Kwa mwezi mzima nimeamua kula Kiazi utamu, Muhogo na Kiazi mbatata kwasababu vyakula vya mafuta na nyama mtaani sina imani navyo, nipo sahihi?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,081
Nipo kikazi mkoa flani pande bush ndani ndani, na kwakweli nilichoona huku mitaani chakula sina imani nacho, Nimezoea kula chakula safi kilichopikwa nyumbani na hata mchana huwa nalia nyumbani ama naletewa chakula kilichopikwa nyumbani, mara kadhaa tunaenda hotelini ama restaurants nzuri na staff wenzangu, ni kama elf 10 hivi kwa lunch pekee ila nachojali zaidi ni ubora wa chakula, wenzangu wanaokula kila siku huko ni kawaida kutumia laki 2 hadi 4 kwa lunch tu.

Sasa huku nilipoenda kikazi sikiamini chakula sababu hakuna hotel ama migahawa safi, migahawa iliyopo ina uswahili mwingi kutaka faida kwa namna yoyote bila kujali afya.

Nyanya wanachanganya na zilizooza tena wanatumia ndoo badala ya sufuria
Nazi wanatumia za kiwandani
Nyama zina kaharufu fulani hivi kauvundo ukiikata kati kati
sahani wanaoshea maji yake yale waliyooshea zingine
mboga za majani zimesinyaa
Mafuta nayo si ajabu yame expire

Ila kuna sehemu karibu na shamba huwa wanauza matunda na wanachoma viazi na mihogo, naona kuna afadhali. huwa naenda na bahasha mpya nachagua vya kuchoma, wanaviosha na baada ya muda inakuwa tayari.

Sijapata matatizo yoyote ya tumbo wala afya, nakula chakula cha ndani, maganda natupa.

Hii vipi wadau.
foto_no_exif (1).jpg
 
Pika mwenyewe ama nenda migahawa yenye hadhi. Maisha magumu sana mkuu, mama ntilie wengi wananunua viungo na mboga zisizo katika hali nzuri ili wapate faida zaidi. Nyanya masalo, mboga majani zilizosinyaa, mafuta ya kupima (machafu + cholesterol), ukichanganya na uchafu wa mazingira ndo basi tena.
 
Back
Top Bottom