Kwa haya maagizo ya Mungu juu ya Taifa la Israel (1 Samweli 15: 2-3) Kanisa halina budi kuomba

Eddo Sambai

JF-Expert Member
Aug 1, 2013
2,344
1,771
Ndugu watu wa Jf amani ya Bwana ikae nanyi.

Awali ya yote naomba ninukuu 1Samweli 15: 2 - 3 iwe ndio msingi wa mada yangu.

2 - Bwana wa majeshi asema hivi "Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatendea Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri."

3 - "Basi sasa nenda ukawapige Amaleki, Na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na Kondoo, Ngamia na Punda"

Baada ya nukuu hiyo ya mistari miwili kutoka kwenye Biblia takatifu ambacho ndicho kitabu cha imani cha Wakristo wote pamoja na Wayahudi, naomba niseme yafuatayo.

Moja ya kazi ambazo kanisa imepewa ni kuiombea Israeli na hii nI kwasababu Taifa la Israeli limebarikiwa na yeyote atakayeibariki/kuiombea Israeli basi naye atabarikiwa.

Sasa basi kutokana na matendo pamoja na mienendo inayofanywa na majirani wa Israeli (Arabic Countries) juu ya kuizuru Israeli, pia tukio la tarehe 05/10/2023 kitendo cha kundi la HAMASI kuivamia na kuishambulia na kuuwa makumi ya wana wa Israel.

Je, ni nani anayejua hasira ya Mungu wa Izrael imewaka kiasi gani?
Je, ni nani anayejua ni maelekezo yapi wana wa Israeli waliyopewa na Mungu kufanya dhidi ya maadui zake?

Hayo maswali mawili yananipelekea kusema "KANISA LIOMBE JUU YA ISRAELI"

Ukristo na Uyahudi wote kwapamoja huamini katika Mungu Mmoja. Tofauti yao ni kwamba Myahudi haamini katika Kristo wakati Wakristo huamini kuwa Kristo ndiye njia ya pekee ya kumwendea/kumwabudu Mungu muumba mbingu na nchi.

Israeli ilipewa Sheria (Torati) waitumie ili kuweza Kumwabudu na kumtumikia Mungu.

Kristo yeye ni Imani, Imani sio sheria na kila mwenye kumwamini Kristo basi huyo hana haja ya kufungwa na sheria.

Tuiombee ISRAELI.
 
Waliotunga mashairi ya Biblia na Quran kama kuna moto kwa Mungu basi wao moto wa gesi utawahusu.
 
........ahahahaaaaaaa inafikirisha sana mkuu
eti Mungu kawatuma waue watoto,wanawake mpaka mifugo-aliwaumba ili wauawe.
Mungu yupo wala halina mjadala, lakini dini za Ibrahim tumepigwa ni Utapeli mtupu.
 
Fuata hizo hizo ndio dini rasmi kwa dunia tuliyonayo lakini kwa kiasi na utumie na akili zako.

Uongo ni mwingi ingawa ukweli humo.

Dini ya kweli ni matendo yako mema tu.
Mungu yupo Ila dini za Ibrahim za uwongo ..dini gani tufuate ya huyo Mungu aliyepo!?
 
Ndugu watu wa Jf amani ya Bwana ikae nanyi.

Awali ya yote naomba ninukuu 1Samweli 15: 2 - 3 iwe ndio msingi wa mada yangu.

2 - Bwana wa majeshi asema hivi "Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatendea Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri."

3 - "Basi sasa nenda ukawapige Amaleki, Na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na Kondoo, Ngamia na Punda"

Baada ya nukuu hiyo ya mistari miwili kutoka kwenye Biblia takatifu ambacho ndicho kitabu cha imani cha Wakristo wote pamoja na Wayahudi, naomba niseme yafuatayo.

Moja ya kazi ambazo kanisa imepewa ni kuiombea Israeli na hii nI kwasababu Taifa la Israeli limebarikiwa na yeyote atakayeibariki/kuiombea Israeli basi naye atabarikiwa.

Sasa basi kutokana na matendo pamoja na mienendo inayofanywa na majirani wa Israeli (Arabic Countries) juu ya kuizuru Israeli, pia tukio la tarehe 05/10/2023 kitendo cha kundi la HAMASI kuivamia na kuishambulia na kuuwa makumi ya wana wa Israel.

Je, ni nani anayejua hasira ya Mungu wa Izrael imewaka kiasi gani?
Je, ni nani anayejua ni maelekezo yapi wana wa Israeli waliyopewa na Mungu kufanya dhidi ya maadui zake?

Hayo maswali mawili yananipelekea kusema "KANISA LIOMBE JUU YA ISRAELI"

Ukristo na Uyahudi wote kwapamoja huamini katika Mungu Mmoja. Tofauti yao ni kwamba Myahudi haamini katika Kristo wakati Wakristo huamini kuwa Kristo ndiye njia ya pekee ya kumwendea/kumwabudu Mungu muumba mbingu na nchi.

Israeli ilipewa Sheria (Torati) waitumie ili kuweza Kumwabudu na kumtumikia Mungu.

Kristo yeye ni Imani, Imani sio sheria na kila mwenye kumwamini Kristo basi huyo hana haja ya kufungwa na sheria.

Tuiombee ISRAELI.
Msingi wa Kanisa ni Injili, Injili imeletwa na Yesu Kristo.
Sasa tuanze kupitia maandiko yanasemaje kupitia kwa Yesu Kristo mwenyewe!

Luka 8:20-22​

20 Mtu mmoja akamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje wanataka kukuona.” 21 Yesu akamjibu, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wote wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”

Mama na ndugu zake Yesu walikuwa Wayahudi pia ila hapa anatuambia kuwa Ndugu zake ni wale wanalolisikia neno la Mungu na kulitii kwa maana wale wamfutao yeye.

Israel ni nani?
1700553933257.png

1700554129714.png

1700555245131.png

1700555003313.png

Kimaandiko Yesu Kristo kupitia Injili aliwakataa Wayahudi ambao walishindwa kusikia neno lake, sijajua ni nani hasa aliepenyeza bendera za Israel kwenye makanisa na kufanya kazi ya kuwaombea walewale walimkataa Yesu Kristo! na mpaka leo hawajawahi kumkiri kuwa ndiye mwokozi wao.

Huu ndiyo uelewa wangu juu ya maandiko.

Swali ninalo jiuliza Ikiwa Warumi ndiyo walioshirikiana na Wayahudi kumuua Yesu Kristo! ilikuwaje wakaenda kuweka Makao makuu ya kanisa kwao ilihali wao waliomuua na kuwatesa wafuasi wa Yesu? kwanini makao makuu yasiwe Uturuki ya sasa? maana huku kulikuwa na makanisa saba toka kale
 
........ahahahaaaaaaa inafikirisha sana mkuu
eti Mungu kawatuma waue watoto,wanawake mpaka mifugo-aliwaumba ili wauawe.
Vyote vilivyopo kwenye Dunia hii ni ubatili mtupu na havina thamani Yoyote kwa Mungu isipokuwa wale wanaomwamini na Kumwabudu tu.
Mungu hana hasara yoyote akiamua kuufuta ulimwengu huu, pia usiamini au uamini kamwe hautoweza zuiya Siku ambayo Mungu amepanga kuja kuuangamiza ulimwengu huu
 
Kuna kitu alikuwa anatumia mtunzi wa Biblia . Nafikiri ni kitu cha Arusha au Jamaica
 
Kila naposoma Uzi mtu anatetea asichokijua napata hasira Sana....dini ya kweli ni upendo tu
 
Sasa Huyo Mungu kama ni Mungu wa kweli si angewaumba waisrael peke yao? Mungu gani mpumbavu anasema Kaue watu wote, kwani hao wànaouawa waliumbwa na nani? Ndio mjue kwamba kila jamii ina Mungu wao.
... wa Wamasai yeye aliishawaambia kwamba ng'ombe wote Duniani ni mali ya Wamasai!
😅
 
Wa Tz hangaikeni na Katiba au kakitabu.
Mana hata hao Waizraeli Biblia iko mbali na fantasy zao na inwakera kweli kweli wanaitumia kinyume na mazingira au wakati halisi ili kusapoti uchafu wao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom