The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 7,382
- 8,437
Marekani Kupitia Balozi wake Nchini Tanzania amesema Demokrasia ya Kila Nchi lazima iendane na mazingira na tamaduni za Nchi husika.
Balozi alikuwa akizungumza kwenye kikao Cha wadau wa Demokrasia Tanzania..
Kwa msimamo huu wa marekani ni wazi Mabeberu wanamuelewa Rais Samia na kuwatupia virago Wapinzani uchwara.
---
Balozi wa Marekani, Dkt. Michael Battle: Demokrasia ya Tanzania ifanane na Tanzania
Balozi wa Marekani, Dkt. Michael Battle amesema si lazima demokrasia ya nchi moja ifanane na ya nchi nyingine kwani demokrasia inapaswa kuwa ya kipekee iliyoundwa na nchi husika.
Akizungumza katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Demokrasia ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) jijini Dar es Salaam amesema Demokrasia ya Tanzania inapaswa kuzingatia mazingira ya Tanzania.
“Ni muhimu kufahamu kwamba kila demokrasia haionekani sawa, kila demokrasia haipaswi kuonekana sawa, demokrasia lazima iangalie mazingira ya nchi. Demokrasia ya Tanzania haitakuwa mfumo wa utawala wa kifalme, demokrasia ya Tanzania lazima ifanane na Tanzania yenyewe, lazima ionyeshe utamaduni wa Tanzania, lazima iwe ya Tanzania pekee, lazima iwe milki ya Watanzania, lazima iundwe na Watanzania.
Demokrasia ya Tanzania lazima iwe ya kwake yenyewe na hakuna taifa lingine duniani linalo haki ya kuamulia Tanzania jinsi inavyopaswa kuwa,” amesema.
My Take
1. Hii Kauli ni msiba na nyundo ya utosini Kwa Chadema ikipigilia msumari Kauli ya Kinana kwamba Demokrasia na Uhuru lazima uwe na mipaka,matusi sio utamaduni wa Tanzania na kamwe haiwezi kuwa Demokrasia hapa kwetu.
2. USA anabadilo sera ya Nje Ili Kukabiliana na ushawishi unaokua wa Russia na China.