Kwa hili TEMESA wamenishangaza sana

Barua ya placement kutoka Utumishi imesema uripoti ndani ya wiki mbili na mwajiri wako atakupangia kazi siyo interview. Ujinga huo wa Temesa
 
Wasalaam wanandugu
Kuna kijana mmoja,amefanya interview za utumishi na akafaulu,utumishi wakampangia TEMESA kama kituo cha kazi kwa kumtumia barua ,baada ya kusubiri kwa wiki chache TEMESA wakampigia simu ya kuitwa kwenye interview nyingine ambayo itafanywa na TEMESA wenyewe ambayo itabidi afaulu ili kuweza kupata kazi:-
Swali je ni sahihi kwa mtu ambaye ameshafaulu interview ya utumishi na kupangiwa kituo cha kazi,kufanyiwa interview nyingine na taasisi husika ili aweze kuajiriwa ? Hii interview ya TEMESA imefanyika leo , yeye pamoja na wenzake ,
Sisi ofisini kwetu jamaa wameletwa na utumishi kuripoti kazini tumewachukua bila ya interiew yeyote.
Tafadhali naomba ufafanuzi ....
TAMESA NI JIPU kuna watu wanafanya kazi kama hawataki, ila kwa hili inawezekana kabsa hawamfanyii interview ya ofisni kwao labda wanataka wampereke kweingine. inabdi awambie.
 
Back
Top Bottom