Kwa mwendo huu wa CHADEMA kufanya mambo kienyeji na ubabaishaji, kushika Dola tusahau kabisa

Kwa Chadema hii bora niachane na siasa kabisa hadi tutakapopata chama au wapinzani makini na si ulaghai wa mtu mmoja
 
Mkuu wala usingehangaika kujibu ujinga! hujagundua kitu hapo? Umeona kuna kijana yeyote wa Chadema anajibu upuuzi huo? Vijana wa Chadema ni makini sana wako kimya hawajajibu upuuzi! Yaani walevi wa kutwanga vitwanga wa Lumumba wameanzisha uzi kujibizana wao kwa wao hadi aibuu.Achana nao.
Dogo pamoja na maneno yako lakini umechangi uzi huu mara mbili.Ubora wa uzi ni idadi ya wasomaji na sio wachangiaji.La msingi wasome na kuondoka na elimu.
 
Mkuu wala usingehangaika kujibu ujinga! hujagundua kitu hapo? Umeona kuna kijana yeyote wa Chadema anajibu upuuzi huo? Vijana wa Chadema ni makini sana wako kimya hawajajibu upuuzi! Yaani walevi wa kutwanga vitwanga wa Lumumba wameanzisha uzi kujibizana wao kwa wao hadi aibuu.Achana nao.
Hawa jamaa wamedumaa hadi wanadahani wakijiita kada ndo watu watajua ni makada kwelikweli, huu uzi wamauanzisha wenyewe na kujibizana wenyewe.
 
Eti kada wa sisiemu anajiita kada wa chadema makubwa !!! acha nikuache, si Chadema wala chama chochote cha upinzani kitakachoweza kushika dora kwa mwenendo wa KATIBA ILIOPO. Rais wa nchi ndiye Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote nchini + wakati huo huo yeye ni mwenyekiti wa ccm (na mara nyingine na yeye pia ni mgombea akiwa bado ni Rais) + wakati huo huo yeye ndiye anayemteua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. KWA HAYA NA MENGINE KAMA KUNA MPINZANI ANATEGEMEA KUSHINDA URAIS SI TU ANAOTA BALI PIA NI WA KUMPIMA AKILI ZAKE.
Hapo mkuu sijakuelewa,jibu hoja sio za kukimbilia kwa raisi na serikali, embu tujibie hoja hizo hapo juu turidhike
 
Mkuu wala usingehangaika kujibu ujinga! hujagundua kitu hapo? Umeona kuna kijana yeyote wa Chadema anajibu upuuzi huo? Vijana wa Chadema ni makini sana wako kimya hawajajibu upuuzi! Yaani walevi wa kutwanga vitwanga wa Lumumba wameanzisha uzi kujibizana wao kwa wao hadi aibuu.Achana nao.
Ikumbukwe kura si za vijana wa chadema tuu hata hawa wengine mkitupa hoja nzuri mnaweza kutuvua kama samaki wabicho kutoka osheni
 
Mkuu wala usingehangaika kujibu ujinga! hujagundua kitu hapo? Umeona kuna kijana yeyote wa Chadema anajibu upuuzi huo? Vijana wa Chadema ni makini sana wako kimya hawajajibu upuuzi! Yaani walevi wa kutwanga vitwanga wa Lumumba wameanzisha uzi kujibizana wao kwa wao hadi aibuu.Achana nao.
Kwa hiyo mpuuzi ni wewe peke yako ndani ya BAVICHA kwa sababu umejibu. Au wewe ndiyo Bebi wao
 
Sisi tusiofungamana na upande wowote kuna ukweli hapo tena wenye mantiki na mwanachadema yeyote ambae haoni hilo basi anakaugonjwa kanaitwa mBoWe

Watu makini kama wanachama wa cdm mara nyingi hujibu hoja kwa hoja na sio kubeza ila hawawezi kujibu kwa sababu kuna ukweli
 
Kuna mambo yanakera sana tena yanakasirisha.

Siku zote chama chetu kimekuwa kikijinasibu kuwa ni chama makini sana. Siku zote tumekuwa tukiutangazia umma kuwa sisi ni tofauti na CCM ambao tunasema kuwa hawana dira wala mwelekeo. Tunawasema kuwa CCM wamechoka na wameishiwa pumzi.

Sasa haya yanayoendelea ndani ya chama chetu hakika manenomyetu yanatusuta. Nayasema haya kutokana na hoja zifuatazo ambazo kwa hakika zinakera na zinasikitisha.

  1. Haiwezekani Makada watiifu wa CCM kama Sumaye tunawateua kuwa wajumbe wa Kamati Kuu bila hata kuwa wanachama wa chama chetu. Sumaye hajawahi kuwa Mwanachama wa CHADEMA lakini leo hii Mbowe anatutangazia kuwa amemteua kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na sisi wanachama tunaridhika tu.
  2. Lowasa anaitwa kuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu lakini hakuna uthibitisho wowote kuwa aliwahi kuteuliwa na chama kwenye nafasi hiyo, sisi wanachama bado tunakaa kimya.
  3. Chama kimegawanyika makundi makuu hasimu mawili na sisi tunabaki kimya. CHADEMA Asilia na CHADEMA Maslahi.
  4. Nafasi ya Katibu Mkuu inashikiliwa na watu wawili na sisi wanachama hatuhoji. Salum Malimu ndiye pendekezo la Lowasa na Mashinji anaungwa Mkono na Mbowe pamoja na Baregu. Wanachama tupo kimya.
  5. Jukumu la kuimarisha chama Mikoani tunawakabidhi watu ambao hawakijui chama; Lowasa na Salum Mwalimu.
  6. Mbaya zaidi, Lowasa anatangaza kuzunguka nchi nzima kuimarisha chama ameishia Monduli tu kupiga Selfie na Balozi wa Japan nchini. Hakuna Ratiba ya ziara hiyo mikoani na sisi wanachama tumekaa kimya.
Kweli CHADEMA makini ilishaondoka na Zitto na Dr Slaa. Yaliyobaki ni maigizo.
Mbona watu wote wametoka ccm vyama vyingi vimeanza mwaka 1992 kwahiyo ukitaka mtu asiyekuwa mwanaccm lazima awe na miaka ishirini na zaidi kidogo kwahiyo hiyo ndio demokrasia ndugu
 
Hapo mkuu sijakuelewa,jibu hoja sio za kukimbilia kwa raisi na serikali, embu tujibie hoja hizo hapo juu turidhike
Samahani mkuu kama hukunielewa,ngoja nijitahidi ili unielewe, kwanza hoja nimeijibu ila inatakiwa uwe na uelewa wa ziada kunipata. Kama umemsoma mleta mada anajalibu kutuuliza blah blah nyingi za viongozi na mambo yanayohusiana na chama ( nadhani umemsoma sirudii ameuliza nini) je tutaweza siku moja kushinda uchaguzi kutokana na matukio hayo ya viongozi na mwenendo wa chama kwa ujumla ........ SASA MIMI SIKUTAKA KULUMBANA NAE KAMA HIZO BLAH BLAH ZAKE ZIKO SAHIHI AU HAPANA ( maana anajifanya kutuonea huruma kuwa hivo vitu ndio vinavyosababisha sisi CHADEMA kukosa ushindi.) ILA NIMEMWAMBIA VITU AMBAVYO VINAVYOTUFANYA WAPINZANI TUSISHINDE UCHAGUZI NA HATUTOKUJA KUSHINDA KWA SABABU HIZO NA SI HIZO BLAH BLAH ZAKE ANAZOJIFANYA KUZIOROZESHA HAPA.( japo sikuzisema kule ni kama nilikuwa namwambia sababu zetu zinazokwamisha kwa sisi "wapinzani" kushindwa kwenye chaguzi za urais MAANA KAMA NI MATATIZO NDANI YA CHAMA NI KAWAIDA ) Nadhani umenielewa, haswa kama ulianza kumsoma mleta mada HOJA YAKE YA MSINGI ALILENGA KUTUFIKISHIA UJUMBE GANI.
 
Sasa hivi habari ya mjini ni magufuri ukipita mitaan watu walishasahau kama kuna CHADEMA, na wasipoangalia 2020 watapoteza viti vingi vya ubunge watu tunajuta kuchagua wabunge wa chadema.
 
Duni Haji alipotangaza kurudi cuf alisema Chdema wanaishi kama kambale kila mtu ni boss makao makuu wanasema hivi,majimboni wanasema hivi, wilayani nako wana kauli zao hii ndio shida ya kuongozwa na dj afadhali wakati Slaa alipokuwa katibu mkuu alikuwa anamfichia makosa
 
Kwa hiyo mpuuzi ni wewe peke yako ndani ya BAVICHA kwa sababu umejibu. Au wewe ndiyo Bebi wao
Mkuu acha hasira, mambo yanayofanyika ndani ya Chadema wewe kama ni mwanaCHADEMA basi ni kutatua kichama na si kuleta huku kwani hata hao "walioshika dola" chama chao kina shida vile vile, lakini kama wewe ni ccm matatizo/shida za CHADEMA wewe zinakuathiri nini si uwaache wanachama wao watayamaliza matatizo yao wenyewe.
 
Mleta mada hongera kwa mada hii yenye ukweli mtupu ila nikupe pole tu maana nimewapita Bavicha pale uwanja wa wazi wa pale chuo kikuu huria Kinondoni ndo wanajikusanya tayari kwa kuja kwako. Na wanachokuja nacho si kujibu hoja ni matusi tu maana hawana uwezo na ushawishi wa kupinga hayo.
 
Haaaaaaa ukweli mtuupuu chadema ina hesabu siku tuu , karibuni chama makini Act wazalendo
 
Back
Top Bottom