Kwa mtaji wa Tsh. 400,000/- naweza fanya biashara gani?

Nina mtaji wa sh laki nne je naweza fanya biashara gani kama ujasiriamali ?
Kama uko Dar es salaam

Kesho wahi saa 10 asubuhi pale ilala boma upoint nguo za akina dada huwa zina range 1500-4000, then unakujaa kuuza kitaa 4000-7000 kama unaweza pata kakibanda unaweza ziweka maana nguo za laki 3 ni nyingi sana unakaa asubuhi kibandani ikifika jioni unaanza kutembeza baadhi.

Hakikisha unapita chocho zote nyumba hadi nyumba, saloon, vibanda vya chipsi, kwenye migahawa pia

Unaweza pata uzoefu na mwanga kidogo
 
Nunua jiko kubwa tsh. Makadilio 30,000
Nunua mkaa gunia 1 makadilio tsh. 35,000
Nunua ndoo moja kubwa ya mafuta yakupikia sijui kiasi gani?? Let say tsh. 45,0000

Nunua viungo tangawizi na vitunguu swaumu tsh. 5,000

Na vifaa vingine vinavyoitajika mfano kalai la kukaangia
Anza kwa kununua kuku 3 wakubwa makadilio kila kuku elfu 18,000 jumla tsh. 54,000 chinja tafuta kijiwe kizuri cha jioni kaanga nyama yako yakuku safi na ubora mkubwa punguzo ya bei ili kuvuta wateja,

Wateja wakiongezeka utaongeza idadi ya kuku na wengine wataweka oda nyama ikiwa tamuuuuuuuuuuuuu,

Ubunifu wako utakuongezea thamani kila kheri.
USIITUMIE PESA YOTE KUINGINZA KWENYE BIASHARA LAZIMA UBAKISHE ILI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZITAKAZOJITOKEZA HAPO BADAE
 
Nina mtaji wa sh laki nne je naweza fanya biashara gani kama ujasiriamali ?
Kama upo maeneo ya kanda ya ziwa nenda kisiwa kimoja kinaitwa Goziba kusanya samaki mzigo ukiwa mkubwa nenda kauze samaki na bondo. Hiyo 400,000 nakuhakikishia kwa wiki utapata zaidi ya 100,000 faida.

Ukiachana na hiyo ya samaki chukua dagaa kauzie mwaloni kirumba kakusanye huko bukoba na hii utakuja kutoa ushuhuda hapa tena kuhusiana na dagaa nitafute nikupe maelekezo yote make nailewa sana.

Nenda ushirombo au Simiyu kusanya kuku wa kienyeji afu uje kuuza Mwanza mjini kwa bei ya jumla. Man biashara ipo nyingi sana. But deal na chakula kwa muda huu
 
Asante mkuu umenifungua sana ubarikiwe, narudi Chuo kumaliza degree yangu hii but nikirudi nataka nijichanganye mtaani but saving zangu zinafika laki 9 na nikiuza gheto zima (nimepanga) Total nitafikisha 1.5M na hii laptop nikiamua kuiuza nitakua nmeongezea kwenye mtaji Hope nikianza hiyo biashara itanilipa sivyo mkuu.
Mkuu kuna possibility ya kupoteza hela yote km utakuwa haujipanga vizuri ....ushauri wangu hakikisha una back up plan kwa kuanza let's say nusu ya hyo hela uliyonayo huku nyingine unaiweka pembeni just incase.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama uko dar es salaam

Kesho wahi saa 10 asubuhi pale ilala boma upoint nguo za akina dada huwa zina range 1500-4000 , then unakujaa kuuza kitaa 4000-7000 kama unaweza pata kakibanda unaweza ziweka maana nguo za laki 3 ni nyingi sana unakaa asubuhi kibandani ikifika jioni unaanza kutembeza baadhi..
Mkuu shukrani sana maana hii biashara ya nguo za mtumba za kike nataka niianze pia pesa sio shida shida ni mda tu maana ni muajiriwa. ukiachana na ilala boma Chimbo gani linakuwaga na nguo za kuchagua kwa bei hiyo?? vp karume muda huo vipi?
 
Asante mkuu umenifungua sana ubarikiwe, narudi Chuo kumaliza degree yangu hii but nikirudi nataka nijichanganye mtaani but saving zangu zinafika laki 9 na nikiuza gheto zima (nimepanga) Total nitafikisha 1.5M na hii laptop nikiamua kuiuza nitakua nmeongezea kwenye mtaji Hope nikianza hiyo biashara itanilipa sivyo mkuu.
Mkuu cku siku moja najua kabsa cku moja utakuja kutoa hapa ushuhuda ata mimi narudi kumaliza semester moja ilibaki but kwa huku kanda ya ziwa lazima nirudi make nimefurahia lkzo ya Corona mkuu.
 
Mkuu cku siku moja najua kabsa cku moja utakuja kutoa hapa ushuhuda ata mimi narudi kumaliza semester moja ilibaki but kwa huku kanda ya ziwa lazima nirudi make nimefurahia lkzo ya Corona mkuu.
Asante mkuu mimi niko Mwanza nashindwa kuelewa hii fursa imetupitaje twende tukamalize then tutafutane mkuu.
 
Nunua jiko kubwa tsh. Makadilio 30,000
Nunua mkaa gunia 1 makadilio tsh. 35,000
Nunua ndoo moja kubwa ya mafuta yakupikia sijui kiasi gani?? Let say tsh. 45,0000
Nunua viungo tangawizi na vitunguu swaumu tsh. 5,000.....
Safi sana kuna jamaa baada ya kukosa ajira kwasababu ya corona maana alikuwa mwalimu alianzisha hiyo alisema inalipa kwa siku hakosi elfu 10 faida kwa kuku wanne
 
Back
Top Bottom