Kwanini baadhi ya Watanzania hufurahia sana mabaya yanapotutokea kama Taifa?

Yangekuwa yanachanwa mabango yasiyo na heshima huu utetezi wako ungekuwa na nguvu, lakini mabango yanayochanwa ni yale yanasema ukweli mchungu. Hata mabango yanayokuwepo sasa, sio yale yenye ukweli mchungu, bali ni yale ambayo rais atayajibu ili kusaka kiki. Na yote hiyo ni Hadaa kuwa rais ni msikivu jambo ambalo sio kweli.
Hilo la kutaka kiki silifahamu. Tubaki kwenye hili la mabango.
 
Mkuu siji contradict, bali nasema ukweli. Acha nikupe mfano wa nchi zenye demokrasia duniani zinapopiga kura mfano mzuri ni wa nchi ya INDIA chama cha BJP hawakupata viti vingi WALISHINDWA jijini Delhi na chama AAP KUJITWALIA VITI 62 kati ya viti 70. kimewafanya BJP kushtuka.
Sasa unafikiri india pamoja na kuwa na demokrasia kubwa duniani.
Je Mbona basi wengine HAWAKUMTAKA MODI na chama chake?
Huwezikupendwa na kila mtu.
Na hilo lako la 99% silijui mkuu. Shukrani.

Nasema hivi ni bora ukae kimya, kama hujui hilo la ushindi wa 99% basi ww ni mgeni wa nchi hii ama hujui unaloongea. Niambie toka Magufuli ameingia madarakani ni uchaguzi gani mpinzani yoyote kashinda?
 
Yangekuwa yanachanwa mabango yasiyo na heshima huu utetezi wako ungekuwa na nguvu, lakini mabango yanayochanwa ni yale yanasema ukweli mchungu. Hata mabango yanayokuwepo sasa, sio yale yenye ukweli mchungu, bali ni yale ambayo rais atayajibu ili kusaka kiki. Na yote hiyo ni Hadaa kuwa rais ni msikivu jambo ambalo sio kweli.
Hata kama wewe ungekuwa ni rais leo hii, je ungefurahi kuona bango linalo dhalilisha utawala wako?
 
Narudia tena, Magufuli sio rais wa kwanza dunia hii, mabango yanayosema ukweli sio kwa ajili ya kumfurahisha rais, bali kusema ukweli ili upatiwe ufumbuzi. Labda kama amekuwa rais bila kujua nini maana ya urais. Ama kwake urais ni sehemu ya kutukuzwa mapenzi yake, na sio wajibu kwa kazi aliyoiomba.
 
Hayo nayosema ukweli hayachanwi mkuu, bali ni kama nilivyokueleza hapo nyuma.
 
Nasema hivi ni bora ukae kimya, kama hujui hilo la ushindi wa 99% basi ww ni mgeni wa nchi hii ama hujui unaloongea. Niambie toka Magufuli ameingia madarakani ni uchaguzi gani mpinzani yoyote kashinda?
Wali WABUNGE wa UPINZANI walioshinda uchaguzi na wako bungeni, je WALIUPATAJE ubunge kama si KUSHINDA kwao?
mbona unauliza swali lililo wazi?
 
Usidhani kuwa hatujui kuwa hao walio bungeni waliingia bungeni wakati wa Kikwete. Wakati huo demokrasia na tume ya uchaguzi walikuwa na aibu kwa mbali. Nitajie mpinzani aliyeshinda baada ya Magufuli kuingia madarakani, na yote hayo ni kutokana na matumiziya madaraka ya urais.
 
Ni swali linalonishinda kujijibu. Labda mnisaidie kuelewa. Ni kwa nini hasa baadhi ya Watanzania hufurahia sana wakati nchi inapitia changa moto mbalimbali hasa zinazohusu kusutwa ama kunyimwa misaada na wafadhili?

Ndege yetu ilipokamatwa SA, wengine walipiga vigelegele vya furaha, tunapotaka kuwekewa vikwazo vya misaada ya kiuchumi ambayo ingewasaidiaWatanzania wengi vijijini, baadhi wanafurahia sana na kusherehekea.

Si kila jambo ama maamuzi anayoyafanya Rais Magufuli ni aslimia 100 makamilifu.

Ana mapungufu mengi, Wakati mwingine ametoa maamuzi ambayo si kamilifu. Nina maana yeye si Malaika. Amejikwaa mara nyingi kwa misemo ama maamuzi.

Je, hili ndio yaweza kuwa sababu ya kumchukia kwa baadhi yetu na kumweka kwenye public lynching/ hadharani ili kuungana na maadui wa Taifa letu wanao tuonea wivu?

Kwa nini hasa baadhi wanafurahia sana tunapoingia matatizoni kama taifa?

Nini Tatizo la watu kama hawa?
Hawajui kwamba mabaya hayana macho? wote tutaumia. Wakinyima misaada ya elimu, watoto wetu wataumia na sisi wazazi tutaumia. Ndio maana tunahitaji sana kujua maana ya uzalendo.
 
Ndo hivo mkuu. Shukrani.
 
Usidhani kuwa hatujui kuwa hao walio bungeni waliingia bungeni wakati wa Kikwete. Wakati huo demokrasia na tume ya uchaguzi walikuwa na aibu kwa mbali. Nitajie mpinzani aliyeshinda baada ya Magufuli kuingia madarakani, na yote hayo ni kutokana na matumiziya madaraka ya urais.
Mkuu tusubiri uchaguzi ujao. Ikiwa CCM itapata wabunge WOTE 100% hapo utakuwa na HAKI ya KUULIZA swali lolote!!
Hata hivyo ni vizuri nikukumbushe kuwa vyama vya upinzani na upizani ni kikatiba. Usiwe na wasiwasi.
 
Husikii wakihubiri 99%? Au unadhani wanahubiri kwa bahati mbaya? Hizo ndio aina ya siasa za Magufuli linapokuja kwenye suala la ushindani. Wala usiongee lolote kwenye uchaguzi chini ya amri ya Magufuli.
 
Ni swali linalonishinda kujijibu. Labda mnisaidie kuelewa. Ni kwa nini hasa baadhi ya Watanzania hufurahia sana wakati nchi inapitia changa moto mbalimbali hasa zinazohusu kusutwa ama kunyimwa misaada na wafadhili?

Ndege yetu ilipokamatwa SA, wengine walipiga vigelegele vya furaha, tunapotaka kuwekewa vikwazo vya misaada ya kiuchumi ambayo ingewasaidiaWatanzania wengi vijijini, baadhi wanafurahia sana na kusherehekea.

Si kila jambo ama maamuzi anayoyafanya Rais Magufuli ni aslimia 100 makamilifu.

Ana mapungufu mengi, Wakati mwingine ametoa maamuzi ambayo si kamilifu. Nina maana yeye si Malaika. Amejikwaa mara nyingi kwa misemo ama maamuzi.

Je, hili ndio yaweza kuwa sababu ya kumchukia kwa baadhi yetu na kumweka kwenye public lynching/ hadharani ili kuungana na maadui wa Taifa letu wanao tuonea wivu?

Kwa nini hasa baadhi wanafurahia sana tunapoingia matatizoni kama taifa?

Nini Tatizo la watu kama hawa?
Kwamba tambua kwamba hakuna mtu anaewaonea wivu, hii nchi ni nchi maskini sana na fukara, anawezaje mtu kuonea wivu fukara ?, sijui kama umetumwa kuja kuuliza au unajitolea tu !!, kama umetumwa basi waambie hao mabosi wako, huku chini raia wa kawaida maskini hawana furaha na namna wanavyoendesha hii nchi, kumbuka hii nchi ya kwetu sote, kila raia wa nchi hii anayo haki kisheria kufanya shughuli zake halali mahala popote hapa nchini, haiwezekani Juma anatuhumiwa kutenda kosa Fulani anakamatwa anawekwa rumande na ananyimwa dhamana halafu John anatenda kosa yeye anaachwa huru huku vyombo vya ulinzi na usalama vikidai vinafanya kwanza upelelezi ili kuona kama kuna jianai inataka John ashitakiwe,
Unabambika watu na kesi za kupika ili kuridhishwa matakwa yako, Unaingilia mahakama ili ifanye kazi zake kwa mapenzi yako, Unatumia fedha zetu za kodi kuhujumu wale wenye mawazo tofauti na ya kwako wakati mahospitalini hakuna dawa na mahitaji muhimu !!, tunatamani yatokee zaidi ya haya machache yanayowasibu
 
Umeongea mengi sana. acha nichukue moja ama mawilihivi na unisaidie kuelewa.
1.Huu USHAMBA/PRIMITIVITY wake unakujaje? Na unaweza kuufafafanua ili KAMA upo basi AJIREKEBISHE?

2.Huu UKABILA unakuja kujaje hapa?.
Je Unaweza kutusaidia wengine wetu. Pengine HATUUONI ili tufunguke macho?
Kumbe wewe hauhitaji kushauliwa kwa sababu majibu unayo, kaa hivyohivyo...
 
Back
Top Bottom