Kwa wanaosafiri sijui huu ni ushamba?

Utasikia mtu tangu anaanza safari asubuhi mpaka anafika safari yake jioni anapiga simu kila baada ya dakika kumi kutambulisha alipofika, utadhani kabeba pembe za ndovu..!!
Na wale wa kwenye facebook wanaoandika on my way to Mwanza sala zendu please.
 
mimi nakereka sana na wale wanaokula chakula toka mwanzo wa safari mpaka anafika mara ndizi, mahindi mara karanga duuu
 
Mi napendaga yule kila kituo ananunua viroba vya z na kujivutia ka master sport gari likita kuondoka mdomo unatema miksa, alafu anafunga mdomo wake na kaugorooooo hana habari na mtu
 
Tz kubwa sana usifikiri kila mtu ana smartphone wee ndo mshamba wa mwisho unae dhani kila mtu anamiliki sim kama yako tembea uone.
 
Magari hayaaminiki pia madereva wengi wao siyo makini.ajari nyingi husababishwa na uzembe,kwa hiyo simu Ni muhimu Sana,lakini isiwe kila baada ya muda mfupi..
 
Magari hayaaminiki pia madereva wengi wao siyo makini.ajari nyingi husababishwa na uzembe,kwa hiyo simu Ni muhimu Sana,lakini isiwe kila baada ya muda mfupi..

Sababu nyingine ni kuzuia mitongozo kwenye bus....Yani ile ukitaka kunisemesha Niko busy na simu....dizaini "Niko mikese honey, nakupenda" halafu full chatting yani, nikipumzika nimesinziaa......Hapo kama abiria wa jirani alitaka kutupa ndoano anakuwa hana nguvu....!
 
aaaagh hiyo issue jana tu imenikumbusha dah mpaka kero kila kituo hata wakisimama kuchimba dawa unataarifiwa inakera sana ni ushamba kula bati ukifika uendako tuma ujumbe kuna watu wana viherehere na safari.
 
mimi nakereka sana na wale wanaokula chakula toka mwanzo wa safari mpaka anafika mara ndizi, mahindi mara karanga duuu

Hivi kama una kakitabu, kajarida au gazeti unajisomea ili kujiongezea ujuzi, maarifa au kupata taarifa mpya utakuwa kweli na muda wa kufuatilia jirani yako anakula mahindi, yai au nini sijui? Kama unasafiri mfano Dar to Mwanza hivi unateea kweli the whole trip uwe umekaa tu kuangalia abiria wenzako au kusinzia the whole trip?!
 
Utasikia mtu tangu anaanza safari asubuhi mpaka anafika safari yake jioni anapiga simu kila baada ya dakika kumi kutambulisha alipofika, utadhani kabeba pembe za ndovu..!!

Kila baada ya dk 10? Unamuhesabia toka asubuhi hadi jioni?Mzee huo muda wa kumfuatilia mtu usiemjua toka asubuhi hadi jioni unautoa wapi?
 
Ilimradi hajavunja sheria poa tu.

Kama vipi tafuta headphones.

Unajuaje pengine ana wake 22 kama Chifu Burito?
 
kama ni kweli kila dk10 anapiga simu ni ujinga ila na ni ushamba, kama kila baada ya saa moja ni werevu na sio ushamba.
 
na wewe nae ni Great Thinker?

But mind you in the same coach we had some other nationalities, wajerumani wawili, wajapani wanne na mfaransa mmoja but I could not hear any of them shouting over their cellphones although they are richer than these poor swahilis.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom