Kwako Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete.

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,922
3,234
Nikiwa muajiriwa katika kampuni binafsi moja hapa nchini. Nimeamua kukuandikia hii barua kutoa dukuduku langu la moyoni juu ya hiyo sheria ya mafao uliyo isaini ya NSSF, PPF na kadhalika.

Wewe ndio utakuwa Rais wa kwanza
Tanzania kupandikiza sumu kwenye mioyo ya watanzania wengi na kuifanya nchi wakati wowote kuingia kwenye machafuko. Muheshimiwa Rais, Tanzania ni kama hamna ajira za kudumu kwa sisi wafanyakazi wa wa makampuni binafsi. Atupendi ajira za kuajiriwa, inatatulazimu kufanya kwa sababu vijana wengi atuna fursa mbalimbali za kupata mikopo (Dhamana). Atudumu katika ajira zaidi ya miaka 4 kutokana na kufukuzwa kazi, kuacha wenyewe kwa manyanaso mbali mbali.

Nilikuamini, tulikuamini pindi tulipo fahamu kauli yako mbiu ya maisha mazuri kwa kila mtanzania, sasa imekuwa maisha magumu na mabaya kwa kila mtanzania. Hari mpya nguvu mpya kweli inasonenesha.

Pesa zetu wafanyakazi zinatusaidia sana hasa kipindi kazi imekwisha labda kwa kufukuzwa na kadhalika. Zinatusaidia kulipa karo za watoto wetu, pango na hata kamsingi cha kufungua biashara. Kwa % kubwa ya mishahara yetu tupatayo, huwa aikutani, atuwezi kutunzia pesa ya mishara.

Kama
mashirika haya hayana pesa, sasa ni vyema kuongeza kodi katika makampuni ya migodi ili utajiri huu mkubwa utunufaishe na siyo kunufaisha mataifa mengine ili serikali yako isizitamani pesa yangu na za walala hoi wengi.

Pia bila kusahau matumizi makubwa katika serikali yako ambayo kimsingi ayana ulazima. Wafanya kazi tulitegemea PAYE kushuka kwa asilimia kubwa
sana ambayo kimsingi ni mzigo mkubwa kwetu.
Na kwa taharifa yako tu, kwa hili ndiyo umekiua chama cha mapinduzi moja kwa moja. Wanachi awatapenda kiona CCM inatawala 2015, na ikitawala International criminal court the hague uhaholanzi itaihusu Tanzania. Jali Taznania jali maslai ya Chama chako ili usiwaachie wenzako matatizo pindi ukingatuka. Kanga, Fulana, kofia atuziitaji tena, sisi siyo wajinga na mkizileta!!

Kama utakuwa ujapitia hapa JF na ukaisoma hii barua naomba wasaidizi wako wakufikishie mapema na utengue sheria uliyoisaini ya kigaidi na unyanyasaji na kinyume na haki za kibinadamu, aitufai la sivyo
Tanzania aita kuwa kisiwa cha amani kwa sababu umetushika pabaya sana. Kuna vitu vya kuvumilia lakini hili alivumiliki, natokwa na machozi na ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo.
Asante

Mlalahoi
 
nafikiri anakuona baba rejao,ngoja atajibu tu ingawa kuchukua maamuzi ni mzito mno,cjui darasani alikuaje huyu jamaa
 
ni magwege kweli kama kuna jimbo limeweza kumchagua maji marefu kuwa mbunge unategemea nini
 
Hapa ni wafanya kazi wote kugoma kwenda kazini wikimoja.
Binafsi na serikalini.
Wala sio kwenda barabrani
 
Dah... pole ndugu !!!! kwa kweli ni udhalimu mkubwa kupitisha sheria kama hii bila hata kumshirikisha mhusika mkuu ambaye ni mfanyakazi mwenyewe!!!!!!!!!!!!!! Kwa sasa imeshapitishwa na inaoperate SASA TUJE NA MIKAKATI NINI CHA KUFANYA ILI IFUTILIWE MBALI!!!
 
Poleni watanganyika wenzangu kikwete rais wangu mbona unajiandaa kuwa mwenyekiti wa chama cha upinzani?kwanini unakata mti huku umeukalia? je wasaidizi wako hawajakwambia kuwa usitupe mawe huku ikiwa kwenye nyumba ya vioo?
 
Back
Top Bottom