Kwa hili nimeamini kuwa Polisi wapo kisiasa pia!

Msafiri Kasian

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,133
659
Jana kuna kitendo kilinishangaza Arusha,niliingia kwenye Zahanati ya Polisi pale Central(kwa wale wa Arusha wanafahamu mahali hapa) kwa sababu za kitabu tu.

Nilipoingia pale Zahanati,wahudumu walikuwa ni Polisi waliovalia sare nyeupe(kama traffic police vile) na dada mmoja aliyekuwa amevaa kiraia(t-shirt yake ya Yanga na suruali) ambaye ndiye aliyekuja kunihudumia baadae.

Katika ile sehemu ya kupumzkia wagonjwa huku wakisubiri huduma,kulikuwa na Polisi wengine wa kiume wanne waliokuwa wamevalia sare zao zile za khaki. Hawa walikuwa ni vijana kabisa wanatazama runinga kubwa iliyokuwepo mahali pale huku wakipiga stori.

Ilipofika mida ya saa 6 mchana,taarifa ya habari ITV ikamwonyesha Mbunge wa Arumeru Mashariki,Ndg. Joshua Nassari akiwa Iringa anahutubia hadhira ya watu.
Katika yake,Nassari alikemea kitendo cha yule mtuhumiwa wa mauji(sikumbuki alitaja mauaji ya nani) kutoroka mbele ya Polisi... Ndipo wale polisi nao wakaanza;

Wa kwanza "hawa nao hawana sera kabisa..."
wa pili "hawa kazi kuilalamikia polisi tu..."
mwingine nae akadakia,"hawa ingekuwa kipindi cha Mkapa na Mahita wangekoma...",hapa aliongea akimahanisha rais Kikwete hawezi kuwafanya kitu.
waliendelea na maneno mengine ya kejeli kwa CHADEMA kama vile,hawa wanapiga tu kelele majukwaani na mengine sikuyanukuu kichwani.

Sasa tujiulize,kwa majadiliano kama haya miongoni mwa polisi yanaashiria nini?

Mtazamo wangu: Hawa wakiambiwa,"nenda pale piga risasi wale...",watapiga tu na ndio maana mauaji ya raia wasio na hatia hayapungui,kwasababu polisi wanadhihirisha kutumika kisiasa.
 
Wapo kisiasa wanatiwa kiburi na kikwete na mchimbi,wanaishi kwa rushwa na dhuluma mtaani hakuna anaewakemea na sasa hivi ndio wanatetewa mpaka na jaji ihema na teofil makunga...si ajabu kwa wanayoyasema.
 
wengi wanavyeti feki walikimbia umande wakapigika then wakatafuta vyeti mostly vya dv4,bt kwan kazi yao yahitaj kutumia akil?
 
Tatizo lao ni shule hakuna kwa walio wengi, inasikitisha kuwa na jeshi la vihiyo!
 
Wapo kisiasa wanatiwa kiburi na kikwete na mchimbi,wanaishi kwa rushwa na dhuluma mtaani hakuna anaewakemea na sasa hivi ndio wanatetewa mpaka na jaji ihema na teofil makunga...si ajabu kwa wanayoyasema.

mambo kama haya ndo tunayoshuhudia hadi mahakamani,mahakimu ndo wanaonekana kusahau haki za watu.
 
Tatizo lao ni shule hakuna kwa walio wengi, inasikitisha kuwa na jeshi la vihiyo!

Lakini kumbuka kuna wale waloenda na vyeti saafi kabisa,hawa ni wale ambao upolisi ni wito kwao. Labda wenye matatizo ni wale tu wenye vyeti vya kuungaunga.
 
Hawa jamaa polisi wanaipenda sana CCM kwa kuwa imewaacha wachukue rushwa watakavyo, wawabambikizie watu kesi hadi wachoke, wasiende kupambana na majambazi hadi wakiambiwa majambazi yameondoka na wazurure tu mitaani wakati wa kazi bila sababu za msingi...

Jeshi hili la hovyohovyo linalonuka rushwa kamwe haliwezi kupenda chama kinachodhamiria kuangamiza ufisadi kama CDM kwani wanajua ndio kiama chao. Acha wafu wazikane wenyewe, CCM na Polisi, CDM na wananchi
 
kuna baadhi yao ni wapenzi wa CCM,kuna wengine ni wapenzi wa CDM, kuna wengine CUF. Hivyo mwavumilie tu. Lkini kisheria hawatakiwi kuonesha ushabiki wa vyama.
 
Nani kakwambia kuwa polisi wanataka ma academcians? wao wana vyuo vyao vinavyofundisha taaluma yao sio u profesa! we vipi?! tii mamlaka.
 
inawezekana hata wewe uelewa wako ni mdogo maana lazima watu kama hao wawepo kwenye Jamii, ndio maana kuna unyumbuliko wa kazi hatuzwezi wote kuwa sawa
 
Back
Top Bottom