Kwamtoro nina jambo zuri sana la kuwaambia Dada zangu mlio na umri wa 30+ pamoja wana MMU wote

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,922
3,234
Nimesikia sana maneno maneno ya kuwadharau na kuwaponda wasichana wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea.

Nilimsikia kijana moja akisema, msichana mwenye miaka zaidi ya 30 anaolewa na mwanaume ambaye tayari anamtoto au ambaye amemuacha mke wake.

Kijana mwingine tena nikamsikia, Wasichana wenye umri mkubwa wanapata tabu sana kuolewa, amna anayependa kuoa msichana mwenye umri mkubwa, nini alikuwa anafanya siku zote, ni kama ilivyo ngumu kwa mtu kupata kazi akiwa na miaka 30 huku akiwa hana ujuzi. Wasio na ajira wanayo sehemu yao ya kucheza lakini vijana wengi wafanyakazi wanapenda kuoa msichana mwenye umri wa miaka 20-26. Wamama walio kwenye ndoa ndio usiseme kwa jinsi wanavyo wasema maneno mabaya wenzao.

@kwamtoro nawaambia habari njema dada zangu wazuri wa JF na wanachama kindakindaki wa jukwaa pedwa la MMU. Hasa nyinyi mlio na zaidi ya umri wa miaka 30 kwenda juu ambao hamja olewa. Kwanza nyinyi ni wazuri, mnajielewa na mnajitambua. Acha neni na maneno yenye mifano hapo juu kutoka kwa vijana na wanawake wenzenu. Maneno yao yasiwafanye mfikie hatua ya kuolewa na mtu ambaye umpendi. Kuolewa siyo ndio kupata mafanikio. Kumbuka ni maisha yako, yakienda mrama hamna mtu yoyote atakusaidia.

Wengine wanasema awawezi kuoa mwanamke mwenye miaka 30+. Waache walivyo,siku moja watatembea nyuma ya mwanamke mwenye miaka 30+, ambaye anajielewa katika wakati muhimu na sehemu sahihi. Anashika visivyo shikika, anazungusha visivyo zungushika, watabadilisha akili zao kwa force. Ha ha ha ha!!!

Si utani. Kama unataka kuolewa , tafadhali yazungushe macho yako vizuri na yaangushe kwa kijana ambaye unapenda aina ya maisha yake aishiyo, tabia zake na si kwa kijana unaye mpenda. Kwa sababu kuna mstari mdogo sana unao tenganisha love na hate, kama hubby wako akikupiga vibao mara mbili, upendo wote unapaa kupitia madirishani.

USIJITOE KAFARA YA FURAHA YAKO KWA AJILI YA MANENO YA JAMII ILIYO KUZUNGUKA. Kuna maisha mazuri sana zaidi ya kuolewa. Ndoa ni nzuri, lakini haiweki shape ya masha yako, badala yake wewe ndio utaya shape. Mwanaume anaiaribu ndoa kwa kujifikiria yeye zaidi, kuitawala, badala ya kuweka upendo kama agizo la Mungu. Na kwa makusudi anaamua kuishi maisha ya usingle huku akifahamu amekwisha oa. Sisemi wanaume wote wapo hivyo ila wengi wapo hivyo. Na sisemi kama hamna wanawake wabaya, wapo pia. Lakini wapo wachache ukitofautisha na wanaume wasiojibidisha, wasumbufu, wajinga, wavivu, wabinafsi, wababe na wabahili.

MIMI NI MWANAUME NAJUA VIZURI NINI NINACHO MAANISHA. Mdada hamna kitu kibaya sana kama kuungana na mwanaume mvivu, muongeaji kama chiriku, mpumbafu, dhaifu, mbinafsi na mbabe wa kijinga.

INAANZA NA SISI WANAUME. MWANAMKE MWENYE FURAHA ANAIFANYA NDOA IWE NA FURAHA. Mwanaume anatakiwa afanye nini, kila siku anapaswa ampende mke wake kama maagizo ya Mungu yasemavyo, na kumfanya awe na furaha. Badala ya kupenda kumcommand mke wake kama zombie. Mwanaume anaye oa anatakiwa awe tayari kubeba jukumu lake jipya na kila kinacho husu ndoa, kufanya kila juhudi kuhakikisha ndoa inafanikiwa.

Wanaume kiukweli kabisa wanafanya ndoa zisiwe na mvuto siku hizi kwa wasichana seriously. Wanaume wengi wanawaita wake zao majina ya ajabu sana. Ila wakienda nnje wanawaita majina wanawake wengine BABY! Yamkini wanawake wengine utawakuta ni wakubwa kwao kiumri na wabayaaa!!!

Aibu sana! Embu fikiria mwanaume anampiga mke wake mateke huku mke wake akiwa na mimba ya miezi 8 katika sehemu za mfuko wa mimba. Wanaume wengi ngumu ku smile majumbani kwao wakiwa na wake zao pamoja na watoto

Wanaume wengi wanapenda kufanyiwa vitu vingi sana na wake zao lakini wao hawawezi kuwafanyia wake zao hivyo. Wanaume wanapenda wafuliwe dirty boxers lakini ni wangapi kati yao wanafua chupi za wake zao? Wanaume wangapi unawaona mtaani wanawashika wake zao mikono wakiwa wanatembea? Na pengine utawasikiwa wanaume wakiwagombeza wake zao na kuwaita wavivu na pindi mke akiitaji mashine ya kufulia ambayo labda ni ya mtumba tu, inauzwa laki nne anambiwa sina pesa. Ila yeye kwa siku anatumia elfu kumi na tano kila jioni kwa kununua bia na nyama choma ambayo kwa mwezi ni shilingi laki nne na nusu.

Mwanaume kweli amepoteza upendo, furaha, shukrani kwa mwenza wake. Na sasa wanawatafuta wengine zaidi kuwatesa.

NDUGU ZANGU WANAUME; JIFUNZE JINSI YA KUPENDA, KUJALI, KUMKUBALI MWANAMKE. NA KWA WALE AMBAO TAYARI WAMEKWISHA OA SIYO VYEMA KULALAMIKA HILI NA LILE. NA WALE AMBAO WAPO TAYARI KUOA, CHAGUENI THE BEST AS MUCH AS POSSIBLE. SABABU AIJILISHI NI JINSI GANI UONAVYO, INAANZA NA SISI.


MIMI NI KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 33, NIPO SINGLE NA NAJIKUBALI. JAPO MIEZI MICHACHE SANA NITAFUNGA NDOA. NITAMUOA MSICHANA AMBAYE NIMEPENDEZWA NA MAISHA YAKE JINSI AISHIVYO, IMANI YAKE NA TABIA YAKE, SIJALI UZURI WAKE.

Nawaheshimu sana wanawake wote, wanajiunga na familia nyingine ambazo hazijui hata kusema neno karibu huku wakiwa na tabasamu, maisha yao kama wanyama wa mwituni. Wanabeba ujauzito kwa muda wa miezi tisa ambazo kimsingi baadae akijifungua kwa kiasi Fulani hupunguza urembo wake

ASANTE!!!!
 
Uwa sielewi wanaume wanaowaita wake zao magoli kipa..hvi mwanamke anaekufanyia majukum yte hayo si madogo..anakuaje goli kipa?sikatai kusaidiana but isiwe lazma at any risky situations .cz ana majukum mwngne makubwa yanamtazama kama kulea..skuhiz imekuwa kawaida mwanamke ajifungue ..afta miez mitatu anakiacha kichanga na maid anaenda job..kurud usku wte na mume anafurahia jaman wanawake inapobidi tujitambue.tusikubari kuwa pressurised na wanaume selfish..30 or 40 bdo una thaman tusikubali maneno ya mtu mwngne yakuendeshe.mimi nimeolewa ata my early 20s..but kwwli Nina rafki na ndugu zangu wanao approach 30s bla kuolewa nawaona wanavyohangaika uwa naumia sana.
 
smonetimes, wanawake huwa tunakukimbilia kuolewa kisa tunaogopa kufika 30 huku tukiwa single. kwangu mimi hakuna tatizo kuolewa ukiwa kwenye 30s. kwanza unakuwa more matured, ni rahisi kutulia na kuheshimu ndoa, na unakuwa umejijenga vizuri kiuchumi

Well said, ifikie mahala wadada watulie. Wasiweke akili yao kwa kuogopa mashinikizo.
 
smonetimes, wanawake huwa tunakukimbilia kuolewa kisa tunaogopa kufika 30 huku tukiwa single. kwangu mimi hakuna tatizo kuolewa ukiwa kwenye 30s. kwanza unakuwa more matured, ni rahisi kutulia na kuheshimu ndoa, na unakuwa umejijenga vizuri kiuchumi

Thumb up ila angalia usije olewa na mjane!!!!!
 
Mmmmmmmh! Umekuja msikini KWAMTORO kuswali au wafuja tu jina letu? Mashekh na Shekhat wakikubamba utashaaa.
 
Sometimes mtu ukiwaza msichana wa miaka 30+ na yule wa miaka 21+ hamna tofauti ingawa si wote.

Watu wamekuwa wakitegemea wasichana wa kuanzia miaka 30+ na kuendelea wametulia na wamejipanga kimaisha na kwa future.
Ila utakuta huyo wa miaka 30+ naye hana tofauti na yule wa miaka 20+ na sana sana anajifanya anajua,ukiona msichana kafikisha 30 na kuendelea halafu anapenda starehe,club humkosi,stori za soloon kila siku,hela zake anatumia kutengeneza kucha na fashion mpya basi ujue hata akiolewa kumhandle ni kazi sana.
Mfano kama mwanaume umri wangu ni 30+ halafu nikawa na msichana wa kuanzia miaka 20 halafu anajielewa na isitoshe unaweza kukuta anakusikiliza unamcontrol na yupo radhi,yanini kutoana jasho na hawa wa 30+ yrs?
Na pia mpaka msichana afike 30+ ajiangalie wengi wao si wife material
 
Hao wanaobwabwaja wehu tu. Mdomo jumba la maneno wacha wabwabwaje. Ndoa yenyewe mchezo wa pata potea. Unaweza pata mume kitombelo mpaka baaasi. Hao hao ndo wanamchuna kwa chati. Au mume jina, senti tano yake huioni. Au mume zigo la miba, kajibweteka tu.

Sazingine Mungu anakunyima mume kukuepusha na vimbwanga tu. Maisha ni zaidi ya ndoa. Kuishi na mtu nyumba moja how can that make you achieve your dreams, fulfill your ambitions???? Tatizo watu wengi ni DREAM LESS NA AMBITION LESS, WAKO WAKO TU, NDO MAANA NDOA NI KILA KITU KWAO.
 
Sometimes mtu ukiwaza msichana wa miaka 30+ na yule wa miaka 21+ hamna tofauti ingawa si wote.

Watu wamekuwa wakitegemea wasichana wa kuanzia miaka 30+ na kuendelea wametulia na wamejipanga kimaisha na kwa future.
Ila utakuta huyo wa miaka 30+ naye hana tofauti na yule wa miaka 20+ na sana sana anajifanya anajua,ukiona msichana kafikisha 30 na kuendelea halafu anapenda starehe,club humkosi,stori za soloon kila siku,hela zake anatumia kutengeneza kucha na fashion mpya basi ujue hata akiolewa kumhandle ni kazi sana.
Mfano kama mwanaume umri wangu ni 30+ halafu nikawa na msichana wa kuanzia miaka 20 halafu anajielewa na isitoshe unaweza kukuta anakusikiliza unamcontrol na yupo radhi,yanini kutoana jasho na hawa wa 30+ yrs?
Na pia mpaka msichana afike 30+ ajiangalie wengi wao si wife material
Wife material is HIGHLY CIRCUMSTANCIAL!
 
Ndoa za maana mjini humu brides wengi wanakuwa above 30. Richard Mzirai n Cythia, Haidary Plaza n Mercy Galabawa, Mange Kimambi n Lance, Shamimi 8020 na Abdul Zungu, Jackline Jikas na Mlatie Rosegarden bar, etc.

HARUSI TALK OF THE TOWN SIO UCHOCHORONI AKUJUE NANI? Alaaaaaaaa! Ujanja kupata sio kuwahi.
 
Mmmmmmmh! Umekuja msikini KWAMTORO kuswali au wafuja tu jina letu? Mashekh na Shekhat wakikubamba utashaaa.

KWAMTORO hii ni tarafa moja bomba sana ipo Kondoa. Ukifika huko utatamani ulowee kabisa.
 
Back
Top Bottom