"Kuwatungia Sheria Kali Mafisadi Haitasaidia"......Sitta

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Alifafanua kuwa nchini Tanzania walarushwa ni watu wakubwa na wenye fedha nyingi hivyo hata ikitungwa sheria kama inayotumika nchini China ya kuwanyonga mafisadi hawa, haitofanikiwa kwani watatumia fedha zao kuipindisha.

Spika Sitta aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua kongamano la mwaka la wadau wa kuzuia na kupambana na rushwa, lililoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Source: Mwananchi
lowasa sita.jpg
 
sitta punguza siasa wewe kama uwawezi mafisadi waachie wataopambana nao,
watanzania wamechoka maneno matupu
 
Aishauri serikali kutibu chanzo chake



Sitta2%2813%29.jpg

Spika wa Bunge, Samuel Sitta.



Spika wa Bunge, Samuel Sitta, amesema vitendo vya ulaji rushwa nchini vinaongezeka kwa kasi kubwa na kwamba imefika hatua ambapo watu wanaopata utajiri kwa njia za rushwa wanaheshimika katika jamii.
Katika kukabiliana na hali hiyo, Sitta ameishauri serikali ijielekeze kwenye kutibu chanzo cha rushwa badala ya kusubiri kuwakamata wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la mwaka la wadau wa kuzuia na kupambana na rushwa, lililoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru).
Alisema inasikitisha kuona baadhi ya watu wametajirika kwa kula rushwa na sasa wanaonekana mashujaa kwenye jamii.
“Kukamata wala rushwa na kuwafikisha mahakamani si tiba sahihi ya kudhibiti rushwa, dawa ni kwenda kutibu chanzo chake maana hata malaria huwezi kuidhibiti bila kuua mazalia ya mbu,” alisisitiza Sitta.
Alisema kuna umuhimu wa kubuni mikakati shirikishi na endelevu ya kukabiliana na adui rushwa ambayo hudhoofisha maendeleo.
Alisema Tanzania haitaweza kujikwamua na lindi la umaskini, magonjwa, ujinga na uhalifu bila kwanza kutokomeza rushwa. Alisema kukithiri kwa rushwa kumesababisha hata zile nchi zilizojaliwa utajiri na rasilimali nyingi kuendelea kuwa maskini na hatimaye kukumbwa na machafuko.
Alisema hali hiyo inatokana na ukweli kuwa rasilimali huwanufaisha wachache katika jamii na kuwaacha wengi katika minyororo ya umaskini.
Balozi wa Sweden nchini, Staffan Herrstrom, alisema rushwa kubwa kubwa na ndogo bado ni tatizo kubwa kwa nchi nyingi za Afrika na hatua za makusudi hazinabudi kuchukuliwa ili kuikomesha.
Alisema serikali ya Tanzania miaka ya karibuni imejitahidi kwa kiwango kikubwa kupambana na rushwa hasa kwa kutunga Sheria mpya.
Alisema rushwa inasambaa zaidi panapokuwa na mazingira ya usiri na kuwanyima wananchi taarifa.
Alisema polisi na mahakama ndiko kunatajwa mara kwa mara kukithiri kwa vitendo vya rushwa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, alisema mapambano dhidi ya rushwa yatafanikiwa iwapo wananchi watashirikiana na taasisi hiyo kikamilifu.
Mbunge wa Kibaha, Dk. Zainabu Gama (CCM), alisema rushwa inaenea kwa kasi kutokana na mambo mengi ya serikali kufanywa kwa siri siri.
“Kwenye zabuni ndiko hali ni mbaya zaidi, haya mambo ya usiri tusipoyaacha rushwa itaishi hapa milele maana kila kitu top secret top secret,” alisisitiza.
Alisema kwenye mikataba mikubwa nako kumejaa rushwa na wabunge wakiomba kuangalia mikataba hiyo kabla haijasainiwa wanaambiwa kuwa ni siri.
Alisema kuna umuhimu wa kukomesha rushwa katika chaguzi nchini kwani ni dhahiri kiongozi akiingia madarakani kwa misingi ya rushwa hataweza kupambana nayo.
Aliishauri serikali iangalie upya mafao ya wastaafu kwa kuyaboresha kwani watu wanapomaliza utumishi wao wanapewa mafao kiduchu.
“Mtoto anaenda kijijini anakuta baba yake ambaye kastaafu kachoka hana hata senti, sasa na yeye akikabidhiwa ofisi hatataka kuwa kama baba yake, atataka azoezoe ili baadaye aishi maisha mazuri sasa kuondoa hali hii angalau mtu akistaafu awe na kiasi cha kumtosha,” alisema.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaa, Dk. Exavery Rwaitama, alisema ili kurudisha maadili, viongozi wanaoshutumiwa wanapaswa kujiuzulu. Alisema kinga ni bora kuliko tiba hivyo dawa ya kupambana na kutokomeza rushwa ni kuangalia inakoanzia badala ya kusubiri matokeo yake.
“Kiongozi akishutumiwa anapaswa kujiuzulu na si lazima iwepo Sheria ya kuelezea jambo hili, kiustaarabu ukishutumiwa watu wakasema hawana imani na wewe ondoka,” alisema.
“Na Rais akiona mtu wake anashutumiwa shutumiwa anapaswa kumwambia akae kando aendelee na biashara zake,” alisema.
Kuhusu biashara na siasa, Dk. Rwaitama alisema wanasiasa wanaofanyabishara wamekuwa wakitumia nafasi zao kustawisha biashara zao.
Alisema kuna haja ya kuweka muundo utakaotenganisha vitu hivyo ili mtu kama ni mfanyabiashara aendelee na biashara zake na aachane na siasa.
“Ukiwa waziri hata kama biashara yako ni ya ovyo ovyo tu lakini mwisho wa siku itastawi maana utatumia nafasi yako kuistawisha,” alisema.



CHANZO: NIPASHE
 
Huyu bwana Sam aliwahi kusimamia CDA pale Dodoma na mji mpaka leo haujakaa vizuri kama ule wa Abuja ambao ramani yake naambiwa ni ya Dom. Pia amekuwa waziri wa ujenzi. Hivi alipata wapi fedha za kujenga nyumba ya ghorofa moja kule Urambo miaka ya 70/80? Ghorofa lilikuwa moja tu wilaya nzima, yaani nyumba yake? Au anapata kipato cha nguvu ktuoka kwenye firm yake ya sheria? Au ndio mambo ya kuwa kwenye ukoo wa kichifu? Does he practise what he preaches?
 
Back
Top Bottom