Kwa mnaotaka kuja Norway, ujipange kwa vyakula na vinywaji

Per Diem

JF-Expert Member
Mar 28, 2018
2,189
3,713
Moja ya swali ambalo nimeulizwa Sana na wadau humu Ni kuhusu chakula.

Imenibidi nijibu hili kwa kuweka post maana Kuna Mtu amesema yeye amefanya kila aliwezalo kuja na amefanikiwa kwa 90%(anajua mwenyewe kafanyaje) maana yeye ni Mtu anayependa kula na kupiga gambe.

Mimi mwanzo kabisa nilipoingia niseme wazi nilipata changamoto kubwa Sana ya chakula, ulikuwa mtihani Ila baada ya muda nilizoea vyakula vyao na gharama zake taratibu.

Hivyo ni vyema nikaeleza Hali halisi ili Mtu ajue kupoje kwenye suala la chakula huku.
Huku hakuna mama ntilie au mgahawa bubu ambapo utaingia na sh.2000 utaondoka umeshiba, la hasha huku kwenye msosi kuna migahawa ambayo ni ya hadhi kidogo na bei imechangamka ukitaka kula na kushiba andaa 60000 hadi 80000, elfu sitini Hadi elfu themanini.

Karibu vyakula vingi vinapatikana ni pesa yako tu.

Nakutolea mfano tu: kilo ya mchele huku ni Kati ya Tshs 6000 - 8000, na kilo ya nyama ni Kati ya Tshs 70000 - 90000. Yes ni elfu sabini hadi elfu tisini(natamani bongo iwe hivi ili watu waheshimiane)

Hivyo kula wali nyama ni anasa, Mimi chakula changu kikubwa ni mikate, sausage, maziwa, samaki, chips n.k.

Maji ya kunywa Mara nyingi nikienda kwenye kazi nachota ya bomba, ni masafi na mazuri Sana Ila ukitaka kununua ya chupa ni sawa pia.

Kuhusu beer Kuna gharama kidogo Ila bei ni sh.8500 kwa baadhi ya bia na nyingine ni zaidi ya hapo, hadi heineken zipo Ila ni sh 12000. Na pia soda pepsi zipo bei ni humohumo 8500

Suala la mwisho ambalo ungependa kujua ni gharama za ninapoishi, ni chumba kimoja Cha kulala na gharama ni million 2 kwa mwezi.

Nahisi nitakuwa nimejibu maswali ya wadau wengi pamoja na aliyeniuliza.
Chini ni picha moja ya mgahawa nikiwa na maji ya Farris, na vyakula ndani ya huo mgahawa.

Picha nyingine ni bar, huku hata ukiwa bar hakuna kujuana kila mtu afanye mishe zake, hawapendi kabisa kupiga story na mtu wasiyemjua.

IMG_20210314_205528_281.jpg
IMG_20210314_205222_276.jpg
IMG_20210314_204816_272.jpg
IMG_20210314_221835_260.jpg

 
k]Katika pitapita zangu zote majuu, nilichowaapreciate na kuona wametupita mbali sana na hatutakuja kuwakuta ni tabia ya usafi, kila kitu kisafi kuanzia mazingira ya nje, makazi, vyakula, usafiri, magari yote mapya, watu wasafi, hukuti nzi hata sehemu moja utatafuta inzi hutamkuta, hadi hewa safi.

Ukifika kule hata ukila chakula cha kimasikini tu ile kukaa miezi miwili mitatu hadi ngozi inabadilika unanawiri, yaani Mungu kawabariki upako wa maisha mazuri hadi ya hewa inakunawirisha hata kama hali yako ya chini tofauti na bongo mtu ana mihela lakini kakomaa utafikiri anachuna ngozi za watu, ukitoka huko kushuka tu uwanja wa dsm, kuanzia harufu ni tofauti kabisa, mazingira tofauti, watu tofauti hafuru ya umasikini imetapakaa kila mahali. Mungu atusaidie waafrica.
 
Back
Top Bottom