Kuweni makini na matapeli wanaojifanya ni Maafisa wa TRA

Financial Analyst

JF-Expert Member
Nov 27, 2017
1,605
2,748
Hadi sasa nimeshapigiwa simu mara tatu na watu wanaojifanya ni TRA wakiniambia kuwa sitoi risiti za EFD na hawataki kuyafikisha juu kwa hio nimtumie kapesa kakula ili apotezee.

Halafu unakuta jamaa wanajua jina lako, info zako, jinsi ulivyo na location ya duka lilipo. Jamaa wana ustadi wa kuongea kama wana nyadhifa kweli na usipokuwa makini wanakutapeli.

Lakini nilikuja gundua, hawa jamaa wanachukua jina la duka na namba yako kutoka kwenye bango la duka. Mara ya kwanza nilinywea kweli ila namshukuru Mungu sikupanic kwa hio sikutuma pesa yoyote.

KUWENI MAKINI.
 
Back
Top Bottom