Kuzini!

Degelingi

Member
Apr 14, 2011
42
0
Hili neno kuzini nje ya ndoa linanipa shida kulielewa, hivi kuna kuzini ndani ya ndoa? naomba tafsiri ya neno hili kuzini!
 
kimsingi inatakiwa isemwe fulani amezini-maana yake amefanya mapenzi na mtu ambaye siyo mke/mume wake ambaye ameolewa.

Tunajichanganya tu utakuta mtu anasema naenda kupata ushauri nasaha. kimsingi alitakiwa aseme naenda kupata nasaha au naenda kupata ushauri, full stop
 
Maandiko yanasema ukitoka nje ya ndoa, baada ya hapo hata ukikutana na mkeo/mmeo ni kwamba utakuwa unazini Kama hujatubu kwa Mungu na kwa mkeo/mmeo.
 
Kuzini nje ya ndoa , ni kwa wale tu walioko kwenye ndoa na kuamua kufanya zinaa.

Hakuna kitu kuzini ndani ya ndoa, kwa maana ya mume na mke kufanya jimahi.

Zinaaa nyingine ni kwa wale ambao bado kuoa/kuolewa au kuingia kwenye fungate ya ndoa, hawa wanaitwa wazinifu tu, ila ahisemwi kuwa ni nje ya ndoa.
 
Hili neno kuzini nje ya ndoa linanipa shida kulielewa,
hivi kuna kuzini ndani ya ndoa? naomba tafsiri ya neno hili kuzini!

Amezini nje ya ndoa - Huyu mtu ni mzinifu lakini hajaoa
Amezini ndani ya ndoa - Ina maana kaoa halafu kenda kuzini
(Tafsiri yangu - mpya)
 
Hawa wanaitwa waasherati nadhani. Uzinzi/uzinifu ni exclusively kwa wanandoa pekee.
Zinaaa nyingine ni kwa wale ambao bado kuoa/kuolewa au kuingia kwenye fungate ya ndoa, hawa wanaitwa wazinifu tu, ila ahisemwi kuwa ni nje ya ndoa.
 
Aziniye na mwanamke hana akili kabisa.
Siongezi wala sipunguzi nawaachieni nyie wataalam , wachambuzi na wajuzi wa Kiswakinge
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom