Kwa nionavyo, Wakili huyu hatakuwa na mwisho mwema kiroho

1. Mara ya kwanza Kesi iliyosumbua sana, ya yule mmiliki wa mabasi maarufu ya J Four(J4) ya kuwaua wadeni wake kwa kuwapiga risasi, mpaka kuhukumiwa kufungwa maisha(kama sijasahau ilikuwa kunyongwa hadi kufa) ambayo kiuhalisia ni kweli jamaa aliwaua watu wale(alikiri kuhusika), Wakili huyu kwa kuwa anafahamu namna alivyo na mtandao mkubwa wa mahakimu akaingilia kesi ile na kesi kuanza upya, na kwa dalili zilizokuwepo ni kwamba yule jamaa(J4) alikuwa anaelekea kushinda kesi(sijui kama hukumu ilishatoka maana niliondoka Tz, nikaacha kufuatilia) hivyo roho za wale waliouawa zikawa zimedhulumiwa kwa kujuana na nguvu ya pesa.

2. Kesi ya mke wa marehemu Bilionea Msuya,
Baada ya mauaji ya dada wa marehemu bilionea Msuya, mama wa mtoto mmoja na aliyekuwa akifanya kazi Wizara ya Fedha, kuuawa kwa kuchinjwa kama kuku, Mke wa marehemu bilionea Msuya alikiri kuhusika na mauaji yale kwa kigezo kuwa marehemu(dada wa bilionea Msuya) alikuwa akimsumbua sana kwenye mirathi, hivyo akahukumiwa kifungo cha maisha kama sijasahau

Ni yule yule wakili kuingilia kesi hiyo ambayo awali mtuhumiwa alikiri kuhusika na mauaji hayo, baada ya muda na wakili huyo kuchezesha kama kawaida yake, February mwaka huu muuaji kaachiwa huru bila shaka yoyote kua hakuhusika

Ni kesi hii ndiyo inayoibua maswali na kejeli nyingi kwa mahakama zetu na vyombo vya ulinzi na usalama hasa jeshi la polisi upande wa upelelezi, na wengi kuona kua kesi ile haikumtendea haki marehemu dada wa bilionea Msuya ambayo kimsingi ni kweli

Sasa mimi nimekaa na kutafakari sana, kimwili na hasa kiroho, nikajiuliza huyu wakili mwenye koneksheni na majaji mbona ameifanya pesa, koneksheni na elimu yake kama fimbo ya kuwachapia wale wasiofika bei,
Roho za marehemu hao zinalia, familia za marehemu hao zinataabika, watoto wa marehemu hao wanateseka sababu ya kuuawa kwa wapendwa wao, ni nani atazifuta machozi familia hizi, Ee Mwenyezi Mungu ni nani atawafuta machozi watoto wa marehemu hao ambao wengine walikua wakisoma shule nzuri leo hii wanaenda kidumu na mfagio sababu ya kuuawa kwa wapendwa wao na mbaya zaidi ukweli kupindishwa na mhusika wa kupindisha ukweli ni huyu wakili, ninajua nayeye ana watoto ana ndugu na ipo siku hao waovu anaowatetea, roho za marehemu zitamrudia yeye na kizazi chake kwa kua anafanya hivyo si kwa sababu watu hao walionewa bali watu hao wamemlipa pesa ya kutosha ambayo anaweza kugawana na wenzake na kesi ikapindishwa , na kuwashuhudia uongo marehemu hao

Ukweli utabaki pale pale, dunia tunapita, vile unavyowatendea wenzako nawe siku moja utatendewa vivyo hivyo kama si wewe basi kizazi chako. Pesa haijawahi kutosha na haitotosha kamwe, unashuhudia vipi uongo ambao unajua kweli yake, kweli pesa mwanaharamu, Ee Mwenyezi Mungu nijaalie nipunguze tamaa hasa dhidi ya pesa, sijui huyo mtoto wa dada wa Bilionea Msuya atakua na umri gani lakini katika kufikiria kwangu hata akiwa mkubwa ataoneshwa watu wawili waliohusika na kifo cha mama yake, Muuaji(ambaye awali alikiri) na wakili aliyemsimamia na kumtetea kua hakuhusika ilihali anajua kuwa alihusika.

Najua hata watu hao wangefungwa isingewaongezea kitu familia zao lakini kitendo cha wao kufungwa kingeleta ahueni kwa wapendwa wao.

Sijui kwanini kesi ya huyu dada wa bilionea Msuya imeniumiza sana, nimeumia sana, japo nikiri kuwa mimi sikuwahi kuwafahamu watu hao ila nilikuwa interested tu kuona haki ikitendeka kwa kua wauaji walikiri,

Ndugu na rafiki yangu wakili najua unazipenda kesi hizi kwakua zinakupa pesa ndefu kwa wakati mmoja lakini kweli ya mauaji ya watu hao unazijua, ni kesi zenye nguvu za kiroho, naomba nikukumbushe "Karma is a bitch" kama si kwako hata kwa vizazi vyako.

Mungu azitie nguvu familia za marehemu. "Sisi ni wake na kwake tutarejea"
Amina
Mm huwa nawashangaa has wanaojiita mawakili. Mteja wake anekiri mbele yake juwa ametenda kosa mfano ameua, ameiba nk. Jambo la kushangaza wakili huyo atasimama mahakamani na kusema kuwa mteja wake hajatenda kosa (hajaua, hajaiba nk). Na mtuhumiwa huyo itamuachia huru. Mawakili wana kesi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu
 
Mahakama za mitaani hizi ni shida sana. Wanadhani kesi kubwa kama hiyo jaji anafunga watu kwa hisia. Hebu ngoja tujiulize: mtaani ni watu wangapi wanaitwa wachawi au chinjachinja wanyonya damu? Bila shaka ni wengi na unaweza kwenda kwenye jamii ukakuta mtu fulani anaaminika kuwa ni chinjachinja mnyonya damu na karibia watu wote. Je, ni kweli kuwa kuna chinjachinja mnyonya damu?
The court is not your mother.
Kwamba mama yako akihisi una njaa anakupa chakula ule. Mahakama inahitaji uishawishi una njaa na unahitaji kula.
 
ndio maana kuna level za makosa polisi wanakupeleka mahakamani,nyingine wanajua kabisa ni kupotezeana muda na nguvu za kuhudumia wengine,tutasikia tu unatafutwa na ndugu mara baada ya kuonekana mara ya mwisho ktk gari la polisi.

mahakamani kuna kutafsiri sheria,sio kutoa haki.
Unajua madhara ya watu kupotea mikononi mwa polisi? Unawaza uovu mbaya sana kichwani mwako.
 
Kuna kesi moja tandahimba kuna dada mmoja msukuma anafanya kazi halmashauri kwahiyo alichukua pesa milion 20 akampa dogo mmoja amnunulie korosho kwa mfumo wa kangomba, yule dogo hakununua hata kilo moja pesa kazificha mwisho wa siku yule dada kamdai kwa njia ya kawaida dogo anakataa kuwa hawajawahi kupeana pesa wameenda mpaka mahakamani dogo kashinda
dogo kajitafutia matatizo makubwa. na dada alimpa hela kienyeji dogo. pesa ndefu hiyo haitakiwi kupeane kienyeji kisa mnajuana miaka
 
Unajua madhara ya watu kupotea mikononi mwa polisi? Unawaza uovu mbaya sana kichwani mwako.
ili uonekane unajenga hoja yenye mashiko,unatakiwa ukemee watu kupotea,sio polisi pekee hata misituni.
hasa ukizingatia hoja yako kwamba tunajadili MADHARA.

ok madhara ni kama watu kupungua katika jamii,watu kupoteza muda wakiwatafuta badala wafanye shughuli zao nyingine,watu kupoteza imani kwa jeshi la polisi ambayo huwa wanadai haipo pia nk.
 
Wabongo kwa kwenda na upepo hatujambo. Siku ukutwe na kesi umesingiziwa kuua au kubaka ndio utajua wakili wa utetezi kazi yake nini. Mtu hukuwepo kwenye tukio lakini unakomaa kua huyo mama muuaji kwa mambo ya kuona mtandaoni.
Mtoa post unatudanganya kabisa kua huyo mama alishahukumiwa wakati hukumu imetoka juzi.
 
ili uonekane unajenga hoja yenye mashiko,unatakiwa ukemee watu kupotea,sio polisi pekee hata misituni.
hasa ukizingatia hoja yako kwamba tunajadili MADHARA.

ok madhara ni kama watu kupungua katika jamii,watu kupoteza muda wakiwatafuta badala wafanye shughuli zao nyingine,watu kupoteza imani kwa jeshi la polisi ambayo huwa wanadai haipo pia nk.
Sahihi
 
Kesi ya huyu dada wa kigamboni iliniuma, hukumu iliniuma, dada aliuliwa mbele ya mwanaye, sijui huyo mtoto akikua itakuwaje.

Mungu aingilie kati
 
Kama hajui hata hilo jambo la wazi kabisa hayo mengine huoni kuwa nayo ni uongo? Wengi ya wanaohoji hii hukumu ukiwauliza, hawajui hata mwenendo wa kesi ulivyokuwa.
Acha kutetea rushwa ya wazi. Dosari ndogo ya maelezo haishindi ushahidi uliotolewa.

Kama Jaji wa kesi hii ni ndugu yako mwambie tu asubiri hukumu ya Mungu.
 
Katika kesi za jinai, dosari na mashaka katika ushahidi wa DPP ndiyo humwachia huru mtuhumiwa.

Haijalishi ushahidi una nguvu kiasi gani, bali ushahidi una mashaka kiasi gani.

Mtaimba sana na wanasheria lakini ukweli ndiyo huo kwamba mtuhumiwa hafungwi kwa ushahidi wenye shaka.
 
Kesi za mauaji bila kuwepo eyewitness ni ngumu sana kumfunga mtu kuna upenyo mwingi wa mtu kuachiwa huru na wengi sana huwa wanashinda na wanarudi uraiani na kuua ameua kweli, kinachowafanya wateseke ni kesi kutokuwa na dhamana tu inambidi mtu akae muda mrefu mahabusu lakini mwisho wa siku wengi hawafungwi

Watu huwa wanatafuta kwenye upenyo ni wapi ushahidi hauna nguvu ndo hapo hapo wanapitia na kuachiwa huru tena ukiwa na pesa ndo rahisi kabisa
 
1. Mara ya kwanza Kesi iliyosumbua sana, ya yule mmiliki wa mabasi maarufu ya J Four(J4) ya kuwaua wadeni wake kwa kuwapiga risasi, mpaka kuhukumiwa kufungwa maisha(kama sijasahau ilikuwa kunyongwa hadi kufa) ambayo kiuhalisia ni kweli jamaa aliwaua watu wale(alikiri kuhusika), Wakili huyu kwa kuwa anafahamu namna alivyo na mtandao mkubwa wa mahakimu akaingilia kesi ile na kesi kuanza upya, na kwa dalili zilizokuwepo ni kwamba yule jamaa(J4) alikuwa anaelekea kushinda kesi(sijui kama hukumu ilishatoka maana niliondoka Tz, nikaacha kufuatilia) hivyo roho za wale waliouawa zikawa zimedhulumiwa kwa kujuana na nguvu ya pesa.

2. Kesi ya mke wa marehemu Bilionea Msuya,
Baada ya mauaji ya dada wa marehemu bilionea Msuya, mama wa mtoto mmoja na aliyekuwa akifanya kazi Wizara ya Fedha, kuuawa kwa kuchinjwa kama kuku, Mke wa marehemu bilionea Msuya alikiri kuhusika na mauaji yale kwa kigezo kuwa marehemu(dada wa bilionea Msuya) alikuwa akimsumbua sana kwenye mirathi, hivyo akahukumiwa kifungo cha maisha kama sijasahau

Ni yule yule wakili kuingilia kesi hiyo ambayo awali mtuhumiwa alikiri kuhusika na mauaji hayo, baada ya muda na wakili huyo kuchezesha kama kawaida yake, February mwaka huu muuaji kaachiwa huru bila shaka yoyote kua hakuhusika

Ni kesi hii ndiyo inayoibua maswali na kejeli nyingi kwa mahakama zetu na vyombo vya ulinzi na usalama hasa jeshi la polisi upande wa upelelezi, na wengi kuona kua kesi ile haikumtendea haki marehemu dada wa bilionea Msuya ambayo kimsingi ni kweli

Sasa mimi nimekaa na kutafakari sana, kimwili na hasa kiroho, nikajiuliza huyu wakili mwenye koneksheni na majaji mbona ameifanya pesa, koneksheni na elimu yake kama fimbo ya kuwachapia wale wasiofika bei,
Roho za marehemu hao zinalia, familia za marehemu hao zinataabika, watoto wa marehemu hao wanateseka sababu ya kuuawa kwa wapendwa wao, ni nani atazifuta machozi familia hizi, Ee Mwenyezi Mungu ni nani atawafuta machozi watoto wa marehemu hao ambao wengine walikua wakisoma shule nzuri leo hii wanaenda kidumu na mfagio sababu ya kuuawa kwa wapendwa wao na mbaya zaidi ukweli kupindishwa na mhusika wa kupindisha ukweli ni huyu wakili, ninajua nayeye ana watoto ana ndugu na ipo siku hao waovu anaowatetea, roho za marehemu zitamrudia yeye na kizazi chake kwa kua anafanya hivyo si kwa sababu watu hao walionewa bali watu hao wamemlipa pesa ya kutosha ambayo anaweza kugawana na wenzake na kesi ikapindishwa , na kuwashuhudia uongo marehemu hao

Ukweli utabaki pale pale, dunia tunapita, vile unavyowatendea wenzako nawe siku moja utatendewa vivyo hivyo kama si wewe basi kizazi chako. Pesa haijawahi kutosha na haitotosha kamwe, unashuhudia vipi uongo ambao unajua kweli yake, kweli pesa mwanaharamu, Ee Mwenyezi Mungu nijaalie nipunguze tamaa hasa dhidi ya pesa, sijui huyo mtoto wa dada wa Bilionea Msuya atakua na umri gani lakini katika kufikiria kwangu hata akiwa mkubwa ataoneshwa watu wawili waliohusika na kifo cha mama yake, Muuaji(ambaye awali alikiri) na wakili aliyemsimamia na kumtetea kua hakuhusika ilihali anajua kuwa alihusika.

Najua hata watu hao wangefungwa isingewaongezea kitu familia zao lakini kitendo cha wao kufungwa kingeleta ahueni kwa wapendwa wao.

Sijui kwanini kesi ya huyu dada wa bilionea Msuya imeniumiza sana, nimeumia sana, japo nikiri kuwa mimi sikuwahi kuwafahamu watu hao ila nilikuwa interested tu kuona haki ikitendeka kwa kua wauaji walikiri,

Ndugu na rafiki yangu wakili najua unazipenda kesi hizi kwakua zinakupa pesa ndefu kwa wakati mmoja lakini kweli ya mauaji ya watu hao unazijua, ni kesi zenye nguvu za kiroho, naomba nikukumbushe "Karma is a bitch" kama si kwako hata kwa vizazi vyako.

Mungu azitie nguvu familia za marehemu. "Sisi ni wake na kwake tutarejea"
Amina
Sikio lakufa halisikii dawa.

Umeeleza ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli.

Kuna Jaji mmoja ameolewa Butiama, alifanyia maskini mahoka mahakamani, akijua yeye ni mshindi Kila WAKATI, ila miezi michache tulikula Tanga la mtoto wake wakiume aliyepata ajali Arusha na kuzikwa Butiama.

Mungu akamaliza ugomvi na amejifunza kitu.
 
Una maanisha chanzo cha mtoto wa "miguu ya ng'ombe" kufariki kwa ajali hiyo ndiyo sababu?
 
Kesi za mauaji bila kuwepo eyewitness ni ngumu sana kumfunga mtu kuna upenyo mwingi wa mtu kuachiwa huru na wengi sana huwa wanashinda na wanarudi uraiani na kuua ameua kweli, kinachowafanya wateseke ni kesi kutokuwa na dhamana tu inambidi mtu akae muda mrefu mahabusu lakini mwisho wa siku wengi hawafungwi

Watu huwa wanatafuta kwenye upenyo ni wapi ushahidi hauna nguvu ndo hapo hapo wanapitia na kuachiwa huru tena ukiwa na pesa ndo rahisi kabisa
Yes, kwa mfano; kuna jamaa anaiba mke wa mtu. Akajishauri afanye nini kumpata yule mwanamke, akaona akamuuwe mume wa yule mwanamke. Jamaa akaplot mpango wake peke yake bila kumshirikisha mtu yeyote.

Kwa kuwa jamaa anajua ratiba za mume wa yule dada, akamvizia siku moja anarudi usiku wa saa 6. Akaenda kujiseti kwenye kichaka karibu na nyumba ya mhusika. Yeye alikua amepaki bodaboda mbali kidogo akaiweka kichakani pia. Si unajua nyumba zetu hizi umejenga Zingiziwa ndani ndani/Mabwepande huko vichaka kibao. Jamaa alipotokea akampiga risasi nje ya geti lake, alikufa pale pale. Mwamba huyooo akapotea gizani.

Akaenda alipopark chombo yake akasepa kimya kimya. Usiku huo huo majira ya saa 4 aliongea na mke wa marehem na wakaagana vizuri kuwa usiku mwema, usiku mwema mi nalala. Jamaa akaiacha simu yake chumbani, hakutoka nayo. So hata mukitrace mnara wake utasoma alikua nyumbani mida hiyo.

Katika kesi kama hii, polisi hata wafanye nini ni ngumu kumpata muuwaji. Suspect wa kwanza anaweza kuwa mke. Lakini hakuna mahali popote mke ataonekana amehusika kwa sababu hakukuwa na viashiria vya kutoelewana kati ya mke na mume na wala mke ukichunguza simu zake hutaona mazungumzo yoyote ya plan za kuuwawa mumewe.

Katika mazingira kama haya Jamhuri inamfunga vipi mtu?
 
Back
Top Bottom