Kuzimika Kwa Taa Neshno: Serikali Imehuzunishwa Sana

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
[h=3]Kuzimika Kwa Taa Neshno: Serikali Imehuzunishwa Sana[/h] |


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali imehuzunishwa sana na tukio la jana wakati wa mchezo wa fainali ya

Kombe la Kagame kati ya vilabu vya Simba na Yanga ambapo umeme ulikatika ghafla

kwenye Uwanja wa Taifa. Wizara inawaomba radhi wapenzi wa soka wa Tanzania na

Afrika Mashariki na Kati kwa usumbufu uliojitokeza.

Tukio hilo ambalo siyo la kawaida halikutazamiwa.

wananchi, hususani wapenda michezo, kwamba tukio la aina hiyo halitatokea

Aidha, Serikali inawashukuru wananchi wote waliojitokeza uwanjani hapo

kushuhudia mchezo wa jana kwa kuwa watulivu wakati wote wa tukio hilo hadi umeme

Kwa kutambua uzito wa suala hili, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na

Michezo imeunda Kamati ya watu wanne (4) kuchunguza sababu zilizosababisha

umeme kukatika na kukosekana uwanjani hapo. Kamati hiyo itaongozwa na Naibu

Katibu Mkuu wa Wizara, Bi. Sihaba Nkinga. Wajumbe wengine ni Bw. Charles Bagenda,

Mkuu wa Kitengo cha Umeme cha Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Bw.

Mohamed Kiganja, Kaimu Katibu Mkuu, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Bi. Anna

Chungu, Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizarani.

Kamati itakamilisha kazi yake ndani ya siku saba (7) kuanzia kesho tarehe 12

Julai, 2011 na itakabidhi taarifa yake kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na

Michezo, Dkt. Emmanuel J. Nchimbi (Mb).

Wizara inapenda kutumia fursa hii kuzipongeza timu za Simba, Yanga na Ocean

View zilizoshiriki kwenye mashindano ya mwaka huu kwa kuonyesha kiwango kizuri

cha mchezo na nidhamu ya hali ya juu. Aidha, Wizara inaipongeza klabu ya Yanga kwa

Imetolewa na:-

KATIBU MKUU,
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
 
hi taarifa mbona imeandikwa hovyo hovyo. Ni mtu mzima au mtoto kaandika? Sasa tume inachunguza nini? Mbona ni kazi ya kuita watu wawili ofisini wajieleze, nusu saa tu kwisha kazi
 
  • Thanks
Reactions: Aza
hi taarifa mbona imeandikwa hovyo hovyo. Ni mtu mzima au mtoto kaandika? Sasa tume inachunguza nini? Mbona ni kazi ya kuita watu wawili ofisini wajieleze, nusu saa tu kwisha kazi
nusu saa muda mrefu sana just dakika 5!!!! Mkuu utashanga report inakuja na findings kuwa sababu ya jenereta kulipuka ubungo au tanesco ilitangaza mgao then ilikuwa zamu ya uwanja wa taifa!!
 
St. Mbona umeogopa kumalizia habari? Usijali basi nitakusaidia kumalizia hii habari........wizara inaipongeza klabu ya Yanga kwa ushindi mnono. Ila hii ya kuundwa tume imenichekesha sana, kuna memba mmoja alishatabiri kuundwa kwa tume.
 
Serikali yahuzunishwa na kukatika umeme uwanjani lakini haisikitishwi wala kuunda tume kwa sisi wananchi tusio na umeme kwa muda mrefu sasa! Maajabu!
 
mtoa habari ni mtu wa simba katakata maneno mengine haswa yanayo ihusu yanga,ok hakuna haja ya tume jamani hili swala dogo sana manager wa uwanja,na wenzie waachie ngazi mara moja,maana tangu tanesco itangaze mgao walikuwa wapi wasinunue generator?
 
Serikali yahuzunishwa na kukatika umeme uwanjani lakini haisikitishwi wala kuunda tume kwa sisi wananchi tusio na umeme kwa muda mrefu sasa! Maajabu!

wewe ndo umenena,apo sasa hakuna anayejali mana uko wanakoishi wakubwa hawana mgao huu,yani tunapata umeme masaa 2-3 kwa 24 hrs??
na kikwete na ngeleja kimya kabisa,au wanampango wa richmond mpya?
 
Back
Top Bottom