Mama timmy
JF-Expert Member
- Jan 2, 2013
- 656
- 209
Naomba contact zenu
Yes huo utaalam ninao,nitakupm contacts zetu ili nikusaidie vizuri
Nina maswali kadhaa kuhusu utotoleshaji wa viifaranga wa kienyeji/CHOTARA
1. Kama una incubator yenye capacity ya mayai 1000 unahitaji kuku wangapi as parent stock ili kuendesha hiyo incubator bila shids?
2. Napataje parent stock.?
3. Kwa nini kuku chotara sometimes wanatoa vifaranga vidhaifu sana na wasiokua?
Natanguliza shukrani zangu
Vp kuhusu soko la sungura mkuu?
htuc,Kimsingi ukiwa na Incubator moja yenye uwezo wa kuchukua mayai 1000,huwezi kuweka mayai yote 1000 kwa wakati mmoja kwani ukifanya hivyo ina maana kuna mayai mengine utapoteza kwa kusubiri wiki tatu ili mayai uliyoweka yotorewe kwanza kisha uweke mengine.Incubator yenye uwezo wa kuchukua mayai 1000,utatakiwa ugawanye idadi hiyo ya mayai kwa tatu ili upate mayai utakayokuwa unayaweka kila wiki.Ukigawanya utapata mayai 333 ambayo kila wiki utapaswa kuyaingiza kwenye Incubator yako.Utaweka siku ya kwanza mayai 333,yatakopofika siku ya saba unayashusha chini,unaweka mengine yanakuwa na siku 1 na haya siku 1 yakifikia siku 7 na ya yale ya siku 7 yankuwa na siku 14.Siku ya 19 unayashusha kwenye kitotoreo(hatcher).
Hivyo ukiwa na machine ya kutotoa mayai 1000,utatakiwa uwe na parent stock 100,na kwa kuwa ni parest stock aina ya chotara utakagaji wake si mkubwa sana kama parent stock wa kuku pure wa mayai.Hao kuku 100 kila siku utaokota mayai 50 na mayai 50 ukizidisha kwa 7 utapata mayai 350,kati ya hayo, mayai 333 ndiyo utakayoingiza kwenye incubator.
Parent stock wa chotara wanatengenezwa kwa kuchukua kuku pure wa kienyeji(majike) ukipata kuchi wa Singida au Tabora ni wazuri zaidi then unacross na majogoo pure wa kisasa breed ya MAYAI mfano Rhode Ireland red(RID) au Barred polmouth rock.Ile cross ya kwanza ndio utakayoifanya parent wako na utawawekea tena majoo ya kisasa ili kuboresha kosaafu yao ili waweze kutaga zaidi.Kama utahitaji waliocrosiwa kabisa tuwasiliane.
Kupata vifaranga dhaifu kunasababishwa na mambo mengi sana.Mfano,mayai yakiwa madogo chini ya gram 45,kuweka mayai kwenye machine bila kuyatibu,joto kuwa dogo kwenye Incubator nk.
Ndugu yangu soko la Sungura hapa kwetu Tanzania bado ni dogo sana.Wengi wanafuga kama mapambo nyumbani.

Vp Kuhusu uwezo wa utagaji wa cross breed ukilinganisha na pure breed?
Mayai yanatibiwa vipi? na njia zipi hutumika kuyatibu kabla ya kuyaweka kwenye Mashine?
Kuna Soko la ku export nje ya nchi?
Kichwa mbovu naomba contact zako
Mkuu vipi kuhusu Dawa? Ni dawa zipi ni muhimu mtu kuwa nazo kama za huduma ya kwanza ukiachilia zile za Chanjo? Na vipi zile za Chanjo kuna mbadala wa zile za kuwekwa kwenye Fridge?
Na mwisho ukisoma machapisho Mbalimbali kuna kukinzana kuhusu njia za kutumia wakati wa kuchanja hao kuku, Mfano unaweza kuta Dawa ya Ugonjwa mmoja tu ina Maelezo tofauti tofauti ya Jinsi ya Kuwapa dawa, Wapo wana dai inatakiwa wawekewa Machoni, wengine kwenye Mabawa na wengine kwenye Maji hiyo ni chanjo ya Ugonjwa mmoja tu
Mheshimiwa Kichwa mbovu, nataka nijikite kwenye uzalishaji wa vifaranga wa kuku wa kienyeji! Ni wapi naweza pata mashine ya uhakika ya kutotolesha mayai yenye kutumia mafuta ya taa? Maana za umeme sizitaki umeme hauaminiki tena. Uwezo wa juu kwa mashine hizo zinazotumia mafuta ya taa zinazopatikana Tanzania ni mayai mangapi? Unaweza kunidokeza juu ya bei zake na ubora wake! Nikiipata nitanunua nitotoreshe vifaranga nawalisha kwa mwezi mmoja nawauza! Najua italipa tu. Natanguliza shukrani zangu.Ndugu wana jamii forum,ifike wakati tuache kulalamika, tujitume kwa bidii kufanya kazi kwani kazi ndio msingi wa maisha yetu.Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa,kuajilikiwa ni utumwa pia ni hasara kama utapiga vizuri hesabu zako.Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.
Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi .Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk ,kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini.Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.
Karibuni kwa mjadala.
Mheshimiwa Kichwa mbovu, nataka nijikite kwenye uzalishaji wa vifaranga wa kuku wa kienyeji! Ni wapi naweza pata mashine ya uhakika ya kutotolesha mayai yenye kutumia mafuta ya taa? Maana za umeme sizitaki umeme hauaminiki tena. Uwezo wa juu kwa mashine hizo zinazotumia mafuta ya taa zinazopatikana Tanzania ni mayai mangapi? Unaweza kunidokeza juu ya bei zake na ubora wake! Nikiipata nitanunua nitotoreshe vifaranga nawalisha kwa mwezi mmoja nawauza! Najua italipa tu. Natanguliza shukrani zangu.
Kuhusu kujadili hakuna la kujadili hapa mada yako iko bayana kabisa kwamba kujiajiri ndiyo jibu la kujiweka huru kifedha, huko kwenye kazi za mishahara ya kupimiwa acha wakae walioridhika, tutawaajiri ukifika wakati maana wao wanaogopa risk! Wewe tumwagie maarifa tu hapa sisi tuanze kidogo kidogo tutaendelea kupeana updates mbele kwa mbele!
Alichosema chasha ni sahihi kabisa,mashine zinazotengenezwa hapa nchini ni usanii tupu,watengenezaji hawako serious na kazi.Kuzinunua ni kutupa pesa tu pasi na sababu yoyote ya maana.Hata hizi zinazotumia umeme bado ufanisi wake ni mdogo sana kiasi kwamba haziwezi kukupa faida.Kama uko serious na kazi pata machine kutoka nje ya nchi,mfano China au Italy huko utapata za uhakika.Kisha nunua generator kwa ajili ya emergence hapo utatengeze pesa,haitakiwi kufanya biashara kwa kubahatisha.Mheshimiwa Kichwa mbovu, nataka nijikite kwenye uzalishaji wa vifaranga wa kuku wa kienyeji! Ni wapi naweza pata mashine ya uhakika ya kutotolesha mayai yenye kutumia mafuta ya taa? Maana za umeme sizitaki umeme hauaminiki tena. Uwezo wa juu kwa mashine hizo zinazotumia mafuta ya taa zinazopatikana Tanzania ni mayai mangapi? Unaweza kunidokeza juu ya bei zake na ubora wake! Nikiipata nitanunua nitotoreshe vifaranga nawalisha kwa mwezi mmoja nawauza! Najua italipa tu. Natanguliza shukrani zangu.