Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Nimekuwa nasikiliza kampeni za wagombea urais mbali mbali kunadi watakachokifanya kuboresha hali za Watz walio masikini, lakini sijamsikia mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete akiahidi kwamba akichaguliwa tena safari atayapiga mnada mashangingi ya maafisa wakuu wa serikali ili kuboresha huduma mbali mbali za jamii zilizozorota kama vile afya, elimu n.k. Nilimsikia Dr Slaa na Lipumba kwa nyakati tofauti wakitoa ahadi hizo.
Jee JK anaogopa nini kutoa ahadi kama hiyo iliyo bora? Hata kama ni ahadi tu, kwani ahadi nyingine alizotoa si za kipuuzi kabisa? Au kama kawaida yake, anaogopa kususwa na mafisadi wanaombeba ambao kazi yao kubwa ni kuboresha maisha yao kuliko yale ya wengine wengi walio masikini?