Lung'wando
Member
- Dec 11, 2011
- 43
- 4
Mmoja wa wana JF ametukumbusha ule wakati tulipokuwa tunasoma Elimu ya Utambuzi kupitia Gazeti la Jitambue. Lilitolewa na TK Media. Baada ya kifo cha Munga Tehenan, gazeti nalo likapotea. Hata hivyo nina hakika kwamba Wanachama na Watanzania wengi wamesikitika sana kulikosa Gazeti hilo. Naomba kwa yeyote mwenye kuwa na habari yoyote kuhusu kurudi Gazeti hili atufahamishe. Tumekosa Elimu ya Utambuzi kwa muda mrefu sasa.