Kwa Mujibu wa Akili za Wana CCM, Ukiwa CCM si fisadi ila Ukihamia chama Pinzani unakuwa Fisadi.

moshdar

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
2,416
1,219
Salaam Wana JF.

Juzi tulitoa uzi, Taz hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-sasa-je-hawa-ni-mafisadi-au-si-mafisadi.html Kiufupi uzi huo ulitolewa kutokana na ukweli kwamba, baada ya lowassa, na wanaccm wenzake, kushutumiwa kwa ufisadi, ni ccm waliouthibitishia umma wa watanzania, kwa maneno yao (yaliyotoka katika vinywa vyao) na kwa vitendo yao (vya kumchunguza na kutomkuta na kosa, Lowassa na wenzake, na pia vya kutompeleka mahakamani Lowassa na wenzake) kuwa Lowassa, na watuhumiwa wenzake sambamba na wafuasi wao, si mafisadi. Uzi huo ulihoji ni kwa nini leo hii CCM wanageuka na wanaililialilia CDM na UKAWA eti lowassa na wenzake wanaohamia cdm na ukawa eti ni mafisadi?!!!

Uzi ulitoa rai kuwa, kwa kuwa inaonekana ama CCM wana visa tu na baadhi ya wana ccm wenzao, ama wamechanganyiwa au wana makusudi flani yasiyo na nia njema dhidi ya wanaccm wenzao, kwa kuwazushia mabaya yasiyo kweli kwa nia ya kuziminya haki zao za kisiasa, basi ni vema, mapema kabisa, CCM watuthibitishie iwapo bado wanasimamia msimamo wao wa awali kwamba, ile list of shame, iliyohusisha vigogo kumi na moja wa ccm, ni bado, kwa mujibu wa msimamo wa awali wa ccm, si mafisadi au kwa sasa ccm wamebadili msimamo?

Lengo ilikuwa ni kutuwezesha kuwa na msimamo mmoja kama Taifa dhidi ya watuhumiwa bila kujali kuwa BADO wapo ccm au wamehamia UKAWA.

Ndugu wana JF, na Watanzania wenzangu, nimesikitishwa sana, na kuogopa sana, baada ya kuona kwamba, katika wanaCCM wote waliochangia uzi huo, rejea uzi uliotajwa hapo juu, hakuna hata mwanaccm mmoja aliyeweza kuonesha ni upi hasa msimamo wa ccm kwa sasa dhidi ya watuhumiwa. Kwa maana nyingine CCM haijui lipi na lipi au kipi ni kipi, hawajui waseme nini au wasiseme nini, hawajui waelekee wapi wala wasielekee wapi. Kifupi hiki chama kimechanganyikiwa, hakijui kinakoelekea yaan hawana mwelekeo na kwa hivyo, kauli ya mwanaccm Horace Kolimba inathibitika, miaka kadhaa baada ya kutolewa, kuwa ccm imepoteza dira na mwelekeo.

Ndugu zangu hii ni hatari sana kwa nchi. Kama nchi, tunaongozwa na chama ambacho kipo "totally comfused", hakiwezi hata kutoa msimamo hata kwa mambo mazito sana kwa Taifa. yaani mpaka leo hii hiki chama hakijui, iwapo ama la, Chenge, rostam, mkapa ni mafisadi au si mafisadi. Mpaka leo hiki chama hakijiui, iwapo ama la, Lowassa, sambamba na robo tatu ya wanaccm wanaomwamini na kumfuata, na hivyo kuwa tayari kumpigia kura popote alipo ili awe Rais wa Tanzania, ni fisadi ama siyo fisadi.

Ama kwa hakika CCM imepoteza dira, CCM imepoteza mwelekeo, CCM haina maono tena.

Hata kwa mambo mazito sana, yenye maslahi mapana na ya wazi kwa nchi yetu, CCM haina msimamo unaoeleweka na ulio wazi kwayo bali wao wanabadilikabadilika, kama bendera fuata upepo, kutegemea na siku ya tukio.

Zaid sana, udhaifu huu wa ccm unathibitisha hoja ya wengi kuwa, tatizo la ufisadi wa ccm si la mwana ccm mmoja mmoja bali ni la mfumo mzima wa ccm ambao umeoza kuanzia juu hadi chini. Kwamba CCM wanafisadi kimfumo na wanalindana kimfumo na kwa hiyo ukiwa ndani yao, na ili kulinda mfumo wao wa kifisadi, wanakufichia uovu wako kwa sababu mfumo wote ni sehemu ya huo uovu wako. Ila ukitoka tu nje yo huo mfumo ovu, na kuwaachia uovu wao ndani ya mfumo wao, na hivyo kuchukua sura mpya ya usafi katika mfumo safi na angavu, basi unageuka na kuwa fisadi mbele ya macho ya ccm!!!!!

ama kweli giza(ccm) na mwanga (cdm/ukawa) haviwezi kukaa pamoja.

Hitimisho la hoja hii ni kutoa rai ya kipekee kwa CDM na UKAWA, kwa wapenda mageuzi/mabadiliko wote kuwa wanayo kazi kubwa na wajibu wa kipekee(moral obligation) wa kuendelea kutoa wito na kuwahimiza wanaccm wote wenye mapenzi mema na Taifa hili, na ambao kwa muda mrefu wamelazimishwa, na mfumo wa kifisadi wa ccm, kutenda ufisadi mmoja au mwingine, sasa watoke sasa nje ya mfumo huo ovu, wajitakase na wajiunge na timu safi, timu ya ushindi, timu ya wanamapinduzi na timu ya ukombozi wa pili, na wa kweli, wa taifa letu. waama, ni jukumu la wanaccm hao wema kutambua sasa wajibu walionao wa kukataa kulazimishwa kuendelea kuwa ndani ya mfumo huo ovu unaosambaratika na kukuputika kwa kasi ya moto wa petroli.

Hatma ya nchi hii haipo tena ccm, hatma ya nchi hii ipo CDM na UKAWA. Mwenye macho haambiwi tizama kwani mene mene tekeli na peres yaani Mungu ameuhesabu ufalme wa CCM na ameupima katika mizani, umepungua, na sasa ufalme huo watapewa CDM na UKAWA.

Tusilale wana CDM/UKAWA bali sasa tuchape kazi kuliko wakati mwingine wowote ule tangu kuanza kwa harakati hizi za kumkomboa Mtanzania....

Aluta continyua.

cc lizaboni, ritz, faiza foxy and Company.
 
Na ukiwa CCM ni fisadi lakini ukiwa CHADEMA/UKAWA ni msafi! Chapati!
baada ya lowassa, na wanaccm wenzake, kushutumiwa kwa ufisadi, ni ccm waliouthibitishia umma wa watanzania, kwa maneno yao (yaliyotoka katika vinywa vyao) na kwa vitendo yao (vya kumchunguza na kutomkuta na kosa, Lowassa na wenzake, na pia vya kutompeleka mahakamani Lowassa na wenzake) kuwa Lowassa, na watuhumiwa wenzake sambamba na wafuasi wao, si mafisadi. Uzi huo ulihoji ni kwa nini leo hii CCM wanageuka na wanaililialilia CDM na UKAWA eti lowassa na wenzake wanaohamia cdm na ukawa eti ni mafisadi?!!!
 
Back
Top Bottom