kwa waoaji...

jdkisiwa

Member
Dec 19, 2012
14
6
Ikifika mwaka 2017 na bado hujaoa
basi ujue Possibility ya wewe kuoa ni
ndogo sana.Sio kwa sababu wanawake
watakuwa wameisha,LA hasha!Ila
hutaweza ku-afford kuoa labda
umtoroshee msichana wa watu Gheto
kwako uishi nae kinyumba ,ila kuoa
jasho la meno litakutoka.
Ukipeleka Ombi la kuoa ujiandae kwa
gharama zifuatazo kutoka Familia ya
Bibi Harusi Mtarajiwa:
1.Blanketi la Bibi kutoka Home
Shopping centre vipisi viwili,rangi ya
Purple
2.Blackberry Q10 ya Mshenga
3.iPhone7 Water Proof(itakuwa
imetoka) ya Baba Mkwe
4.3-Piece-Suit ya NGOWI. kwa ajili ya
Mjomba wa Bibi harusi aliyemsomesha
Bi harusi sekondari huko mwanalugali
5.Samsung Galaxy 9 Bold-Wipe Screen
ya Mama wa Ubatizo wa bibi harusi
6.iPad ya Kungwi wa bi harusi
7.Koti la Single button Leather by
Martin Survivor Kadinda kwa babu wa
bi harusi kutoka Ileje
8.Mahari itajumuisha Less-Wig
Brazillian Hair kwa mama mzaa
chema,na Table sets za mninga kutoka
Orcadeco..Hapo bado hujanunua Suti
yako,Shela ya Bi Harusi ambaye
atang'ang'ania litoke Uturuki,na hapo
ana kijacho chako cha miezi 4
kishaanza kutuna kama kitenesi,bado
hujalipia Ukumbi Mwika Social
Hall,hujammalizia MC Luvanda milioni
4 ya kuwa MC wa harusi
yako...THUBUTUU YAKO!
Ukipewa Bili TOTAL utakuwa
umehamishia mawazo kumalizia ujenzi
wako wa nyumba iliyoko Site kule
Goba,utaona kuoa ni upotevu wa hela
na muda.
Ndugu yangu heri uoe sasa,usiwaone
watu wamechangamka kuoa hii miaka
2 ukajua ni bahati mbaya,WAMEONA
MBALI..Ikifika 2017 utaomba Poo,sasa
hivi we jishaue kuchagua-chagua tu
Mke wa kuoa kama uko mitumbani
Karume,Heri uoe huyohuyo hata kama
miguu yake imepinda kama Upinde wa
Mvua itanyooka mkiwa Honeymoon
 
Back
Top Bottom