Kwa teuzi hizi, Chadema muungeni mkono Rais Samia

Philipo Mwakibinga

Senior Member
May 13, 2013
111
175
KWA UTEUZI HUU UNAOENDELEA KUFANYWA NA RAIS WA JMT MAMA SAMIA, TANZANIA ITAKAA SAWA.

Kwanza nimpongeze Mh Rais kwa uteuzi alioufanya ilikuendelea kusuka kikosi kazi chake chenye lengo la kuleta tijazaidi katika maendeleo yetu.

Niwapongeze wote walioteuliwa na wanaoendelea kuteuliwa kwasababu kuteuliwa na Mh Rais ni nafasi adim na adhimu yenye heshima kubwa sana.

Uteuzi huu umekua wakipekee sana na naweza kusema ni watofauti katika majira yote tuliyopitia. Mh Rais katimiza ahadi kwa Vijana wa Taifa hili kama alivyoitoa pale Mwanza. Rais amekata Kiu ya Vijana na Watanzania juu ya upatikanaji wa nafasi za uongozi pasipokubaguana kwa rangi, kanda ama kabila atokalo mtu. Mama ameteua katika sehemu zote na hili amefanikiwa sana.

Mh Rais ametoa nafasi kwa wenye uwezo kwenda kufanya kazi na kuyafanyia kazi yale wanayopenda kushauri mara kwa mara wapatapo nafasi. Hili limekua jambo jema na heshima kubwa kwa vijana hapa Tanzania.

Uteuzi usiyo na Chembe ya Shaka wala Malalamiko na manung'uniko. Mh Rais amefanya uteuzi ambao umeungwa mkono na kila mtu bila kuwa na masikitiko au hali ya kutoridhika kwa baadhi ya kundi au watu fulani. Hizi ni pointi 3 nyingine muuhimu kwa Mama yetu.

Uteuzi umeonesha kwa vitendo kuwa Tanzania ni yetu sote na sisi ni wamoja. Kwa uteuzi huu Mh Rais kaonesha na kuweka wazi kuwa Ujenzi wa Tanzania yetu unamuhitaji kila mmoja wetu na siyokundi moja tu, la Wanasiasa. Tanzania inahitaji Wakulima, Wanasiasa, Waandishi wa habari, Wanasheria, Wasanii na Wengine wote wenye uwezo wa kufanya kazi ya kulijenga taifa. Rais kaendelea kuwapa nafasi aliowakuta pasi na kinyongo chochote. Huyu ni Kiongozi na Mama wa Kweli katika Taifa letu.

Rai yangu kwa WanaCCM, Wapinzani na Watanzania wote wasio na vyama. Tuendelee kumuunga mkono kwa dhati Rais wetu kwa moyo thabiti na kumlinda kwa gharama yoyote huku tukimuombea Kheri kwa Mungu aweze kutimiza azma yake njema iliyoanza kuonekana kwa Taifa letu.
 
Naona wanaccm mkianzisha mada humu jukwaani ni lazima muitaje cdm ili uzi unoge. Huo ni udhibitisho kuwa cdm ni chama cha kizazi hiki, huku ccm chama cha kizazi kilichopita kikishurutisha kubaki madarakani.
 
Sasa CHADEMA wa nini kwenye heading yako?unatafuta umaarufu na kuteuliwa kupitia CHADEMA? Kafie mbali dogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom