Kwa yule anayefatilia umoja ulio kuwepo enzi za uongozi wa awamu ya kwanza na akilinganisha na uongozi wa awamu zilizofuata hadi kufikia awamu tuliyo nayo sasa ataona mporomoko mkubwa sana wa umoja wa kitaifa.
Enzi za serikali ya awamu ya kwanza umoja ulikuwa ni nguzo kubwa ya taifa letu, ilifika wakati watanzania wakaitana ndugu kila ulipo pita ulikuwa hukosi kusikia neno ndugu likitamkwa hadi kufikia kuwa kama vile neno hilo kuwa slogan ya taifa letu.
Nakumbuka vita vya kagera vilipotokea umoja na mshikamano wetu kama taifa ulikuwa mkubwa sana, vijana walijitokeza kila pembe ya nchi hii kujiandisha jeshini ili kwenda kulipigania taifa lao kumng'oa nduli na dikteta Iddi Amin Dadaa.
Baada ya hapo yakaja mabadiliko ya mfumo wa kisiasa na tukaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, hadi kufikia awamu ya nne ya uongozi katika taifa letu bado tulikuwa na umoja kwa kiasi fulani, kwani mitazamo ya kisiasa kati ya mtanzania mmoja na mwenzake bado haukuleta uhasama Bali ulizaa kitu kama utani mfulani hivi, ukiwa upande wa pili basi unaonekana kama mtani wa yule aliyoko upande wa pili.
Gafla mambo yakabadilika katika awamu hii ya tano , siasa zikatuletea uadui ambao haujapata kutokea, chama kimoja kikaona kuwa kukosolewa kwao nidhambi , tukaanza kuona utekaji wa wanasiasa wa upinzani ukifanyika kwa kasi kubwa, watu wakipotea na wasionekane tena , watu kufunguliwa kesi zenye mrengo wa kisiasa na hadi kufikia kufungwa jela, tumeshuhudia mashambulizi yenye makusudio ya mauwaji yakilenga wana siasa wa upinzani, na hata wananchi wamefikia hali ya kupoteza upendo wa wao kwa wao kisa eti siasa.
Kama tulikubali mfumo wa siasa wa vyama vingi ni lazima ukubali kuwa itafikia muda fulani wananchi watakuchoka na ukiliona hilo tafuta ni kwanini wamekuchoka na sio kuendesha siasa za kibabe kisa tu eti kwa sababu umeshikilia dola.
Usilazimishe wananchi wakupende wakati wanaona huna jipya la kuwafanyia ,toka Uhuru umeshindwa kuondoa kero ya maji wakati nchi imezungukwa na maziwa makubwa pamoja na mito mikubwa takribani kila pembe ya nchi.
Manung'uniko yamejaa nchi nzima ,ufukara unazidi kuongezeka, wafanya biashara wakubwa wameshindwa kuendelea na biashara kwa sababu mfumo wa kodi sio rafiki kwao, kodi imefanywa kama sehemu ya kukomoa na wala sio sehemu ya kukusanya mapato ya serikali kiuhalali.
Wajasiri amali nao usiseme, mama muuza mchicha mwenye mtaji wa shilingi elfu tano unamlazimisha kununua kitambulisho kinacho zidi mtaji wake.
Kuna haja ya kuwakataa wanao tuletea ubaguzi tuwakemee na kuwazomea popote pale walipo.
Mungu ibariki Tanzania.