Kwa jinsi AFCON inavyokwenda, sitashangaa underdog team kunyakua taji hilo la Afrika mwaka huu

Mfalme_wa_Nyika

JF-Expert Member
May 24, 2023
391
862
Yaani nchi ndogo zimewaonesha wanaojiona miamba ya soka Afrika kuwa hakuna mwamba wa milele wote ni wachumba tu mbele ya underdog (team ndogo zisizo maarufu au kuonekana na uwezo wa soka).

Timu kubwa kama Misri, Ghana, Tunisia, Cameroon zimegaragazwa na underdogs kama Namibia, Guinea, Msumbiji na Cape Verde nchi ambazo hazipo kabisa ramani ya soka na wala umaarufu hazina katika kandanda.

Mikeka imechanwa na Favorites mtaani vijana vilio hawana imani tena na timu kubwa zenye majina,
Jana mwenyewe South Afrika kalalishwa chali na Mali mpaka yule Percy Tau kukosa penalti maanake ni ishara kuwa kombe hili linaenda kwa underdog team ambayo watu hawatataraji kuwa inaweza kuchukua.

Kwa upepo huu unavyoenda waarabu hawana lao mwaka huu na sitashangaa nchi yangu Tanzania kumgaragaza Morroco leo mpaka aombe pu.

HUYO HAKIMI LEO ATAKUWA NI MCHUMBA TU MBELE YA SAMMATA
sitashangaa maana underdog upepo ni wao.

Admin hifadhini uzi huu mtakuja kunishukuru badae
Wasalaam

Napenda kuwasilisha.
 
raha ya kuwa underdog ni kuwa ukikandwa ni kawaida wala haiumi ila ukimkanda mtu sio kawaida itawauma mpaka😂
Leo taifa stars hawana chakupoteza ila Morroco wao ndio wana chakupoteza
Kama walishiriki ili watoke kapa hawana cha kupoteza ila kama lengo ni kutaka ubingwa ni dhahiri wana chakupoteza.
 
Shida kocha wetu karopoka mbele ya vyomba vya habr kuwa taifa tunaenda kushiriki tu kuongeza uzoefu huku akishusha lawama kwa Morocco kuwa amewaanda Hadi marefa wao ili Morocco ashinde kwa lazma

Hvyo huyu amroche kaletwa na Nani naomba michuano ikiisha aondoke uko uko aliko afukuzwe

Badala ya kuwajenga wachezaji kiakilia yey anaropoka na kuwatoa mchezoni tukisema. Kma amekula parecent atakataa

Kwa kifupi afukuzwee huyu mtu haraka sana
 
game ni mindset wewe, mpira haushindi uwanjani mpira unaanza na saikolojia...ndio nakuambia morroco na Tanzania alokaa kwenye saikolojia ya ushindi zaidi ni Tanzania leo kuliko morroco mwenye stress
Jidanganye hivyo hivyo, mpira ni dakika 90 uwanjani.
 
Mikeka imechanwa na Favorites mtaani vijana vilio hawana imani tena na timu kubwa zenye majina,
Hili jinamizi ni baya sana, ilichukua mda sana mpaka nikafanikiwa kuliacha
 
Mikocha mingine inakuja kula pesa za bure, si bora wangewaachia uganda,
Badala ya kusema sisi tunaenda kupambana et tunaenda kushiriki tu
 
game ni mindset wewe, mpira haushindi uwanjani mpira unaanza na saikolojia...ndio nakuambia morroco na Tanzania alokaa kwenye saikolojia ya ushindi zaidi ni Tanzania leo kuliko morroco mwenye stress
Kama ni hivyo, Tanzania ingeshachukua world cup mara 10
 
Mimi tangu timu ya waarabu waafrika walipoona wamekuwa vinara world cup wakakana uafrika wao, Niliwachukia. Nawaombea wapigwe kama ngoma ikiwezekana safari hii wasiende world cup kwa tiketi ya afrika. Jana baada ya tunisia kugalagazwa nilipata koke bariiidi.
 
Kama walishiriki ili watoke kapa hawana cha kupoteza ila kama lengo ni kutaka ubingwa ni dhahiri wana chakupoteza.
Kwa uwekezaji wetu kwenye mpira tukijilinganisha na mataifa mengine ni ngumu kuwaza ubingwa, hatuna ubora huo,ila kama wazalendo tunawashabikia wawakilishi wetu na kuwapa morali ya kutupa kile bora zaidi walichonacho
 
Kwahiyo sisi ni washiriki tumeenda kukamilisha ratiba na sio kuonesha ushindani?
 
Mimi tangu timu ya waarabu waafrika walipoona wamekuwa vinara world cup wakakana uafrika wao, Niliwachukia. Nawaombea wapigwe kama ngoma ikiwezekana safari hii wasiende world cup kwa tiketi ya afrika. Jana baada ya tunisia kugalagazwa nilipata koke bariiidi.
Walisema ukweli kwanini mtu akiwa mkweli anachukiwa sisi na wao ni mbingu na ardhi huo ndio ukweli hata mambo yao yamenyooka. Wee angalia Morocco. Misri, Tunisia na Algeria. Wale sio wenzetu.
 
Back
Top Bottom