Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
- Thread starter
- #21
Katika woooote wachangiaji, wewe ndiyo umesema cha maana. Hakuna conventional war hapo -- humuoni adui yako yuko wapi -- yuko nyuma, mbele au kati kati yenu.
Sawa tulipigana na majeshi Idi Amin kwa ujasiri na kuyashinda. Lakini laiti wakati ule Waganda wangeamua kufanya mambo ya ugaidi humu mwetu sijui ingekuwaje.
Hofu ya kujiingiza Somalia hasa kwa kauli ya wazi ya kiserikali itakuwa imetuweka tayari kwenye mapambano na maharamia hao. Swali ni je, tunao uwezo humu ndani kukabiliana nao endapo wataanza vitu vyao kama jinsi tayari wamefanya huko ndani ya Kenya? Hilo ndilo swali la msingi la kujiuliza -- na siyo maneneno maneno tu ya kishabiki.
Umenena.Hivi watu hawajiulizi kwa nini Wazungu wasiingie Somalia kwa kupeleka askari wa ardhini ili kupambana na hao maharamia? Wanachokifanya ni kuwatumia Wakenya (bila shaka serikali zao zinagharamia kampeni hiyo) kufanya vita kwa niaba yao, yaani proxy war.
Tusisahau kwamba hatua ya serikali ya Kenya kuingiza askari kule ilitokana na kutekwa kwa watalii wa Kizungu kutoka ardhi ya Kenya.
Sawa, ni wajibu wa serikali ya kila nchi kulinda raia wa kigeni walio ndani ya nchi zao, lakini lazima ulinzi huo uwe ndani ya mipaka. Wazungu wanaogopa kupeleka majeshi kwa sababu hiyo hiyo -- kwamba guerrila war ni ngumu kuimudu, kama vile Marekani ilivyojikuta Afghanistan, na sasa inatafuta njia ya kutokea kwa heshima.