Mizania
JF-Expert Member
- May 17, 2023
- 1,842
- 1,699
Mkuu kwanza tukubaliane kuwa Rais Samia ametunukiwa PhD ya udaktari wa heshima sio wa kusomea...mtoa mada anadai aliyepewa ndio feki, hana uwezo wa kupata PhD kwa kuisomea.
..je, wewe unaamini Maza ana uwezo wa kielimu na kitaalum kupata PhD?
..Maza amewahi kuandika makala yoyote ktk maarifa ya kitaalam?
..Maza amewahi kuandika kitabu chochote kudhihirisha usomi wake?
..Maza amewahi kualikwa popote na wasomi kutoa mhadhara na kuulizwa maswali kutokana na mada aliyowasilisha?
Walio mtunuku waliamua wenyewe, kwa hiyari yao na kwa vigezo vyao kumpa kwa sababu ya heshima yao kwake, sio kwa sababu ya uwezo wake wa kusoma, hapana.
Pili, nilitaka kuweka kumbukumbu sawa kwa sababu ndugu Goodluck5 alipotosha kuwa ile PhD aliyopewa Rais Samia ni feki/mchongo.
Tatu, Rais Samia ametunukiwa heshima hiyo na watalaamu wa nchi ya nje bila Rais Samia kuwalazimisha.
Ninaami wao kwa utalaamu wao wameona jambo adhimu kwa Rais Samia kiasi cha kustahili hiyo heshima!
Kama mashaka ni uwezo basi wakutiliwa mashaka kuhusu uwezo ni hao maprofesa kwa kumpa heshima ambayo wengi wetu tu naona hakustahili.
Kimsingi kama tunafikira hasi namna hii juu uwezo Rais na kiongozi wetu, basi tujue yeye ni true reflection ya jinsi tulivyo! Maana hajashuka kutoka mbinguni!
Nne, kuhusu kuandika Makala au kitabu, ni mapema mno kusema hata weza kuandika. Kwa maoni yangu, jinsi ambavyo ameweza kuongoza nchi kwa utulivu akiwa mwanamke amedhihirisha uwezo wake kiasi cha a
Kustahili heshima hiyo!
Ukweli usio na shaka ni kuwa ameingia madarakani katika mazingira magumu, hatari na ya pekee. Kaingia baada ya Rais kufa akiwa madarakani, umbi la uchaguzi mkuu halijatulia na bado korona ikiwepo.
Pamoja na hayo amepambana mno hadi nchi sasa ni tulivu, uchumi unatengamaa na kuinukia vizuri, uhuru na demokrasia ya wananchi imetamalaki ilihali uwekezaji umeongezeka miongoni mwa machache
Mkuu waswahili husema, mnyonge, mnyonge ila haki yake mpenzi.