masoko makubwa ya katikati ya majiji yapaswa kuwa ardhini na juu kunafanyika shughuli nyingine tofauti na barabara zinapita na majumba yanajengwa.
yaani karibu theluthi moja ya wakazi wa jiji watakuwa wanafanya shughuli zao chini ya ardhi............ na wakimaliza shughuli zao wanakutana na sub-way/metro, inawachukua chini kwa chini hadi huko kimara, sijui gongo la mboto nk na kuacha daladala juu ya ardhi zikiwa nyeupe 24/7 .............. na hii ingepunguza sana msongamano juu ya ardhi............. kama ni mawazo kama hayo, mi naunga mkono ujenzi huo mia kwa mia..............
Ni Kweli kabisa. Hivi JF umekuwa ukumbi wa kuomboleza? Kulaumu na kutukana kutaleta mabadiliko gani? Kama kweli ni great thinkers kama tunavyojinadi tuje na practical solutions kwa mambo tunayoyaona hayafai. Kwa mfano kuanzisha petitions kwenye mtandao na mitaani kupinga wazo la kubomolewa soko la KARIAKOO TUKIJIWEKEA LENGO LA KUKUSANYA SAHIHI MILIONI MOJA. Baadaye hizo petitions ziwasilishwe Ikulu, au City Council, au Bungeni vyoyvyote vile itakavyoonekana inafaa. Kelele tena mtu uko kilometre elfu tano au zaidi hazisaidii kitu. Hutaki watawala wabovu lakini hujiandikishi kupiga kura, wapi na wapi.DUH ...ama kweli tumekosa ma"thinkers".....Hizi kelele wadau zinawafikia?
ni kweli kabisa. Hivi jf umekuwa ukumbi wa kuomboleza? Kulaumu na kutukana kutaleta mabadiliko gani? Kama kweli ni great thinkers kama tunavyojinadi tuje na practical solutions kwa mambo tunayoyaona hayafai. Kwa mfano kuanzisha petitions kwenye mtandao na mitaani kupinga wazo la kubomolewa soko la kariakoo tukijiwekea lengo la kukusanya sahihi milioni moja. Baadaye hizo petitions ziwasilishwe ikulu, au city council, au bungeni vyoyvyote vile itakavyoonekana inafaa. Kelele tena mtu uko kilometre elfu tano au zaidi hazisaidii kitu. Hutaki watawala wabovu lakini hujiandikishi kupiga kura, wapi na wapi.
Ni jambo la kushangaza kwa sababu wengi wanaotumia soko la kariakoo sio wakazi wa kariakoo...kwa hiyo ni wazi kama watumiaji wanao ishi maeneo yaliyo mbali na kariakoo wakijengewa masoko huko waliko hawatakuwa na uhitaji wa kufunga safari kuja kujazana hapo kariakoo. Na hivyo tutakuwa tumetatua tatizo la msongamano na pia kulinda heshima ya majengo yetu ya ukumbusho.
Lakini swali linabaki,huyo alietoa 'mawazo mtindi' kama hayo ya kubomoa soko la kariakoo halifahamu hili wazo la kuwasogezea huduma wana nchi huko waliko ili kupunguza msongamano hapo sokoni kariakoo????
Au ndo ile wanatengeneza naman nyingine ya ulaji....tunakumbuka ni juzi juzi tu tuliambiwa bora tufe njaa lakini lazima ndege ya raisi na rada zinunuliwe, matokeo yake tumeyaona watu walipiga mamilioni ya hela wakatia mfukoni....nhi yetu bwana,kama kajishamba ka bibi!!