Kwa nilichokiona leo pale ofisi za PSRS Dodoma, nashauri wawe na call centre ya kushughulikia malalamiko

kyanyangwe

JF-Expert Member
Oct 31, 2018
1,147
2,746
Leo asubuhi nilipigiwa na ndugu yangu yuko mkoa fulani akiniomba niende pale ofisi za psrs nikamsaidie kutatua changamoto flani inayomkabili kwenye account yake.

Nimefika sikukuta foleni kubwa kivile ila nimegundua ni kwa nini simu hazipokelewi.

Cha kwanza simu ni moja tu pale tena ya mezani.

Cha pili anaepokea simu ni mtu mmoja tu na huyo huyo ndiye anakua anasolve issue za watu wanaoenda pale physically so sometimes anapolemewa anaacha kupokea simu makusudi tu.

Pia Simu za malalamiko zinazoingia ni nyingi mno,nimekaa pale karibu nusu saa lakini nimeshuhudia simu karibu 100 zinaingia na jamaa zingine akawa hapokei na wakati mwingine akawa anazima simu makusudi tu.

Nimegundua pia psrs wana uhaba wa wafanyakazi,man power ni ndogo mno sijui ile mitihani ya watu zaidi ya elfu 2 huwa wanawezaje kuisahihisha kwa usahihi ndani ya masaa kadhaa na kutoa majibu.

Pia nimegundua katibu mkuu wa psrs ndiye mzembe Coz kuna issues ndogo ndogo zinazohitaji approval yake ila yeye bado kalala usingizi wa pono.

Ushauri wangu ni kwamba psrs waweke call centre itakayokua inashughulikia hizi kesi ndogo ndogo na sio utaratibu wao wa sasa.
 
Ikifika muda wa kukagua vyeti na kusimamia mitihan watu kibao si wasaidiane na hizo kazi,
Wao kupiga mikwara tu, nilikutana na mrembo alokuwa kilaza wa darasa tukiwa primary, anapiga mkwara huyo, nikwamwomba namba yake kwa ajili ya mawasiliano.

Majibu yakë sasa "Mara wakiniona natoa namba watanifikiria vibaya na stori stori kibao tu" akasepa huko ndani kuendelea na usimamizi wa saili nyingine.

Nikajiuliza huyu amefikaje hapa!!! na majibu yake yanafikirisha sana, sijui alijua nitamwomba majibu, pili nikajisemea huu mchezo wa figisu wanafanya huko kwenye kanzidata yao, pia nikaona hiyo ya kutopokea simu na kutatua matatizo ni moja ya core value yao.

Nia yangu ilikuwa ni kuomba namba kwa ajili ya msaada zaidi, ambapo msaada wa haraka kupitia mawasiliano yao ya kiofisi hayapokelewi kwa wakati.
 
Nakuunga mkono ndugu mm nilienda juzi baada ya kuitwa na haohao watu wa kushughulikia malalamiko, nilipofika nilikuwa na barua ikihitaji ishughulikiwe na wao Cha ajabu nilijibiwa kwa mdomo tu tofauti na nilivyotarajia kwanza karibu watumishi wote walishindwa kuielewa barua mtu mtumishi pale mfano neno not-shortlisted anapata tabu kulitaja ataelewa kiufasaha barua inataka nini, nilijibiwa na mmoja tu nae nikajiaminisha kaielewa barua inataka nini. Huu ni ukweli kwa upande mmoja kwa upande wao wanaweza kudhani tunawadharau hapana, wanatakiwa kutambua watu wanaokuja pale kwa asilimia kubwa wana mawazo na hali ngumu kifedha ni masikini haswa wa kipato wanataka angalau nao waonekane kwenye uafadhali kupitia ajira, mtu una hela zako za kutosha utaenda pale kufanya nini.
 
Back
Top Bottom