Norshad
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,128
- 12,216
Salaam,
Natumai wote mmeamka salama.
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika je unasumbuliwa na Pumu? Basi inawezekana leo upo mahali sahihi pa kupata tiba ambayo inaweza ondoa kabisa hilo tatizo lako na ni tiba isiyohusisha madawa ya hospitalini, bali chakula tu.
Chukua kweme, kwa wenyeji wa kaskazini mnazifahamu hizi.
(kokwa za kweme zapatikana sokoni ama kwenye maduka ya Tiba asili, pamoja na kipande cha Papa - SAMAKI (vipande) inategemea mwenyewe unatakaje kulingana na usugu wa tatizo lako
Saga kweme zako mfano wa karanga za kusaga kisha chemshia na hicho kipande ama vipande vya papa, kisha kunywa ile Supu yake, unaweza rudia kutumia hii kitu sababu pia ni kama Supu tu, lakini wewe mwenye tatizo hilo kwako itakuwa ni Supu Tiba.
Inaweza kukusaidia sana ama ukapona kabisa kulingana na usugu wa hilo tatizo, na hii unaweza tumia hata mwenye Pumu ya kurithi.
Kwa wale ambao watatumia tiba hii msisite kuleta mrejesho kwenye uzi huu ili na wengine wafaidike na Tiba hii mujarabu kabisa.
Nimeona kuna umuhimu wa kuweka hapa ili kusaidia na wengine wenye shida hiyo, binafsi nimewasaidia watu kadhaa kwa kuwapa tu maelekezo haya haya na nashukuru wengi wao kwa sasa wapo vizuri na wengine wanasema tatizo hilo limeisha kabisa.
Kila la kheri..
NB: Mimi si mtaalamu wa Tiba Asili bali tiba hii nimefundishwa na Bibi mmoja shamba huko na mimi nimeileta hapa kwenu. Kwa upande wangu nina watu 10nambao wametumia na kati ya hao wapo waliopona kwa maelezo yao na wapo ambao wanasikilizia mpaka sasa kama itarudi tena ama vipi.
Hivyo basi kama tujuavyo inaweza mfaa huyu na mwinyine isimfae lakini unaweza kujarib7 sababu ni kama mboga tu, kweme unaweza tumia kuungia mboga mfano wa nazi na Papa nadhani wote tunamfahamu. (Papa samaki sio Papa wa Gigy Money.
Shukran