Kuuelewa Mgogoro wa CHADEMA na Kuumaliza Kuuelekea 2015

Mwanakijiji,

Nikupongeze kwa makala ambayo natarajia itafungua mjadala mpana utakaoweza kuwaelewesha watu demokrasia na mipaka yake katika kufikia malengo stahiki kwa chama au jumuiya yoyote.

Napenda kufahamu kwa undani zaidi kuhusu mambo yafuatayo:

Nidhamu ya chama na mahusiano na vyama vingine, natarajia utalizungumzia kwenye sehemu ya 2,3 au 4.

Nidhamu ya chama na harakati za kubadilisha uongozi au mwelekeo wa chama( lini na kwa njia zipi wanachama watajiandaa kugombea nafasi katika chama.)

Utekelezaji wa katiba na majukumu ya kila ngazi- majukumu na mipaka yake.
Uandaaji wa viongozi kikatiba ufuate mfumo gani?

Mwisho nataomba ugusie mahitaji na changamoto za technogia katika uwazi na uwajibikaji wa chama.

Kwa sasa naomba kuishia hapa.
 
Ni matumaini yangu, makala itasaidia kunielewesha juu ya tofauti kati ya Nidhamu ya uoga na nidhamu halisi.

Itaelezea kwa kina je kutokutii Amri haramu ni sehemu mojawapo ya nidhamu?.

Je nidhamu ya kijeshi ni Universal?, kwamba hiyo hiyo ndiyo inayotakiwa katika orgization za kisiasa, au hata bureaucratic institutions?.

Na pia Itasaidia kuelezea mchakato wa haki, ni utaratibu gani ambao ni mujarrab wa utoaji haki kwa mwanachama, ili isije ikawa kutofautiana na mwanachama fulani ikachukuliwa kuwa umetofautiana na Chama kizima.

Jeshini hakuana amri HARAMU hata kama MP wako umemzidi vyeti akisema kaa chini ni kaa chini.
 
Hii ni hatua nzuri na hasa kwa wale wanaodhani kuwa siasa zote mwisho wake ni 2015 tu, Tanzania itakuwepo hata baada ya hapo na ndio maana wengine hawaoni aibu kupigania 2015 huku wakishindwa kuangalia miaka 50 iliyopita ambayo kimsingi tumeipoteza kwa zaidi ya 50%!
cc: Mghaka
 
Ninachokupendea MZEE MWANAKIJIJI uwezo ulio nao wa uandishi.

Lakini kuna mapungufu makubwa sana ya uandishi katika makala zako kwa sababu katu hausimami katika jukwaa huru na kungelea jambo ukiwa huma mrengo ulioegemea. Unajaribu (na unafanikiwa sana) kutoa fact ambazo zitaonyesha wema na busara ya upande unaoshabikia huku ukizificha na kutaka kuwaaminisha wasomaji wako kuwa hakuna facts zozote zinazowabeba au kuunga mkono upande unaouchukia/usioupenda.

Sijui kama ni msomaji mzuri wa vitabu lakini ningekushauri usome vitabu vya mtunzi mmoja maarufu sana kwa jina la LEON URIS... huyu ni myahudi raia wa Marekani na mwanahistoria mzuri wa mashariki ya kati hususan izrael/palestine. Una jaribu kuwa kama yeye kwani dhamira yako huwa unaificha na kujitahidi kuongelea facts lakini kwa wenye uelewa kama wako au zaidi ya wako waniona na kuijua dhamira yako tangu sentensi ya kwanza.

NIDHAMU... naona umeamua kulibeba hili neno kama ndio karata yako ya kwanza ya kumsulubu ZZK miongoni mwa karata nyiiingi ulizoziandaa. I DENOUNCE TO THE VERY USE OF THE WORD!!!

Kwako wewe na wenzako mnaohusudu ujinga, nidhamu maana yake ni kukaa kimya!!! kukaa kimya hata kama katiba ya chama inakiukwa!

Kwako wewe nidhamu ni kutohoji matumizi yasiyoeleweka ya mapato ya chama?

Owako wewe nidhamu maana yake ni kukaa, kujikunyata na kuuliwa kisiasa na wapinzani wako bila kujitetea!

Kwako wewe nidhamu ni kukaa kimya hata kama tarehe na muhula wa uongozi wa uongozi uliopo madarakani umeshapita muda wake!

Kwako wewe nidhamu maana yake ni kusimamia matamko ya kipuuzi ya baadhi ya viongozi hata kama matamko hayo yanakiuka katiba ya chama.

Kwako wewe nidhamu maana yake ni kutokuwa huru kama mwanadamu, kwamba kama G.LEMA ana visa na SAID MWEMA kutokana na either historia yake ya kihalifu basi na mwingine nae ajiingize katika mgogoro huo baina ya mhalifu na chombo cha usalama.

MWENYE akili timamu hana haja ya kusoma mwendelezo wa haya makala yako lakini ili kukujibu neno kwa neno tutalazimika kwenda na wewe sambamba mpaka tuone mwisho wa makala zako.

Nidhamu unayoipigania ndani ya chama chako cha kichaga ina tafsiri moja tu mwanakijiji...

Na tafsiri yenyewe ni hii..... usiwe na mitazamo wala mawazo tofauti na MBOWE(samahani hapa namtaja mbowe kama mtu na sio kama mwenyekiti).

Lolote hata kama ni la kipuuzi kiasi gani litakalosemwa na wapambe wa mbowe akina TUNDU LISU, G.LEMA, MSIGWA, SUGU, NASARI ni tamko la chama na hutakiwi kwenda kinyume chake. katiba haifuatwi na yule anayefuata katiba KAMA INAVYOSTAHILI KUFUATWA anaitwa amevunja katiba. ila wale wanaovunja kila siku wanaonekana wanaisimamia.

Jeshini.....siku zote jeshi lina makamnda.. hawa ndio wanaopigana vita kuanzia kwenye makaratasi kabla ya kuvipeleka kwenye medani. waona wanasiasa ndio wanajua wanapigana vita kwa sababu gani na waliobaki wote wanfuata amri.
ZZK ni miongoni mwa makamanda wanaopanga vita mezani, ni miongoni mwa wale walio mstari wa mbele kuvipeleka vita hivi(dhidi ya ccm na ufisadi) mstari wa mbele wa medani. yeye ni miongoni mwa wale wachache wanaojua vita hivi vinapiganwa kwa sababu gani.... mtu kama MSIGWA au SUGU wala hajui sababu ya kupigana vita....

ZZK ameona kwamba zile sababu za kupigana vita zinakiukwa, malengo ya medani yanaelekea kushindwa kufikiwa na kamanda mkuu amezidiwa na ukubwa wa vita (socially, educationally, technologically and internationally).
SIKU ZOOTE AMESIMAMA katika mstari ulionyooka wa kuhakikisha havunji katiba.

Hiyo nidhamu yako unayoiongelea ya kuwaona wale wanaosimamia katiba kuwa ni wakosefu wa didhamu na wale wanaoivunja kuwa ni wenye didhamu ni ushahidi wa double standards na MAHABA yaliyokujaa kwa mangis and puppets na wivu/chuki uliyonayo kwa ZZK and the team.

Bado tunasubiria mwendelezo wa hekaya zako
 
Kuna tatizo la mantiki katika makala mapema kabisa, nayo ni maana nzima ya nidhamu. Nidhamu haijawahi kuwa tabia ya kufumbia macho ujinga na ukweli. Huwezi watu wakabadilisha katiba kinyemela kwa maslahi finyu binafsi halafu ukasema wakae kimya ili waonekane wana nidhamu kwa viongozi. Haiwezekani kutamani kugombea cheo fulani ionekane ni ukosefu wa nidhamu. Your article is simply fallacious hata kabla hujamaliza. Na udhaifu wa uandishi ni pale msomaji anapoweza kupata hitimisho kabla hata ya kufika mwisho. Itawasaidia akina Molemo katika harakati zao za kufifisha demokrasia na kusimika ufalme ndani ya CDM.
 
Wakuu,

Hii hoja ameleta Mwanakijiji ni msingi saana, ni moja ya nakala ukisoma, ikasomwa na ile ya Duru ya Siasa inayo endelea pale Great Thinkers (https://www.jamiiforums.com/great-t...-kambi-ya-upinzani-chadema-3.html#post8060971)Chadema wanaweza kabisa ku reform for the better toka walipo hapa (pabaya) kuelekea kuimarika zaidi. 2015 Siyo mbali.

Kuna members ambae akijibu hoja kwa kuendeshwa na hisia ama ushabiki humshangai sababu hakuna mahala umewahi kuona akijenga hoja hivyo uwezo wake wa kuchambua na kutazama mambo unakua hujui, uchakulia uwezo wake wa kuwakilisha ni mdogo hivyo hashangawi.

Inapotokea hoja ya msingi na makala nzuri kama hii aliyoweka leo Mwanakijiji akaja mzoefu wa Jukwaa kama ZeMarcopolo ama Tuko ambao nawajua vema kwa uchambuzi makini wakiamua wakaweka hoja za ku divert mjadala, huwa nasikitika saana. Na zaidi nawasikitikia Watanzania wengi ambao wanahitaji ukombozi toka kwa wale wenye uwezo wa kuwakomboa lakini badala yake nafasi hiyo inatumika vibaya.

Tuache ushabiki na tubadilike. Tujadilini hoja, tujifunze, na kujifunza kunakuja hata kwa kufuatilia na kuwa msomaji si lazima kila mmoja aka post (hili ni kwa wale wanaojibu kila kitu kwa kuendeshwa na hisia).

DISCLAIMER: Kaka zangu sisemi kua hizi ni tabia zenu, nimegusia sababu hapa ndicho mlichokifanya; ikiwa nimewakwaza naomba in advance mnisamehe.

Mzee Mwanakijiji, this is a great written peace. Looking forward to itakavyoendelea.
AshaDii
Nilipofikia tu mahali unamsifia ZeMarcopolo nikachefuka kabisa na kuacha kuendelea kusoma Bandiko lako.
Huyu Mkunga Mchumia tumbo ni hovyo kabisa..
 
Last edited by a moderator:
Mpaka hapo alipoishia ,,,nimemuelewa sana Mzee Mwanakijiji,hakuna upande wowote alionyesha kuupendelea,,,ametoa mfano mzuri sana wa jeshini,,,,hata katika chama wanatakiwa kuiga mfano huo,,chadema kweli kunamigogoro,,,,na mgogoro chanze chake ni uongozi uliopo kutowafunza nidhamu wanachama wake,,kukubaliana na katiba,,,,,,MWANAKIJIJI,,NATUMAI PIA UPANDE WA CDM UTAGUSIA SWALA LA UKABILA,UDINI,,,
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom