Kwa nini Tanzania tunaheshimu sana titles?

thanks again and have you

JF-Expert Member
May 11, 2023
230
424
Habarini za jioni? Ningependa kufahamu kwa nini Tanzania tunaheshimu sana titles hasa pale tunapohitaji kuteua Viongozi ,mfano Dr,Prof,Brigedia ,Jenerali nk

Je? Kuna uhusiano uliopo kati ya title na uwezo wa kuongoza?mfano Dr kwa title aliyonayo na kisomo tayari anauwezo wa kiuongozi?

Kama tumeamua kuheshimu titles na kuchagua watu wenye titles ,kwanini ? Tunawapeleka watu sehemu ambazo hiyo specialization zao mfano;

Waziri wa afya yeye ni Dr wa sheria
Waziri wa Elimu ni prof wa Kilimo

Sasa inakuaje mtu amesoma mpk akawa professor wa sheria halafu unamchagua kuwa Waziri wa Michezo?

Wajuzi naomba kuelewa.
 
Mkuu ukiwa mkubwa utapata majibu. Dunia ina mambo mengi na kabla hujafa jitahidi ujue angalau siri 3 za dunia sijasema za Tanzania achana na Tanzania .

Ukubwa ni pamoja na majukumu au kuvuta ndumu wakati mwingine kujitoa akili au kumsoma adui. Pengine ukubwa ni kutii kile unachoambiwa na mwisho unapokuwa huru unajikomboa.

Ukubwa ni pamoja na kuweka maisha yako rehani. Naam ni kuamua kupambana na adui ata kama unahakika ataweza kukushinda!!
Ukubwa ni kumsikiliza adui baada ya kuhisi ana silaha bora kuliko yako. La hasha, je ukubwa ni kupambana bila hata ya kuwa na hakika nini unapambania na utafaidika kwa kiwango gani.

Ukubwa sio umri wala sio urefu. Kamwe sio wingi wa watoto au majukumu. Ukubwa ni kitu adimu.
 
Positions kama Uwaziri sio Technical ndio maana ana Katibu ambae ndio Mtendaji Mkuu uyu kama ni afya ni Muhimu akawa Daktari na Awe na Uzoefu fulani ili awe jicho kwa Waziri ambae yeye ni mtu Kisera(Policy)
 
Mkuu ukiwa mkubwa utapata majibu. Dunia ina mambo mengi na kabla hujafa jitahidi ujue angalau siri 3 za dunia sijasema za Tanzania achana na Tanzania .

Ukubwa ni pamoja na majukumu au kuvuta ndumu wakati mwingine kujitoa akili au kumsoma adui. Pengine ukubwa ni kutii kile unachoambiwa na mwisho unapokuwa huru unajikomboa.

Ukubwa ni pamoja na kuweka maisha yako rehani. Naam ni kuamua kupambana na adui ata kama unahakika ataweza kukushinda!!
Ukubwa ni kumsikiliza adui baada ya kuhisi ana silaha bora kuliko yako. La hasha, je ukubwa ni kupambana bila hata ya kuwa na hakika nini unapambania na utafaidika kwa kiwango gani.

Ukubwa sio umri wala sio urefu. Kamwe sio wingi wa watoto au majukumu. Ukubwa ni kitu adimu.
Ahsante
 
Tanzania mtu akishaiba pesa za wananchi kilichobaki Ni kujipa taitoo. Wanapendelea hii ya u Dr.
Dr. Kibajaji
Dr. Mkerewe wa kuchovya
Dr. Tecno
Dr. Total
Dr. Shitman
 
Back
Top Bottom