, bandari yetu inaweza kuwa mshindani mkubwa sana wa DP World huko mbeleni. Sasa wao wameliona hilo leo wakati sisi hatuoni na wanajaribu kutuzuia kwa njia ya uwekezaji.

Kama kweli DP World ni wawekezaji wakubwa na wana nia njema, kwanini mpaka sasa hawajaweza kuziendeleza bandari za Beira (Mozambique), Durban and Angola kwa kiasi kikubwa au kwa technology kubwa kama ilivyo kwao Dubai? Hapo ndipo utaona kuwa strategy yao au malengo yao ni kucontrol zaidi ili kuhakikisha kuwa Dubai ports zinaendelea kuwa main ports na sisi tunakuwa tegemezi kwao.

Wanachokitaka Kenya na sisi tunakitaka. Wanachokitaka Mozambique na sisi tunakitaka. Wanachokitaka RSA na sisi tunakutaka pia na wenzetu wanakitaka. Sasa hapa unafikiri DP World watawezaje kuturidhisha wote kwa pamoja? Hii ni kama vile ndoa ya wake watatu.

 
Correction point;

Hiyo video ya Kenya ni ya zamani.

Na hilo "dili" halikuwezekana bandari zote.

Angalia vizuri. Huyo ni Musalia Mudavad, enzi za serikali ya Kenyatta Jr, saivi ni kiongozi kama PM, serikali ya Ruto.

Nipo tayari kusahihishwa.
 
Usifate ya Wakenya, kibiashara bado bandari ya Dar ni ndogo sana. Shindana nao kibiashara, wakikuwahi wao imekula kwako.
 
Usifate ya Wakenya, kibiashara bado bandari ya Dar ni ndogo sana. Shindana nao kibiashara, wakikuwahi wao imekula kwako.
Kwa nini Mozambique na Jibuti hawajafaidika kwa kiasi kile kile ambacho sisi tunategemea kufaidi?

Hawa watu wako hapa kwa ajili ya kudiversify their sources of income. Mafuta yanakauka. Huoni hata Qatar wametumia pesa kibao kwa ajili ya Kombe la Dunia. Saudi Arabia sasa wanalipa pesa ya kufa mtu kupeleka wachezaji Saudi Arabia ..... Qatar wanataka kuinunua Man United almost mara 2 ya ghrama halisi. Huo ndiyo uwekezaji unaoendelea huo upande. Theirs looking for different sources of income for their next generation. Period!!
 
Back
Top Bottom