Kwa nini jeshi letu la polisi tusilivunje na kuunda chombo kipya chenye kujua majukumu yake?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Jeshi letu la Polisi limekuwa likilaumiwa kila siku kutokana na utendaji wake mbovu unao pelekea kuonekana kama chombo cha kunyanyasa raia wema wasio na hatiya.Hali hii imesababisha wananchi kukosa imani na utendaji wa jeshi hili unaofanywa makusudi kama mradi mchafu wa kuchuma pesa za raia.

Mambo mengi yamekuwa yakijitokeza na kulichafua jeshi hili.Halina tena sifa mbele ya jamii pamoja na kauli yao mtambuka kuhusiana na dhana ya polisi shirikishi.Wananchi wengi wamekuwa wakinadi maisha yao kwa kuyaweka rehani kukisaidia chombo hiki kupambana na wahalifu lakini mwisho wa siku kwa kupitia jeshi hili siri hizo za wananchi uhanikwa hadharani na kusababisha chuki miongoni mwa raia wema na wahalifu.

Iliwahi kutokea kwa Mbunge mmoja wa zamani kupitia CCM,kuliomba bunge kulivunja jeshi hili na kulifanyia reform lakini alionekana kama hana nia njema kwa jeshi hili.Laiti kama ushauri wake ungetumiwa vizuri hakuna ubishi jeshi letu leo lingekuwa na nidhamu ya hali ya juu.

Wakati mwingine napata wakati mgumu kwa kutafakari ni vigezo gani vinatumika kuwapata vijana wa kujiunga na jeswhi hili ikiwa kila uchafu unaofanywa hapa nchini una baraka za polisi hawa.Matukio yanayo tokea leo hii ya uvunjifu wa amani mengi source huwa ni jeshi la polisi.Leo hii huwezi kuamini japokuwa ndiyo hali halisi,vijana amabo ni askari polisi wanahusika na kila aina ya biashara haramu ndani ya nchi hii.Viongozi wanajua lakini wamekaa kimya ama kwa kuwa na hisa na vijana hao.Unga unaosambazwa miokani hivi sasa supplier dealer wake ni askari polisi,ushahidi upo na centers zao zina julikana.

Kubambikiwa kesi kwa raia wema wasio na hatia ni jambo la kawaida hali inayopeleka kujenga uhasama katika jamii yetu.Una kamatwa na kuwekewa bangi mfukoni,ukifikishwa polisi kama huna pesa za kutoa/kuhonga una bambikiwa kesi ya mauaji.Hali hii imepelekea ule msemo wa unaingia bure polisi lakini kutoka ni kwa pesa kushika kasi na kulichafua kabisa jeshi hili.

Kuna askari polisi waliopewa pikipiki kwa ajili ya kudhibiti uhalifu,lakini mbaya zaidi pikipiki zile zimekuwa na kazi maalumu ya kukusanya pesa kwa kuwakamata raia wasio kuwa na hatia kwa kubambikiwa kesi.Mlalamiko haya yapo, makamanda wa mikoa wanayajua lakini hakuna hatua madhubuti zinazo chukuliwa kudhibiti hali hii kisai cha kuonekana ni mpango maalumu kwa kazi maalumu.

Nikisema niorodheshe kero za jeshi hili la polisi unaweza kuandika kitabu cha kurasa 3000.Cha msingi hapa ni kulivunja jeshi hili na kuunda chombo chenye heshima cha ulinzi kinachoweza kusimamia na kutekeleza sheria pasi na shuruti.Zamani kimbilio la watu wengi lilikuwa ni polisi lakini hali ya leo imebadilika na kusababisha watu kujichukulia sheria mkononi kwa kukosa imani na jeshi hili.

Jeshi hili limekuwa chombo cha kukandamiza demokrasia na kutumiwa kuwadhibiti vyama vya upinzani pasi na majukumu yake kisheria.Hatuwezi kuwa na chombo ambacho kinatumika kimabavu kukandamiza haki za raia na kukubali kutumiwa na watalawa kwa maslahi binafsi.Hatuwezi kuwa na chombo kinacho halalisha ujambazi nchini kwa askari wake kutumika kwenye matukio ya uhalifu bila kufikishwa mahakamani ili hali taarifa zao zipo wazi na zina julikana.

Tunataka jeshi ambalo litathibitishwa na majukumu yake kuwekwa bayana kwenye katiba yetu na nini adhabu yake ikithibitka limekwenda kinyume na matakwa na majukumu yake kikatiba.Ikiwezekana Mkuu wa jeshi la polisi athibitshwe na bunge ili aweze kuwajibika kwa wananchi na kuondoa ushabiki kwa kuwa tu mkuu huyo ameteuliwa na mtu mmoja

Mwisho, amani ya nchi yetu itategemea sana uadilifu na uwajibikaji wa jeshi hili na kuachwa kutumiwa kama chombo cha ukandamizaji kwa kufanya kazi zake bila upendeleo.Kiundwe chombo ambacho kitakuwa na uwezo wa kudhibiti nidhamu ya jeshi hili na kulipa bunge taarifa ili kuweza kuliwajibisha jeshi la polisi.Kiwe chombo cha kweli katika kusimamia ukweli bila kumuonea mtu.Litumike kama taasisi ya ulinzi na usalama wa raia na mali zake na si jeshi la kukandamiza na kuonea wananchi.Serikali iboreshe maisha ya askari hawa kwa kuwapa mishahara mizuri na makazi bora ili ufanisi wa majukumu yake uweze kuonekana.
 
Back
Top Bottom