Kwa anayetafuta kazi!

Maswa

Member
Feb 17, 2011
50
3
Kwa wale wote wenye taaluma na wasio na taaluma yoyote napendekeza yafuatayo:
1. Tambua kipaji na mtaji wa asili ulionao.
2. Badili mtizamo wa kimaijsha.
3. Kujitambua wewe na thamani yako katika uzalishaji
4. Kutambua umuhimu wa rasilimali uliyonayo i.e Knowledge and Skills are assets for production
5. Buni miradi binafsi ili kutengeneza ajiri ya kudumu isiyo na longolongo.
6. Usitake kutumia mtaji mkubwa anza na mdogo hata kama ni 5,000/=
7. Tekeleza malengo yako
8. Heshimu malengo yako
9. Heshimu malengo ya wengine
10. Usiwe na aibu ktk kazi yako
11. Usiruhusu mtu adharau kazi yako
12. Mpuuze anayedharau kazi yako kwani binadamu tunatofautiana ktk mitizamo.
13. Fanya ufuatiliaji wa biashara yako hatua kwa hatua hasa ktk hatua za mwanzoni.
.
.
.
.
.
.nth

Ukifuata hayo, hautotafuta ajili kwa nguvu kubwa..matokeo yake utakuja kupata kazi amabyo hautotamani kuifanya kwani kazi yako binafsi itakuwa inakulipa vzr na kwa uhuru wa kufanya maamuzi.

Kwa maelezo zaidi nitafute!
 
Kwa 5,000/- ndo unaanza na biashara gani!? Tupe mchanganuo wa jinsi ya kuanza na huo mtaji!?
 
Sory nimemaanisha TZS. 50,000/= (Elfu hamsini tu)

Mchanganuo wake unategemea kwa wakati huo ni biashara gani unataka kuanza nayo..mf. kuna bishara ya mitumba....silazima uanze na nguo nyingi au viatu vingi...., kunabishara za matunda.......n.k ni nyingine ambazo kwa kiasi hicho unawezakujisogeza sehemu fulani!
 
Hizo biashara za elfu 50, mwisho wa siku unakula mtaji.
Kila mara watu wanatoa ushauri wa mitaji ya kuanzisha biashara !!! mbona hamzitaji biashara zenyewe za kufanya zinazoeleweka na za kudumu na zenye faida na maslahi?
 
Sory nimemaanisha TZS. 50,000/= (Elfu hamsini tu)

Mchanganuo wake unategemea kwa wakati huo ni biashara gani unataka kuanza nayo..mf. kuna bishara ya mitumba....silazima uanze na nguo nyingi au viatu vingi...., kunabishara za matunda.......n.k ni nyingine ambazo kwa kiasi hicho unawezakujisogeza sehemu fulani!

Ok kwa 50,000/ tupe mchanganuo wa kufanya biashara ya matunda mf. Maembe
 
mimi naona ningepata 10,000,000 ningefanya kitu other wize bora nibaki kua mzururaji japo nazaraulika kila pahala kwamba nimesoma mpaka univercity nimeishia kuuza duka. mtaani nina wachafua roho ukiwasikiliza utapona kichaa.
 
@Maswa: Ni kweli kabisa kwa uyasemayo, knowledge ndo mtaji mkubwa kuliko vyote, sina mtaji but soon natumaini kuanza kutangaza kazi zangu Na mtumaini Mungu kua nitafanikiwa. I'm get'n ck of being employd.
 
inawezekana kabisa kufanya biashara kwa mtaji wa sh. 5000, lakini hiyo biashara si kubwa ki hivyo ie. biashara pipi, biscuit, karanga n.k tatizo watu wenye degrii wanajidai hawezi :juggle: kufanya biashara ndogondogo kama hizo, lakini ikumbukwe kuwa hata hao mamilionea walianzia chini, swala ni kufanya kazi kwa bidii na kuwa na malengo..... cha ajabu mtu mwenye digriiii unamkuta anamuomba pesa za matumizi mzazi wake ambaye anafanya biashara ya mtaji mdogo kama huo, ila akiambiwa akae kijiweni azungushe hiyo biashara hakubali hataa, eti aibu
 
jamani watu wengi wanao anza na mtaji mkubwa mara nyingi hushindwa coz anakua hawezi kukontro biashara
anza na mtaji mdogo then utaona kama unapata profit au loss.
 
Back
Top Bottom