Kwa mara ya kwanza nchi imekuwa na ma-IGP wawili

Mmoja ana cheo cha IJP kisichokuwa na madaraka na mwingine ana cheo cha IJP chenye madaraka,kwa hiyo IJP ni mmoja mwenye cheo chenye madaraka na siyo ma IJP 2 huyo mwingine ni kama kabaki na visoda vinavyofanana na nyota lakini siyo nyota za kicheo zenye madaraka.
IJP NDIO NINI?
 
Ungenisaidia sana kama ungejibu hili kama Rais angemtumbua ungemuita na cheo gani? Ama wakati Dau katolewa kuwa DG wa NSSF kabla ya kupangiwa kazi nyingine ulikua unamuitaje? Ama wewe unadhani kuwa IGP kuna tofauti na vyeo vingine sababu ni polisi???
Umeongeza maswali mengine..Jibu maswali yangu kwanza
 
Huko nyuma tumepata kuwa na Majenerali wawili kwenye Jeshi letu la Wananchi(JWTZ),mmoja akiwa Mkuu wa Majeshi(CDF),Gen Twalipo na mwingine akiwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Gen.Tumainieli Kiwelu.Hivyo sio ajabu nchi kuwa na ma IGP wawili ingawa ni jambo jipya kwa polisi
 
Sheria ya Polisi inaongelea "The Inspector General of Police".

The. Mmoja.

Huyu ni mmoja tu, ni Mkuu wa Polisi.

Soma http://policehumanrightsresources.o...e-Police-Force-and-Auxiliary-Services-Act.pdf

Lazima Watu wakubali kuwa Muundo wa Jeshi la Polisi ulikosewa

Cheo cha IGP Kingebaki cha Madaraka na sio cha Muundo ndio sababu kuna huu mjadala!

RPC au OCD akitumbuliwa Cheo cha Madaraka anabaki na Vyeo vya Muundo sasa changamoto ni kwa IGP kuwa ni cha Madaraka na Muundo
 
Bado ni papa ndugu yangu ndo maana amewekwa chemba akiombea kanisa ili isije leta shida ya kuwa na mapapa wawili wanaotoa amri. Kwa hili tuna uhakika
Ndugu kama hujui jambo unauliza
Madaraka ya pope ni haya
- Askofu wa Vatican
-Kiongozi wa kanisa katoliki duniani
-Kiongozi wa nchi ya Vatican
-Kiongozi wa serikali ya Vatican(curia ya Rome)
Sasa katika majukumu hayo uliwahi kumuona pope emiritua Benedic akiyaperform lini.
Ni sawa na useme Lowasa alipojiuzuru akachaguliwa waziri mkuu mwingine kwamba na Lowasa nae anaendelea kuwa waziri mkuu ila anakua amekaa sehemu na uwaziri mkuu wake.
Kuna vyeo vinakua na mtu mmoja akifa au kujiuzuru hakibaki wazi anachaguliwa/ teuliwa tena mtu mwingine mmoja anapewa madaraka yote mwingine ataitwa mstaafu au aliyejiuzuru au wazamani
 
Huko nyuma tumepata kuwa na Majenerali wawili kwenye Jeshi letu la Wananchi(JWTZ),mmoja akiwa Mkuu wa Majeshi(CDF),Gen Twalipo na mwingine akiwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Gen.Tumainieli Kiwelu.Hivyo sio ajabu nchi kuwa na ma IGP wawili ingawa ni jambo jipya kwa polisi

Vijana hawajui hili ndio sababu wanashangaa

Abdallah Twalipo alipoondolewa Jeshini baada ya Vita ya Kagera aliendelea kuitwa Generali!
 
Lazima Watu wakubali kuwa Muundo wa Jeshi la Polisi ulikosewa

Cheo cha IGP Kingebaki cha Madaraka na sio cha Muundo ndio sababu kuna huu mjadala!

RPC au OCD akitumbuliwa Cheo cha Madaraka anabaki na Vyeo vya Muundo sasa changamoto ni kwa IGP kuwa ni cha Madaraka na Muundo
Mkuu ndo mana tunarudi palepale kuwa tuna ma-IGP wawili kwa sasa. Aliyetenguliwa bado ana cheo cha IGP na mpya na yeye ni IGP ingawa madaraka ni tofauti. Siro ana madaraka na cheo cha IGP ila Mangu ana cheo cha IGP pekee. Wote wanapata mshahara sawa
 
Ndugu kama hujui jambo unauliza
Madaraka ya pope ni haya
- Askofu wa Vatican
-Kiongozi wa kanisa katoliki duniani
-Kiongozi wa nchi ya Vatican
-Kiongozi wa serikali ya Vatican(curia ya Rome)
Sasa katika majukumu hayo uliwahi kumuona pope emiritua Benedic akiyaperform lini.
Ni sawa na useme Lowasa alipojiuzuru akachaguliwa waziri mkuu mwingine kwamba na Lowasa nae anaendelea kuwa waziri mkuu ila anakua amekaa sehemu na uwaziri mkuu wake.
Kuna vyeo vinakua na mtu mmoja akifa au kujiuzuru hakibaki wazi anachaguliwa/ teuliwa tena mtu mwingine mmoja anapewa madaraka yote mwingine ataitwa mstaafu au aliyejiuzuru au wazamani
Mtu yeyote atakayesoma sheria ya Polisi (nimeweka link hapo juu) ataona kuna IGP mmoja tu.
 
Mkuu ndo mana tunarudi palepale kuwa tuna ma-IGP wawili kwa sasa. Aliyetenguliwa bado ana cheo cha IGP na mpya na yeye ni IGP ingawa madaraka ni tofauti. Siro ana madaraka na cheo cha IGP ila Mangu ana cheo cha IGP pekee. Wote wanapata mshahara sawa

Wangetakiwa watofautishe Kama Jeshi la Wananchi Tanzania

Kuna Generali na Chief of Defence Force

Ikitokea CDF Mabeyo katumbuliwa atabaki na Cheo chake cha Muundo cha Generali na huyo
Mpya atakuwa CDF lakin kwa Polisi hili hawana walichanganya Cheo cha Muundo na cha Utawala na ndio walipojichanganaya
 
Tatizo kuna watu humu wanabisha bila kuweka facts..Wababaki kulaumu tu
 
Mmoja ana cheo cha IJP kisichokuwa na madaraka na mwingine ana cheo cha IJP chenye madaraka,kwa hiyo IJP ni mmoja mwenye cheo chenye madaraka na siyo ma IJP 2 huyo mwingine ni kama kabaki na visoda vinavyofanana na nyota lakini siyo nyota za kicheo zenye madaraka.
IJP NDIYO CHEO CHA JESHO GANI MKUU MBONA HII MPYA
 
Vijana hawajui hili ndio sababu wanashangaa

Abdallah Twalipo alipoondolewa Jeshini baada ya Vita ya Kagera aliendelea kuitwa Generali!
Kuwa Jenerali wa Jeshi si kuwa CDF. Kunawezekana kuwa na MaGenerali wengi Jeshini lakini CDF mmoja.

Polisi kuwa IGP ni kuwa Mkuu wa Polisi. Na huwezikuwa na wakuu wa polisizaidi ya mmoja.

Someni sheria ya polisi hapo juu imeeleza.
 
Hizo Sheria unazotaka tusome ndio tunazi challenge

IGP kuwa Cheo cha Muundo na hapo hapo kuwa cha Madaraka ni Makosa ya ki binadamu yaliyofanyika

JWTZ walitambua CDF ni Cheo cha Madaraka ndio sababu hakipo Kwny Muundo wao

Ilipaswa muundo wa Jeshi la Polisi kuisha kwny Kamishna na IGP kiwe ni Cheo cha Madaraka pekee sio na cha muundo
 
Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu tumekuwa na maIGP wawili. Mmoja amepewa madaraka ya kuwa mkuu wa jeshi la polisi na mwingine amevuliwa madaraka hayo lakini amebaki na cheo chake.

Wengi hawajui kuwa IGP ni cheo na sawa na vyeo vingine kama Inspekta wa polisi au Mrakibu wa polisi au Koplo. Tofauti ni kwamba vyeo vya chini vinaweza kushikwa na watu wengi lakini cheo cha juu kabisa ambacho ni IGP hushikwa na mtu mmoja tu. Yani makoplo wanaweza kuwa wengi, makamishna wengi, mainspekta wengi lakini IGP mmoja.

Huyo IGP mmoja ndo hupewa madaraka ya kuongoza jeshi la polisi. Kumbuka kuna tofauti kati ya CHEO na MADARAKA. Mtu mwenye cheo cha IGP ndio hupewa madaraka ya kuongoza jeshi la polisi. Sasa kwa mara ya kwanza tumekua na watu wawili wenye cheo kimoja cha IGP.

Tofauti ni kwamba mmoja ameondolewa madaraka ya kuongoza jeshi la polisi, na mwingine kapewa madaraka hayo. Huyu aliyeondolewa madaraka, ameambiwa atapangiwa kazi nyingine. Lakini bado amebaki na cheo chake cha IGP. This means Mangu akiteuliwa balozi atatambulika kama Balozi IGP Ernest Mangu maana cheo chake hajavuliwa. Ni sawa na wale wanajeshi wanaoteuliwa kuwa wakuu wa mikoa, wanabaki na vyeo vyao.

Na kwa kuwa Mangu hajastaafu utumishi, siku akistaafu basi atastaafishwa kwa cheo chake cha IGP. Japo wakati huo anaweza kuwa na madaraka mengine kama ukuu wa mkoa, ubalozi etc.

SWALI: Je ni sahihi kuwa na maIGP wawili kwenye nchi? Yani watu wenye vyeo vinavyolingana japo wana madaraka tofauti. Hii iko sawa au mkuu amechemsha? Maana haijawahi kutokea tangu uhuru. Hebu wale ndugu zetu ambao ni askari watusaidie uelewa kdg.!

Na Malisa G

Vyeo Vya Jeshi La Polisi
  1. Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP)
  2. Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi(DIGP)
  3. Kamishina wa Polisi(CP)
  4. Naibu Kamishina wa Polisi(DCP)
  5. Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP)
  6. Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP)
  7. Mrakibu Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SSP)
  8. Mrakibu wa Polisi(SP)
  9. Mrakibu Msaidizi wa Polisi(ASP)
  10. Mkaguzi wa Polisi(Insp)
  11. Mkaguzi Msaidizi wa Polisi(A/Insp)
  12. Sajini Meja wa polisi(rsm)
  13. Stesheni Sajini wa Polisi(s/sgt)
  14. Sajini wa Polisi(sgt)
  15. Koplo wa Polisi(cpl)
  16. Konstebo wa Polisi(pc)
Hata kama kweli haijapata kutokea tangu uhuru na imetokea sasa, ubaya wake nini?
 
Hizo Sheria unazotaka tusome ndio tunazi challenge

IGP kuwa Cheo cha Muundo na hapo hapo kuwa cha Madaraka ni Makosa ya ki binadamu yaliyofanyika

JWTZ walitambua CDF ni Cheo cha Madaraka ndio sababu hakipo Kwny Muundo wao
Kwa nini unasema IGP ni cheo cha muundo?
 
Kwa nini unasema IGP ni cheo cha muundo?

Kwny Muundo wa Jeshi la Polisi kipo Cheo cha IGP tafuta humu kuna Uzi Jana ulikuwa unajadiliwa

JWTZ hawana Cheo cha CDF kwny Muundo

Utasikia Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania 'Generali' Mabeyo

Lakin utasikia

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro kwa kuwa Muundo na Madaraka wamechanganya n
 
Back
Top Bottom