Kwa hali hii ya colabo za TZ na Congo naona Diamond anaenda tena kuvunja rekodi yake ya views milioni 10 kwa siku 8

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Wiki hii Tanzania imeng'ara baada ya msanii wake Diamond kuweka rekodi ya kupata views milioni 10 siku ya 8 baada ya kutoa hit song aliyomshirikisha papaa mobimba KOFI OLOMIDE.

Ngoma hiyo inayoenda kwa jina la WAAH ilitoka siku ya tarehe 30 Novemba muda wa saa 6 mchana na ikapata views milioni 10 siku ya tarehe 8 saa sita usiku, hivyo kufanikiwa kuingiza views milioni 10 siku ya 8

Kama picha unavyoiona hapo chini video ilipopata views milioni 10 ilikuwa ni siku ya 8.
1607767235229.png


Kwa staili hii kijana inabidi apewe pongezi nyingi maana sio jambo jepesi kufikisha views milioni 10 ndani ya siku 8.

Lakini kwa upepo huu wa collabo za congo na TZ kufanya vizuri, Diamond atapigilia msumari hapo hapo mpaka kieleweke.

Huenda kwa sasa akimshirikisha awilo Longomba ataweza kufikisha views milioni 10 pengine hata siku ya sita.

Pia wasanii wengine wastuke, wasiefanye mziki kwa mazoea, wajaribu kubadilika na kubuni njia mpya za kuteka soko.

Hongera sana Diamond
 
Views sio kipimo cha ubora wa nyimbo .
Watu tulitaka tu kumuona mopao
pancho boy ngoma mbaya haiwezi kuwa hitsong hata siku moja wewe unaweza usipende lakini watu wengi wakapenda na ngoma ikipendwa na watu wengi ndio inakuwa hitsong hiyo ngoma ukienda club utaisikia kitaani utaisikia, kwenye bodaboda pia na kwenye social media
 
pancho boy ngoma mbaya haiwezi kuwa hitsong hata siku moja wewe unaweza usipende lakini watu wengi wakapenda na ngoma ikipendwa na watu wengi ndio inakuwa hitsong hiyo ngoma ukienda club utaisikia kitaani utaisikia, kwenye bodaboda pia na kwenye social media
Kama ulivyosema kila mtu ana sikio lake
 
Back
Top Bottom